4/1/2015.
MAOMBI YANAYOLETA BARAKA.
Maombi yanayoleta Baraka katika maisha yangu, ni maombi ambayo inatakiwa niombe
katika mazingira yafuatayo:-
a)Katika imani
b)Kwa kutumia misingi ya Neno la Mungu
c)Katika haki na kweli,haya mambo Kibiblia yameelezwa Zaburi
51:6,10,17.
Maombi yatakayo lazimisha Baraka za Mungu kuja juu ya mtu
lazima mwamini ahakikishe anaishi maisha ya haki na kweli.
(Ni vigumu kupata mpenyo wa Baraka kama sija ruhusu maisha
yangu yaongozwe na Roho Mtakatifu).
Siri za Kimungu zinajifunua kwa mwamini anayeishi maisha ya
kweli na haki.
Maombi ya wakristo wengi hayapati kibali machoni pa Mungu kwasababuwanaomba
katika hila, na mtu yoyote anayeomba katika hila milango ya kiroho ,au kina cha
maarifa ya rohoni hujifunga.
Kina cha maarifa ya rohoni kikijifunga nitakuwa mkristo
nisiyekuwa na faida katika maeneo mawili:-
A)Katika uso wa
dunia ,nikiwa na maana zaidi sitakuwa na msaada wowote kwa jamii iliyonizunguka
bali nitakuwa mzigo kwa jamii iliyonizunguka,ndiyo maana wakristo wengi
hunyooshewa vidole,hii ni kwasababuni mzigo kwa jamii
Mwanzo 4:1-5.
Kilichomfanya Kaini apoteze kibali machoni pa Mungu heshima
yake itoweke ni:-
i)Hila
ii)Wivu
iii)Majivuno
iv)Kiburi cha uzima ,haya mambo ndiyo yanayowagharimu
waamini wa leo ndiyo maana huishia kwenye kutangatanga katika makanisa na
kutaguta msaada.
Hii haitapingwa na chochote milele mbingu itafungua masikio
kwa mwamini ambaye ameumimina moyo wake kwa Yesu Kristo peke yake.
(Maisha ninayoyaishi chini ya jua ninajiandalia maandalizi
ya ufalme utakaonipokea baada ya kifo cha kimwili ,hapo inategemea maisha ya dhambi baada ya kifo kuna ufalme utakao nipokea
kwaajili ya kulipwa haki yangu sambamba na maisha ya kweli na haki baada ya
kifo cha kimwili kuna ufalme utakaonipokea kwaajili ya kunilipa sambamba na
maisha ya haki na kweli niliyoishi chini ya jua).
B)Sitakuwa na
faida kwenye uso wa Mungu mwamini aiyekuwa na faida kwenye uso wa Mungu mara
nyingi ni Yule mkristo anayepingana au asiyekubali kukaa chini ya mwongozo wa
Biblia unavyosema .
Mara nyingi mwamini asiyekuwa na faida kwenye uso wa Mungu
ni yule ambaye amepoteza kibali ,kwa hiyo mkristo anayepoteza kibali kwenye uso
wa Mungu huandamwa na mambo yafuatayo:-
i)Kukataliwa popote anapokanyaga.
ii)Kuandamwa na magonjwa yasiyoonyesha chanzo katika vipimo vya madaktari
iii)Umasikini vilevile kupoteza ulichonacho.
Mkristo wa aina hii kwamwe haiwezi kuonekana hekima ya Mungu
katika maisha yake kwasababu anakuwa ameshatoka nje na fomula ya Roho
Mtakatifu.
B) ILI NIWE NA
MUUNGANIKO WA BARAKA ZA MUNGU.
Ili niwe na muunganiko na Baraka za Kimungu inatakiwa nizame
sana katika suala la maombi ndiyo yanayolazimisha njia ya mtu kumuona Mungu
kufunguka ,vilevile maombi ndiyo yanayomsaidia mwamini kuzungumza na Mungu
,ndiyo maana inatakiwa niombe katika misingi ya Neno la Mungu (Biblia).
Maombi yatakayo sababisha muunganiko wa mtu na Mungu ni maombi yanayoombwa
sambamba na Maandiko Matakatifu (Biblia).
Kibali cha maombi yetu kujibiwa kwenye uso wa Mungu kitatokana na misingi ya Neno la Mungu ambayo
ni Biblia.
Mkristo anayeishi chini ya msingi wa Neno la Mungu maana
yake anaishi katika kweli ya Neno la Mungu.
ANGALIZO 1:Jinsi
ninavyopoteza muda wa kusoma Biblia katika mambo mengine yasiyokuwa
na maana Ndivyo ninavyojiongezea mashambulizi na
hali ya kushambuliwa
na shetani katika
roho.
Nguvu ya maombi huzalisha imani yenye uwezo wa kustahimili
na uvumilivu ndani yake ,na imani hii mara nyingi ndiyo inayoweza kuzalisha Baraka
hai kwa mwamini,vilevile ndiyo yenye uwezo wa kumshawishi Mungu kubariki,jambo
hili tunalisoma katika kitabu cha Danieli 3: yote.
Nikitaka kuitunza mamlaka ya Mungu katika maisha yangu
haitakiwi niwe mwepesi wa kunena mahali
popote,kwasababu kinywa hunajisi nguvu ya Mungu
iliyoko ndani ya moyo wa mtu,ndiyo maana Meshaki, Shedraki na Abedinego
hawakutaka kumjibu mfalme neno lolote
kama ilivyoandikwa katika Danieli 3:16, waliepuka kuiathiri imani waliyokuwa nayo kwa
Mungu,ndiyo maana mwisho walipata ushindi.
(Hakuna mwamini aliyemtukuza Mungu katika ugumu alionao Mungu
akaacha kumuinua ,Kwahiyo lazima nitambue siku zote imani niliyonayo ipo
kwaajili ya kutengeneza njia mahali paliposhindikana katika maisha yangu ).
Hekima ya Mungu ni namna ambavyo nitajiunganisha na
mtiririko wa Neno la Mungu (Biblia).
C) NINI KIFANYIKE
ILI NIWE SAMBAMBA NA BARAKA ZA MUNGU.
Ili niweze kuendana na Baraka za Mungu inatakiwa nifanye
mwendelezo wa kuikuza imani yangu kupitia Neno la Mungu katika mazingira
yafuatayo:-
a)Kukaa chini kufundushwa Neno la Mungu (Biblia),kwasababu
kitendo cha mimi kufundishwa Neno la Mungu ndivyo milango ya ufahamu wa rohoni
unavyofunguka na kupata upeo wa kuongezeka ziadi katika ufahamu wa Kimungu.
Maelezo na
ufafanuzi kuhusiana na ‘a’
Kitendo cha mimi
kukubali kukaa chini kufundishwa
Neno la Mungu maana yake nimeamua
kuyaruhusu maisha yangu yaongozwe na
Roho Mtakatifu,hapo kutazaliwa mambo yafuatayo :-
i)Kibali
ii)Mpenyo.
iii)Mafanikio.
iv)Ukaribu kati ya mimina Mungu .
Hali ya kufundishwa Neno la Mungu itanizamisha zaidi katika
unyenyekevu wa kiroho kuhusiana na hapo nitapata faida zifuatazo:-
i)Macho ya kiroho kuwa wazi
ii)Masikio ya kiroho kusikia, hapo ndiyo mwanzo wa kupata Neema ya kupambanua
sauti ya Mungu pale anaposema na mimi.
ANGALIZO 2:Siku
zote hakuna aliyefanya kazi yoyote au
biashara kwa muongozo wa Roho
Mtakatifu akafeli, bali hufanikiwa zaidi
maradufu .
Kufundishwa Neno la Mungu
humsaidia mkristo kutambua haki
zake kwenye uso wa Mungu ,mara nyingi hii humsaidia mwamini kuimarika zaidi katika misingi ya kumjua Mungu, ndiyo maana hata Biblia imeelezea kwa kina 1Timotheo
4:4-8.
Nikisimama vizuri
katika misingi ya Neno la Mungu nikafundishwa kweli kuhusu Mungu ukweli
ni kwamba mila yangu haifai ‘‘Ee Yesu nisaidie akili yangu iyakubali haya
niliyoyasikia leo’’.
b)Kusoma Biblia
Maelezo na
ufafanuzi kuhusiana na ‘b’
Mimi kama mwamini lazima nifahamu kitendo cha kusoma Biblia maana yake ni moyo wangu unazungumza na Mungu
waziwazi,kwasababu Mungu asili yake ni Neno
na maneno haya yamethibitishwa kupitia kitabu cha Yohana 1:1,2.
Yohana 1:1 ni
udhihirisho tosha ya kwamba kitendo cha kusoma Biblia maana yake ni Mungu
anazungumza na mimi waziwazi.
(Nikihitaji uponyaji inatakiwa nijifanyie maandalizi kwanza
ya usomaji wa Biblia ili moyo wangu upate utayari wa kupokea kutoka kwa Bwana pale nitakapotamkiwa).
Nikiongeza bidii katika kusoma Biblia ndivyo ninavyozidi kuongezeka katika nguvu za rohoni,kwahiyo ni rahisi
sana nikapata mpenyo utakaoweza
kuendesha maisha yangu ya kiroho na kimwili.
Swali:Nini maana ya kuongezeka nguvu za rohoni?
Jibu:Maana ya kuongezeka nguvu za rohoni ni kile kitendo cha
imani yangu kuliamini Neno la Mungu asilimia zote ndio maana hata Biblia
imesema katika Waebrania 11:6.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni