Jumapili, 4 Oktoba 2015

VIZUIZI VINAVYO FUNGA MAFANIKIO YA WAKRISTO

SOMO LA LEO : 
VIZUIZI VINAVYO FUNGA MAFANIKIO YA MKRISTO.

 1. Kushindwa kusamehe

 2. Kutokuondoa nadhiri kwenye uso wa Mungu, hivyo ndio vizuizi vikuu vinavyo funga mafanikio ya wakristo.

UFAFANUZI KUHUSU KUSHINDWA KUSAMEHE

- Kushindwa kusamehe ni hali inayojenga hila kwenye moyo wa mtu anaye mcha Mungu, na mara nyingi hali hii ya hila katika moyo wa mkristo humletea hathari zifuatazo : 

  i). Kupoteza hali ya kumsikia Roho Mtakatifu.

  ii). Moyo kushambuliwa na mawazo mabaya

  iii). Kupoteza hali ya kumcha Mungu.

- ( Jambo la kuwa nalo makini inatakiwa niwe na tahadhari sana ninapo ingia kwenye nyumba ya Mungu kuabudu kwa sababu, kwenye nyumba ya Mungu ni mahali ambapo kumeteuliwa rasmi kwa ajili ya watu kumwabudu Mungu, yaani ni eneo ambalo limefunikwa na uwepo wa nguvu ya Mungu muda wote ). 

- Kushindwa kusamehe ni hali inayo funga baraka za mtu kwenye uso wa Mungu, kwa sababu mkristo ambaye ameshindwa kusamehe Kibiblia amekengeuka Agano na Mungu, maneno haya hata Biblia imezungumza Mathayo 6: 14-15.

- ( kusamehe ni tendo la kiimani )

- Kitendo cha mimi ....( taja Jina lako ) kutangaza msamaha kwenye ulimwengu wa Roho ninakuwa nimejiunganisha na nguvu ya Mungu yenye uwezo wa kunitoa sehemu moja kimafanikio na kwenda sehemu nyingine kimafanikio, vile vile kunakuwa na Roho kamili ya KiMungu katika kuyalinda maisha yangu.

 - ( Nguvu ya Mungu inaishi katika maisha ya mtu mwenye tabia ya kusamehe na kusahau ).

- Nikitaka kuishi na upako wa kubarikiwa inatakiwa niwe mtu wa kusamehe na kuachilia .

- Nikitaka kubarikiwa na Mungu inatakiwa nijichunge na hila isiwepo kwenye moyo wangu, kwa sababu hila ni Roho kamili ya shetani, vile vile hila hupofusha macho ya kiimani kwa mtu anaye mtegemea Mungu Ee Yesu nisaidie mimi.

- ( Mungu habariki uovu hata siku moja kwa sababu yeye sio dhalimu,kinacho takiwa kwangu kama mtu ninaye amini ni kuyalinda maisha yangu ya wokovu yasinajisike ).

- Wakristo wengi tunaishi maisha ya dhambi kwa sababu tunaendekeza ubinadamu, kuendekeza ubinadamu mara nyingi humfanya mtu awe katika mazingira haya : 

  i).Kushindwa kupambanua Roho anapo sema nawewe au anapokuonya

  ii). Mara  nyingi hutafakari ubatili(uharibifu ) 

  iii). Moyo kushindwa kukubali maonyo, Kwa ufupi mtu wa aina hii haonyekagi.

  iv). Kujawa na kiburi ( majivuno )

- Katika kutafakari Neno la Mungu ndiko ninako pata ufahamu wa kujiongeza zaidi kiroho.

- Kushindwa kusamehe ni hali inayo ondoa utulivu na usikivu katika moyo wa mtu aliye jiandaa kupokea kitu kutoka kwenye uso wa Mungu. 

FAIDA ZA KUSAMEHE
- Faida ya kwanza ya kusamehe ni mkristo kupata hali ya uelewa pale ambapo Roho Mtakatifu anasema nae.

 - Maisha ya wakristo wengi yanavurugika karibia na mafanikio kwa sababu ni wavivu wa kufunga na kuomba, yaani kutafuta muongozo wa Roho katika plani zao.

- ( Kusamehe ni hali inayo leta ukaribu kati ya mtu na Mungu, vile vile mkristo ambaye ameamua kusamehe huwa hatazami ukubwa wa jambo alilo tendewa ). 

- Ninapo samehe maana yake nina ruhusu mapigo mazito katika maisha ya yule mtu, ndio maana Biblia ikaweka dhahiri katika kitabu cha Warumi 12:19-21

- ( Baraka za Mungu zinakuja kwa mtu mwenye bidii ya kuzitafuta ).

- Mungu anayo Roho ya uvumilivu kupita kitu chochote milele na milele.

- Nikitaka kujiita mwenye Imani ni lazima Roho ya uvumilivu niwe nayo.

- Mungu hayuko tayari kujibu maombi ya mtu mwenye hila na visasi, ndio maana wakristo wengi wanadumu katika taabu sana kwa kipindi kirefu, hiyo yote husababishwa kwa kushindwa kuachilia na kusamehe.

- ( Maumivu ya kutendwa yanazidi hata maumivu ya panga likikupitia kwenye mwili, kwa hiyo Yesu Kristo nisaidie niweze kutangaza msamaha ).

- ( shetani anapigwa kupitia mamlaka ya Neno la Mungu na sio kwa kitu chochote chenye ncha kali, kwa hiyo kinacho hitajika katika hili ni kutafuta kina cha Neno la Mungu ili mamlaka intende kazi ).

UFAFANUZI KUHUSU KUTOKUONDOA NADHIRI KWENYE USO WA MUNGU.


- Ikiwa nimeweka nadhiri kwenye uso wa Mungu inatakiwa nihakikishe nadhiri hiyo nimeiondoa kabla haijageuka kuwa laana.

Hakuna maoni: