Jumapili, 22 Mei 2016

YANIPASA KUSHUKURU


Somo la leo: Jumapili

YANIPASA KUSHUKURU.

- Kabla sijaendelea mbele zaidi, yanipasa kujua nini maana ya shukrani?

- Shukrani maana yake ni hali ya moyo kuwa na unyenyekevu wa kupokea taarifa yoyote iliyo mapenzi ya Mungu kwangu.



- Shukrani ni maisha ya rohoni kwa sababu shukrani inatolewa na moyo sio akili, hii ina maana moyo wa mwanadamu ndio mwenye uwezo wa kupambanua mambo ya rohoni.

- Inatakiwa nijifunze kutoa shukrani mbele za Mungu sana sana katika nyakati za mapito, kwa sababu katika nyakati za majaribu ndipo ambapo mbingu inatakiwa ishuhudie Imani yangu kwenye use wa Mungu.

- Shukrani Ina sehemu kubwa sana katika Imani kwa sababu huwa inaandaa mazingira ya kulazimisha muujiza kutokea, ki vipi? Ina maana kitendo cha mimi kumshukuru Mungu katika Jambo fulani hata kama sijalipata inaonyeesha dhahiri ukomavu wa kiimani ndo maana Biblia ikasema Neno hili.
 Waebrania 11:1.

- Kitendo cha Mimi kumshukuru Mungu hata Kama sina kwa wakati huo ninaonyesha dhahiri uhalisia na ukomavu wa kiimani.

- Shukrani Ina nafasi kubwa sana katika kuleta hali ya ushawishi kwenye uso wa Mungu kwenye ulimwengu wa Roho ndio maana kuna watu wengine wao ni kubarikiwaga tu hata shida hawazijui, sababu ya baraka hii ni kutambua thamani ya kumshukuru Mungu katika nyakati ngumu kwenye maisha yao.

- Haitakiwi nimhoji Mungu katika muujiza nilio uomba mbele zake Kwamba kwa nini haujatokea bali inatakiwa niendelee kumshukuru Mungu katika ule muujiza niliouomba mbele zake hata Kama haujatokea hiyo ndio Imani ambayo Mungu anataka aione ndani ya watu wanao mwamini na kumtegemea.

- ( Inatakiwa nijifunze kumshukuru Mungu kwa mambo ambayo sijayamiliki bado, katika hili kutapatikana wepesi wa mambo hayo kuwa katika milki yangu, kwa sababu Waebrania 11:1 inasema dhahiri Kuwa Kuwa na Imani ni kuwa na hakika ya mambo yatarajiwayo ni bayana ya mambo yasioonekana.)

- Nikimshukuru Mungu kwa kitu ambacho bado sijabarikiwa ila namshukuru kwamba nimebarikiwa inaonyesha dhahiri kuwa ninamwamini Mungu kwa asilimia Mia moja, kwa hiyo ni vigumu Mungu kuniacha njia panda, ndio maana kitabu cha Ayubu 22:28 inasema wazi.

- Kitu chochote ninachokikusudia ninapo kuwa kwenye uwezo wa Mungu inatakiwa nikitolee sadaka ya shukrani Kwamba tayari nimesha kipokea na muujiza huo utadhibitika.

- Ili niweze kuitetea nafsi yangu mimi kama mimi inatakiwa nifuate kanuni za Neno la Mungu linavyosema.

KANUNI ZA KUTOA SHUKRANI KWENYE USO WA MUNGU.

- Shukrani inatakiwa iwe katika mazingira yafuatayo:-
 1. Shukrani inatakiwa iwe katika mazingira ya Neno yaani katika kumtukuza Mungu kupitia kinywa changu Kwamba amenitendea hiki.
 2. Shukrani inatakiwa iwe katika mazingira ya tendo Ina maana kutoa sadaka

- Ninapo enda Kutoa shukrani kwenye uso wa Mungu inatakiwa nitazame na uzito wa kile ambacho Mungu amenitendea ndio maana ninashauriwa kabla ya kuchukua hatua ya kwenda kumshukuru Mungu inatakiwa nimuulize Mungu ni kitu gani nimtolee kulingana na uzito wa muujiza wa kile Mungu amenitendea.

- Watu wengi tunapoteza miujiza yetu kwa kutokutambua thamani ya kumtolea Mungu sadaka ya shukrani katika muujiza ambao Mungu ameutenda katika maisha yangu.

- Wakristo wengi wana tabia ya kumtolea Mungu shukrani  pale ambapo amefanikiwa tu, lakini ukweli ni Kwamba inatakiwa umtolee Mungu sadaka ya shukrani katika mazingira yote ya kupata na kukosa.

- Ni tendo la kiimani kumshukuru Mungu katika Jambo nililo muomba hata Kama bado sijalimiliki.

- ( Kitendo cha kuwa katika uwepo wa Mungu ni ishara tosha ya mimi kufanikiwa katika kila Jambo ninalo litaka hata kama Mtumishi hajanitamkia wala kuniwekea mkono.)

Hakuna maoni: