Jumapili, 15 Mei 2016

NAMNA AMBAVYO UCHUMI WANGU UNAWEZA KUIMARIKA


Ibada ya Jumapili:

Somo:- NAMNA AMBAVYO UCHUMI WANGU UNAWEZA KUIMARIKA.

- Uchumi una kanuni zake ili uweze kuimarika katika maisha ya mtu.

- Uchumi wangu ili uweze kuimarika itatokana na ubunifu nitakao kuwa nao katika secta ya uwekezaji wa vitu tofauti tofauti, na vile vile inatakiwa nijifunze kuweka akiba.


- Nikiwa Kama mkristo ninaye mwamini Mungu akiba yangu inatakiwa niiweke katika mazingira ya aina mbili.

- Mimi ninaye mwamini Mungu inatakiwa nitambue chanzo cha Baraka yangu ni madhabahu ambayo Mungu ameisimamisha.

- Namna ya kuweka akiba
 (a). Akiba ya kwanza inatakiwa niiwekeze katika madhabahu ya Mungu Kama Neno la Mungu linavyo sema katika  Mathayo 6:21
- Hii inaitwa bank ya kiroho na ukweli ni Kwamba hii bank haifilisikagi milele na milele.

- Chanzo cha Baraka yangu ni madhabahu inayo nilea na hapo ndipo inapo takiwa niwekeze hazina yangu kwa sababu na moyo Wangu upo hapo.

- Mtu ambaye amejiwekea tabia ya kuhifadhi katika akiba ya kiroho shetani awezi kusogea.

- Wakati wa kuwekeza katika akiba ya kiroho usipoKuwa na Imani unaweza kuona unapoteza lakini ni azina isiyo filisika.

- Hakuna dawa ya kukwamka kiuchumi bila kunenepesha akaunti ya kiroho, Kwa sababu mafanikio ya kiuchumi yanatokana na namna ambavyo ulivyo wekeza kwenye uso wa Mungu.
  Malaki 3:8-12

- ( Madhabahu ya Mungu ni chemchem inayogawa vipawa vya Baraka Kwa watu wanao mwamini Mungu, ndio maana inatakiwa hazina yangu iwe katika madhabahu ya Mungu.)
Mfano mzuri katika Biblia; Matendo ya Mitume 10: tuangalie hazina ya Kornelio ilikuwa madhabahu ya Mungu.

- Makimbilio ni kwenye nyumba ya Mungu Kwa hiyo ikiwa Mimi ninamwamini Mungu haitakiwi nyumba ya Mungu iwe na njaa, lazima nyumba ya Mungu iwe imeshiba muda wote.
Mfano mzuri  tukisoma. Malaki 3:10 inaelezea wazi baraka zinazo tokana na akaunti ya kiroho ambayo mkristo ameifungua katika madhabahu ya Mungu.

- (Umasikini  unatokana na uzembe wa mtu binafsi alionao, pia Umasikini ni laana.)

- ( Inatakiwa nichukie maisha ya kuombaomba yanadhalilisha na vile vile yanafunga mtiririko wa Baraka za Mungu mwisho wa siku nitajikuta namtegemea mwanadamu na ni dhambi).

- Katika utafutaji wa pesa kunahitajika ujasiri na kuriski.

- Ili niweze kupata pesa endelevu haitakiwi vitu hivi viwepo ndani mwangu.
 i). Kuwa na hofu na washirika wangu wa kibiashara.

Somo hili litaendelea wiki ijayo ...............

Hakuna maoni: