SIRI YA IMANI
- Imani ina siri kubwa sana ndani yake ambayo wakristo walio wengi hawajaigundua.
- laiti kama ningeligundua siri ya Imani ningekuwa na hatua nyingine kiroho na kimaisha pia.
- Kuna kitu ambacho inatakiwa tukitazame katika Waebrania 11:1 na hapo ndiko ilipo jificha siri ya Imani, ila leo ni siku ambayo nitagundua siri hiyo na maisha yangu kubadilika.
- Ukweli ni kwamba uhakika ndio Imani, vile vile uhakika ndio msingi wa Imani.
- Uhakika ndio unao ibeba Imani ya mtu kuwa hai, vile vile ndio unao isukuma Imani kufanya kazi, kwa sababu uhakika hutoka katika utu wa ndani wa mtu.
- Uhakika alio nao mtu katika Imani yake ndio unao mtengenezea umbo halisi la baraka zake.
- ( Pamoja na kuombewa lazima kuwepo na juhudi za mtu binafsi katika suala zima la kupata mafanikio au kufunguliwa.)
- Mateso ninayo kumbana nayo leo katika hali ya kimwili ni kwa sababu mimi mwenyewe nimetoka nje ya mnara Wangu unao niongoza kwenye ulimwengu wa Roho.
- Ukitoka nje ya mnara wako unao kuongoza kwenye ulimwengu wa Roho,hata yale uliyo kuwa ukiyapinga utakuta ukiyatenda, hiyo ina sababishwa na nini? Inasababishwa na muunganiko wa mnara ulio kuwepo katika ya mtu na Roho Mtakatifu kukatika.
- Mtu ambaye ametoka nje kwenye mnara wake kwenye ulimwengu wa Roho, hakuna mawasiliano kati ya yeye na Mungu vile vile hakuna muunganiko na baraka za Mungu.
ANGALIZO NO. 1
- Baraka za Mungu zinaporuhusiwa kuja kwenye maisha yangu zikanikuta mimi nimetoka nje na mnara Wangu baraka hiyo inaweza kubebwa na mtu mwingine ambaye yeye yupo katika mnara, kwa hiyo katika jambo hili kunahitajika ufahamu wa kuyatunza mapenzi ya Mungu katika maisha yangu.
- Nikihitaji Neema ya Mungu initembelee inatakiwa nirudi katika mnara Wangu.
- Kutoka nje ya mnara Wangu nina poteza mawasiliano yangu katika ulimwengu wa Roho kati ya mimi na Mungu.
- Maajabu aliyo yatenda Yesu Kristo katika maisha yake ni kwa sababu alikuwa sambamba na mnara wa Roho Mtakatifu ulio kuwa ukimuongoza kwenye ulimwengu wa Roho, Biblia kuna kitu inakifunua Katika. Luka 4:40
- Mkristo ambaye amesimama katika mnara wa Roho Mtakatifu kwenye ulimwengu wa Roho shetani anamwogopa mbele yake hakuna jambo lolote ambalo litashindikana kila jambo atalitatua.
- Ndani ya uhakika hakuna mashaka na mtu yeyote mwenye mashaka katika jambo lolote hana mafanikio. Warumi 14:23,
- Ulinzi wa nguvu za Mungu utasimama katika maisha ya mtu ambaye ameongeza ufahamu
wake kupitia Neno la Mungu, kwa sababu ufahamu wa Neno la Mungu katika maisha ya mwamini ndio unao msaidia mwamini kupata kina cha rohoni, kina cha rohoni anacho Kipata mwamini kutokana na ufahamu ndicho kinacho msaidia kumpa upeo wa kupambanua mapenzi ya Mungu katika maisha yake. Zaburi 91:10-12
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni