26/10/2014
UJUMBE WA LEO
NAMNA YA KUMILIKI
BARAKA ZA MUNGU
Ukweli Mungu anatubariki, lakini kwasababu ya upofu wa
kiroho hatuzioni Baraka hizo zikidhibitika.
Hii ni hatari sana kwa wakristo wengi wanafahamu Baraka za
Mungu ni pesatu,lakini Baraka za Munguzimegawanyika katika sehemu kuu tatu
A)Kuna Baraka za Kiafya.
B)Kuna Baraka za Kiuchumi (Pesa)
C)Kuna Baraka za Uzima wa milele (Wokovu)
Baraka za Mungu haziambatani na maisha ya wakristo wa leo
kwasababu wakristo wa leo wamevaliwa na roho ya Kaini, vilevile roho ya Anania
na Safira,roho ya Kaini, roho ya Anania na Safira huaribu mzunguko mzima wa Baraka
ya mkristo anayechuma na Mungu ,ndio
maana asilimia kubwa ya wakristo waliokoka ni masikini vilevile hawana mpenyo
katika maisha .
Roho ya Kaini tunaisoma kuanzia Mwanzo 4:1-15 roho ya Anania
na Safira tunaisoma katika Matendo ya Mitume 5:1…….
( Wakristo wengi hawazitendei haki karama zilizoko ndani
mwao ndio mwanzo wa maisha yao kuharibika , hili linanidhibitishia utoaji ni
karama vilevile ni imani)
Kwenye uso wa Mungu Kaini aliponzwa na mambo yafuatayo:-
i)Tamaa ya mali.
ii)Wivu, hizi ndizo roho zilizoponza utumishi wa Kaini mpaka
akawa muasi kwenye uso wa Mungu,mpaka sasa ni roho zinazoyagawanya makanisa ya
Mun gu kwasababu wana wa Kaini wamezidi kuwa wengi katika makanisa ya Bwana.
( Hakuna Baraka ya Mungu inayoweza kuingia kwenye maisha ya
mtu anayetoa sadaka iliyo kilema )
Roho ya Kaini ikiyavamia maisha ya mwamini aliyeokoka
huathiri maisha yake katika maeneo yafuatayo :- i) Eneo la kwanza itaharibu Baraka
inayotokana na Mungu katika maisha yake.
ii) Eneo la pili itaharibu mzunguko wa Baraka za wale
wanaomsaidia.
iii) Husababisha na kulazimisha roho ya umasikini katika
maisha ya mtu huyo,vilevile katika uzao wake.
MFANO;Katika hali ya
kibinadamu
Baba
na Mama katika familia wakiwa ni wachoyo hata mtoto watakayemzaa atakuwa ni mchoyo, kwasababu motto anarithi
kutoka kwa Baba na Mama.
Roho ya Kaini huathiri sana Baraka ya mkristo anayechuma na
Mungu.
Ili niweze kuepuka roho ya Kaini inatakiwa niruhusu roho
yangu kuelimishwa na Neno la Mungu,tena katika mazingira yafuatayo:-
i)
Kufundishwa Neno la Mungu (Biblia)
ii)
Kutoa muda wa kusikiliza Neno la Mungu
(Mafundisho)
iii)
Kujifinza hali ya kujisomea Biblia mara kwa mara
usiku na mchana kamaneno aliloagizwa aliloagizwa Yoshua
Yoshua 1:8
Jambo hili ni la kuelewa
sana mkristo anayemwamini Yesu Kristo mwongozo wake ni Biblia.
ANGALIZO :1.Ushauri wa kweli na haki uko ndani ya
Biblia,ukiteleza hapo mzunguko wote wa maisha
Wote unaharibika.
( Nikizitaka Baraka za Mungu lazima nilipe gharama )
Hakuna Baraka ya Mungu inayoweza kuyavaa maisha ya mtu
mwenye asili tatu ndani mwake ambazo ni:-
i) Hila
ii) Wivu
iii)Tamaa
( Inatakiwa nimshukuru Mungu kupitia Baraka ya jirani yangu ambayoMungu
amemsaidia huo ndio upendo).
KIFO CHA WAAMINI.
Kifo cha waamini asilimia tisini na tano duniani kinatokana na kumwibia Mungu sehemu ya kumi
yaani fungu la kumi.
( Mungu ana wivu na sehemu ya kumi kuliko kitu chochote,ndio
maana akasisitiza kwa maandishi kwenye Maandiko
Matakatifu)
Malaki 3:8-12
Sehemu ya kumi ya Mungu mwamini anapoitoa kiuaminifu
humlinda katika mazingira haya:-
a)
Hulinda kazi yake au biashara na mzunguko mzima
wa kipato chake.
b)
Humlinda
afya yake na mzunguko mzima wa familia
yake.
c)
Humuongezea wingi wa siku na maisha marefu.
Kama mimi ni mtoaji wa fungu la kumi kwa uaminifu maana yake
ninairahisisha kazi ya Mungu isone mbele,lakini kama mimi ni mwizi wa fungu la
kumi maana yake ninaididimiza kazi ya Mungu ikwame.
Baraka ya Mungu huja kwa mtu kulingana na mtu anavyokuwa na
bidii ya kutoa.
Maisha ya wakristo walio wengi yanaathirika kwasababu
wanayakataa maarifa ya Mungu na Mungu naye anawakataa wakati wa msiba wao,na
hili jambo kalinena katika maandiko
Mithali 1:24-29.
Ninapomnyima masikini
haja ya moyo wake vilevile nikamnyima Mungu sehemu yake nisitoe kwa
uaminifu,nitakuwa nimetangaza ugomvi na uwepo wa Mungu,kwa hiyo kitakachofuata
katika maisha yake ni majanga tu.
( Mwamini anavyotoa ndivyo anavyojisogeza karibu na uwepo wa
Baraka ya Mungu).
Mkristo anapomuibia Mungu sehemu yake yaani fungu la kumi
huaribu Baraka yake na baraka ya familia kwa ujumla.
NINI INATAKIWA
NIFANYE ILI NIWE MWAMINIFU KWENYE FUNGU LA KUMI
Inatakiwa nitambue kwanza Baraka ninayoipata inatokana na nani, hapo utakuwa
mwanzo wa kuona uzito wa utoaji kiukamilifu kwenye uso wa Mungu.
Jinsi ninavyokuwa mtoaji zaidi katika kuuimarisha ufalme wa
Mungu ndivyo Mungu anavyoniongezea mambo yafuatayo katika maisha yangu:-
i)Wingi wa siku na maisha marefu.
Shauku ya Mungu ni kutuona wakristo waamini tukiuimarisha na kuujenga ufalme wake kupitia
mali zetu, ndio maana katika kipindi cha Mitume mali za wale wakristo waamini
wa kipindi kile zilikuwa ni ushirika
mmoja.
Kama unahitaji Baraka za Mungu kwelilkweli nijifunze
kuuwezesha ufalme wa Mungu.
Kinachowafanya wakristo wasitimize wajibu wao ndani ya
kanisa ni hali ya mazoea na ndiyo inayowaletea laana.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni