11/8/2014
NGUVU YA KUSOMA
BIBLIA.
Wakristo
wengi, sanasana jamii ya waaminio wamepoteza nguvu ya kusoma Biblia, kwasababu
hawana ufahamu kwamba Mungu ni Neno, hii pointi ni halisi kabisa hata Biblia
imefunua katika Yohana 1:1-3.
Kutokana na
Yohana 1:1 nikisoma Biblia maana yake ninamsoma Mungu , vilevile moyo wangu
unafundishwa siri za ufalme wa Mungu.
Mkristo
mwamini anaposoma Biblia maana yake moyo wake unahojiana na Mungu uso kwa uso, ndio maana Yeu kristo alisema
wazi katika Yohana 14:23 .
Mkristo mwamini
anaye iamini Biblia, akikaa chini kusikiliza Neno la Mungu yaani kufundishwa,
akatoa muda wake kusoma Biblia mwamini huyu mpenyo ni lazima kwenye maisha yake
yaani mafanikio ni lazima , kasababu anakuwa ameyaishi mapenzi ya Mungu.
(Mkristo anapotoa
muda wake katika mambo makuu mawili
a).
kujisomea Neno la Mungu mara kwa mara
b).
kulisikiliza Neno la Mungu mara kwa mara katika Imani,maana yake anavalishwa
asili moja na Mungu kwasababu mwamini akiliamini Neno la Mungu(Biblia) maana
yake asili aliyonayo itafanana na asili ya Mungu , jambo hilli hata Biblia imelifunua kwa kina)
1Wakorintho 6:17.
Mkristo
mwamini huunganishwa na Neno la Mungu kupata Baraka zake anazozitamani kwenye
uso wa Mungu.
Nguvu ya
kusoma Biblia ndiyo itakayo nisaidia kuimarika katiaka ufahamu wa rohoni.
Nikijiona
ninakosa hamu ya kusoma Biblia maana yake ninanyemelewa na kifo cha kiroho, kwa
maana zaidi ninakuwa hai katika mwili, katika roho nimekufa. Jambo hili hata Ufunuo3:1 inasema.
FAIDA YA KUSOMA BIBLIA (KUSIKILIZA)
Kuna faida
kuu mbili katika misha ya kristo anayetoa muda kusikiliza Neno la Mungu
vilevile kujisomea Neno la Mungu.
A. Faida ya kwanza ni mkristo kupata
ufahamu
B. Mkristo kupata mtiririko wa maombi
UFAFANUZI KUHUSU
KIPENGELE “A” KINACHO ZUNGUMZIA UFAHAMU.
Maisha ya
mkristo aliyeokoka yaani aliye mwamini Yesu kristo na kumkiri Yesu kristo kuwa
Bwana na Mwokozi wa maisha yake yanahitaji ufahamu zaidi wa rohoni, kwasababu
wakristo waamini wanaishi, vilevile amezungukwa na jamii kubwa ya wasio amini, kwahiyo
kabla ya jamii ya wasioamini hawajaanza kuiamini Biblia inatakiwa wanione mimi
niliye okoka yaani ninaye iamini Biblia nikiyaishi maisha sambamba na kilicho
andikwa kwenye Biblia kiusahihi.
Ufahamu ndio utakayo
yafanya maisha ya mkristo aliye okoka kuwa mvuto kwa jamii ya wasio amini.
Mkristo
mwenye ufahamu huwa kuna mambo yanayo jitokeza kwenye maisha yake i. Hekima
ii.Upendo
iii. Utu
iv. Uvumilivu,Huyo anaweza kuitwa mkristo anayeishi sambamba na haki ya Mungu.
Ufahamu wa Neno
la Mungu katika maisha ya mwamini ndio utakao yasaidia maisha ya mwamini
kubadilika ,hapa inanipa picha haitakiwi nijitaabishe kwa mambo mengine bali
katika kila jambo ni kushukuru ,kwasababu katika pointi ya juu imenifunulia
maisha ya mtu mwenye ufahamu ni vitu gani vinatawa katika maisha yake.
UFAFANUZI WA
KIPENGELE “A” MTIRIRIKO WA MAOMBI
Hii inabidi
ifahamike wazi na kwa kila asikiaye na aelewe, mtirirko wa maombi ataupata mtu
kutokana na kina cha ufahamu wa Neno la Mungu katika moyo wake,na hii inanipa
ufahamu zaidi maombi yenye imani au yanayoombwa na mtu mwenye imani yanatoka
kwenye moyo wenye ufahamu wa ndani katika Neno.
Nikitaka
kupata mtiririko wa maombi lazima niuhusu ufahamu wangu kupata utulivu wakati
waa kusoma Biblia.
Maombi ya
mkristo yanapata nguvu pale anaporuhusu Neno la Mungu kuyaongoza maombi hayo.
Ninapo
litumia Neno la Mungu kwenye maombi yangu maana yake ninamtumia Roho Mtakatifu
kuvunja ukuta alioniwekea shetani kati ya mimi na Baraka zangu.
Mahali
ambapo kanisa linajengwa katika misingi ya kweli yaani ya Neno la Mungu kwa
usahihi huwa kuna mambo kadha kujitokeza
i)Uponyaji
ii) Kutubu
dhambi.
iii)Kusamehewa
dhambi.
iv)Kufunguliwa.
v)Kubarikiwa.
vi)
Madhihirisho ya nguvu za Roho Makatifu,Hayo ni mambo yatakayo onekana katika
kanisa linalofundisha misingi ya kweli ya ucha Mungu.
Kibiblia
maombi ya waamini inatakiwa yasimamiwe au yaongozwe na Neno la Mungu,Hapo
yatakuwa na mvuto wa kutetewa na Roho ambazo Mungu aziweka kwa lengo la kuleta
Baraka kwetu,uponyaji,rehema, na mengineyo mengi na katika kitabu cha Waebrania
Mungu kasisitiza Waebrania 1:14.
Maoni 2 :
Amina. Ahsante kwa Somo zuri
Barikiwa
Chapisha Maoni