Somo la leo :
JIHADHARI NA UPOFU WA KIROHO.
ANGALIZO NO.1
Ni bora nipoteze pesa, mali, majumba na magari lakini si kupoteza muunganiko na Roho Mtakatifu, kwa sababu siri zote za KiMungu tunazipata kwa njia ya Roho Mtakatifu).
- (Heshima niliyo nayo inatokana na Roho wa Mungu kunikalia, kwa hiyo ili niweze kudumu na Roho inatakiwa maarifa ya Neno la Mungu yasimame katika moyo wangu).
- Mbinu ya kwanza ambayo shetani anaitumia kuyaharibu maisha yangu ni kuninyima hali ya kujitambua kwenye ulimwengu wa Roho.
- Nikitaka kuwa salama katika maisha ya ucha Mungu inatakiwa nihakikishe niko hai kwenye ulimwengu wa Roho, hii ni sawa na kusema nikae chini ya maono.
- Mtu mwenye maono ndie mwenye uwezo wa kunielekeza kwa usahihi kuhusu Mungu,hili jambo hata Biblia imelifunua Amosi 3:7
- ( Ugumu wa maisha nina usababisha mimi Kwa sababu ya kutoka nje ya mpango wa Mungu ).
- Hata nitabiriwe hayatatukia mpaka pale nitakapo simama sambamba na mapenzi ya Mungu.
- ( Upofu wa kiroho ndio unao sababisha dhambi katika maisha ya mkristo, hata Biblia kuna kitu imezungumzia kuhusiana na upofu wa kiroho Mathayo 15:10-14 ).
- Upofu wa kiroho hauchelewi kukudhalilisha kwa sababu :
i).Huwa unafunga mlango wa ufahamu wa rohoni ambapo ndipo Mungu anatumia kuzungumza na mtu wake.
- Mtu ambaye mlango wa ufahamu wa rohoni una dalili ya kujifunga yuko hivi:
a). Yale aliyo kuwa akiyapinga ndio utamkuta akiyatenda,
ii). Husababisha mwamini kutokuweza tena kupambanua kwenye ulimwengu wa Roho.
- Upofu wa kiroho mara nyingi huleta athari katika maisha ya mwamini kupinga sauti ya Roho wa Mungu bila yeye kujua.
- Kama mimi ni mkristo kwa nini nisipambane kuishi maisha ya rohoni, kwa sababu maisha ya rohoni ndio yanayo msaidia mkristo kutambulikana kwenye uso wa Mungu.
- Upofu wa kiroho huleta athari zifuatazo kwenye maisha ya mkristo:
Athari ya kwanza : humnyima hali ya mtiririko wa Roho Mtakatifu kwenye maombi yake, na kumweka busy katika mambo yafuatayo: kujadili mambo ya wengine, kujadili habari zisizo kuwa na ukweli ndani yake, kuhudhuria vikao visivyo kuwa na utukufu kwa Mungu.
- Mkristo mwenye uwezo wa kuwaza sambamba na mapenzi ya Mungu ni yule ambaye yuko hai kwenye ulimwengu wa roho.
- ( Kuwa hai kwenye Roho ndio kitu cha msingi kwa sababu utu wa nje utalazimishwa kupata mabadiliko ).
- Nikiwa hai katika Roho maisha yangu ya wokovu yatakuwa salama kwa sababu kila kitu kitakuwa chini ya mwongozo wa Roho Mtakatifu.
- (Kusudi la Mungu kwenye maisha yangu nione kama Mungu aonavyo, hapo naweza kusema namwabudu Mungu katika Roho ).
- Nikiwa kama mkristo inatakiwa nihakikishe nina Roho ya maono, kwa sababu Roho ya maono ndio Mungu huitegemea kuleta ujumbe kwa watu wake.
- Roho ya maono hujidhihirisha katika maisha ya mtu anae tembea katika kweli, vile vile ni Neema ya Mungu inayo kuwa juu ya mtu kwa makusudi fulani.
- Roho ya maono katika maisha ya mtu hukua kulingana na mtu anavyo zidi kuongezeka katika ufahamu wa rohoni kupitia Neno la Mungu.
- Nikiwa kama mkristo siwezi kuyaepuka mambo yote kuna mengine nitayapitia hata kama kuna maumivu, haya mambo yaliwakuta watumishi wa Mungu kwenye kitabu cha Danieli 3 yote.
- (Mamlaka za wakristo hazifanyi kazi kwa sababu wakristo wengi hawana ufahamu sawa sawa wa Neno la Mungu ambalo ndilo upanga).
- Mtu mwenye Roho ya maono ana mambo yafuatayo ndani mwake:
a. Hekima
b. Busara
c. Uvumilivu
- Hekima,busara na uvumilivu ni mambo ya msingi kwa mkristo anae anza safari ya wokovu.
- Nikiwa kama ni mkristo ninae mcha Mungu inatakiwa nichunge sana kinywa changu kisitoe kauli za kuwavunja moyo wengine bali kuwafariji na hili lina hitaji hekima ya KiMungu kulitenda.
NINI KIFANYIKE NIBAKI HAI KIROHO
- ili niweze kubaki hai katika Roho inatakiwa nifanye mambo yafuatayo :
a). Kulazimisha Upendo kwa wale walioko kinyume na mimi sambamba na maandiko yanavyo sema katika Warumi 12:19-21
- Kushindwa kusamehe ni kikwazo kinacho weka maisha ya mkristo anae mcha Mungu katika utata.
- Maisha ni rahisi ila ugumu unasababishwa na sisi wenyewe kutoka nje na mpango wa Mungu.
b).Njia nyingine ya kubaki hai katika Roho ni kusoma Biblia Mwanzo mpaka Ufunuo ili nitafute mapenzi ya Mungu ni yapi.
- ( Haki na kweli vipo ndani ya Neno la Mungu, vile vile uzima na uhai vipo pia ndani ya Neno la Mungu ndio maana inatakiwa Neno la Mungu liwe ndo linatoa mwongozo maishani mwangu).
- Nitakapo kutana na shida kuna mambo inatakiwa nijiulize sio kukurupuka kutafuta waombezi waniombee, Mambo hayo ni :-
1. Je kuna kitu ambacho Mungu ananifundisha?
2. Ni Uonevu wa shetani?
3. Ni jaribu ambalo limepangwa kwa ajili hiyo, baada ya kufahamu hapo ndio ninaweza kuchukua hatua zingine kwa sababu mapenzi ya Mungu nakuwa tayari nimesha yajua.
- Maisha ya wakristo yanahitaji kulinda kinywa kuliko kitu chochote kile kwa sababu mlango wa uovu ni kinywa.
-(Ikiwa ninahitaji msaada kwa Mungu lazima niwe wazi kwa Mungu ).
- Ninapo fanya maungamo kwenye uso wa Mungu Roho yangu itaona aibu ya kuurudia uovu eeh Yesu nisaidie , maana ya hii ni nini? Mtu ambaye ameamua kufanya maungamo hana mpango wa kurudia dhambi.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni