Jumapili, 20 Desemba 2015

MUNGU ANATAKA NIWE NA UFAHAMU

MUNGU ANATAKA NIWE NA UFAHAMU

- Mungu anataka mimi niwe na ufahamu kwa sababu maisha ya kiroho yanategemea sana ufahamu wa Neno la Mungu.


- Ufahamu wa mkristo ukiongezeka kupitia Neno la Mungu ndivyo na Imani yake inavyoongezeka 

- ( Bila ufahamu wa Neno la Mungu ni vigumu kuongezeka kiimani )

- Kuombewa ni kufunguliwa njia, kutafutiwa wepesi lakini ufahamu ni bidii yako wewe katika kufanya mambo yafuatayo :-

i). Kusoma Biblia mara kwa mara, kwa sababu Biblia ni majumuisho ya vitabu mbali mbali vilivyo andikwa na mitume na manabii kwa njia ya Roho Mtakatifu , kwa hiyo hii ndiyo njia nyepesi itakayo weza kuupa ufahamu wangu uhai,vile vile kuuendeleza.

- ( hakuna tatizo lenye uwezo kupita Neno la Mungu ndio maana inatakiwa nijiimarishe katika Ufahamu wa Neno la Mungu )

ii). Kusikiliza Neno la Mungu mara kwa mara, hii hali ya kusikiliza Neno la Mungu mara kwa mara inaweza kunisaidia kama mkristo kuufanya moyo Wangu kuwa na hali ya unyenyekevu kwa sababu moyo ambao unatabia wakulisikiliza Neno la Mungu mara kwa mara ndani yake kutakuwa na misingi ifuatayo
1. Huruma
 2. Utu 
 3. Aibu

- ( Neno la Mungu Lina Jibu ya kila hoja yangu niliyo nayo )

- Suala la kuilinda Imani yangu isijeruhike ni jambo linalo hitaji ufahamu wa kina kwa sababu Imani huja kwa njia hii  
Warumi 10:17

- ( Ninamkiri Yesu kwa kinywa lakini lakini moyo wangu ninaulisha matango mwitu je nini matokeo?  )

- 2016 ni mwaka wa maendeleo ya kiroho na kimwili lakini maendeleo haya yatadhihirika iwapo nitaruhusu hali ya kukua kiufahamu.

- Mkristo ambaye hata ruhusu ufahamu wake kukua hawezi kuwa na mabadiliko ya kiroho na kimwili.
Warumi 10:1,2

- Ufahamu ndio unao weza kunisaidia kupambanua pale Roho Mtakatifu anapotoa maagizo juu ya maisha yangu.

- Kukiri na kuamini ni vitu vinavyo enda sambamba na kuleta ukamilifu, kwa hiyo katika kuamini kukipunguka kukiri hakuna ukamilifu, vile vile katika kukiri kukipunguka kuamini hakuna ukamilifu.

- Ili maisha ya kiroho yawe salama inatakiwa ufahamu wangu niuimarishe vizuri katika kumjua Mungu kwa sababu kumsikia Mungu akisema inategemea ufahamu nilio nao katika Neno lake.

- ( Kuongezeka kwa Imani yangu kunategemea ufahamu nilio nao kwenye Neno la Mungu )

- Ninaye pigana nae ananizidi maarifa kwa sababu mimi sina ufahamu wa kutosha wa Neno la Mungu, kwa hiyo ili niweze kumdhibiti kabla hajaleta uharibifu kwangu inatakiwa niongeze zaidi maishani mwangu ufahamu wa Neno la Mungu na ufahamu huu utanisaidia kupambanua  mapema mapenzi ya adui kabla hayajaniathiri.

- Maisha ya watu wengi yamejaa visasi na malipizi kwa sababu hawana ufahamu wa kumgundua  adui mapema kabla ajaleta maumivu katika maisha yao.

- Lengo kuu la Mungu kutaka mimi niwe na ufahamu ni ili niweze kupambanua mazingira ya hivi vitu vitatu: 
 a). Mwili
 b). Kinywa
 c). Moyo

UFAFANUZI KUHUSIANA NA KIPENGELE (a) KINACHO ZUNGUMZIA MWILI.

- Haya mambo ni ya kuwa nayo makini sana yahusianayo na mwili.

- Taa ya mwili ni jicho, na nguvu ya mwili ni hisia 
Mathayo 6:22-23

- Jicho halishibi kuona lakini ufahamu wangu ukikua kupitia Neno la Mungu Jicho langu litakuwa na kiasi.

- Jicho ndilo linalo sababisha hisia za mwili kuamka kwa hiyo ili jicho langu liweze kuwa na hofu ya Mungu ndani yake au kuwa na kiasi inatakiwa nifanye mambo yafuatayo : 
 1.  Niliruhusu lione lakini nisilipe uwezo wa kuanza kujadili hoja ya kile ambacho limeona 

- Ili niweze kupona katika kizazi hiki cha zinaa na dhambi ambacho Yesu alikisema kwa kinywa chake, inatakiwa nitahiriwe jicho langu, nitahiriwe moyo wangu, na nitahiriwe mwili wangu.

- ( Mkristo kama hajaruhusu hali ya ufahamu  wake kukua vilevile kuwa na kina zaidi katika kumjua. Mungu bado changamoto za maisha hata weza kukabiliana nazo.)

- Mwili una ukaribu sana na dhambi kuliko ukaribu na Roho Mtakatifu na maneno haya yanadhibitishwa kimaandiko katika kitabu cha  
Wagalatia 5:19-21

- Ili mwili wangu uweze kutiishwa inatakiwa moyo wangu kuelimishwa kwa undani zaidi kupitia Neno la Mungu

- Huu ndio ukweli, Mungu amenipa nguvu za kiroho ndo maana nina mwamini lakini mazingira yangu ya kimwili ndiyo yanayo dhohofisha nguvu za kiroho nilizo nazo.

- ( Nitapataje nguvu za kiroho kama bado niko chini ya utawala wa mwili wangu ? )

- Mazingira ya kimwili kwa mujibu wa Wagalatia 5:19 ni vigumu kumpa mkristo nafasi ya kumcha Mungu katika Roho na kweli isipokuwa Neema ya Mungu imeingilia kati kama maandiko yasemavyo. 
Waefeso 2:8

UFAFANUZI KUHUSIANA NA KIPENGELE (b) KINACHO ZUNGUMZIA KINYWA.

- Kinywa ni mlango wa moyo kwa lugha ya Kibiblia kinywa ndicho kinacho dhibitisha nje mawazo ya moyo wa mtu, vile vile kinatoa uhalisia wa mipango ya mtu ijayo, au kwa siku za usoni.
Yakobo 3:8-10

- Neno lolote linalotoka katika kinywa changu au cha mtu fulani halitoki kwa bahati mbaya wala sio kuteleza ni kwamba dhamira yangu au ya mtu inakuwa iko hivyo.

MAELEZO ZAIDI 

Watu wengi husingizia hasira kwamba inamfanya mtu azungumze kitu fulani au atukane, lakini ukweli ni huu hasira ni roho anayo pagawa nayo mtu akiwa na akili zake timamu, kwa hiyo ukiwa na ufahamu wa kutosha wa Neno la Mungu unaweza ukadhibiti udhaifu huo wala usikudhalilishe hata Biblia imetoa angalizo juu ya hilo waraka wa Yakobo 1:20

-  Hasira si jambo linalotoka kwa Mungu, bali ni mojawapo ya matendo ya kimwili kwa hiyo mambo kama hayo kunahitajika ufahamu sana wa Neno la Mungu ili kuyadhibiti.

- Kinywa ninaweza nikakitiisha kupitia usomaji wa Biblia, Tenzi na Zaburi 

- Ukiona kinywa cha mkristo kina kuwa kizito kutamka mambo ambayo yako kinyume na mapenzi ya Mungu jua tayari ndani ya huyo mtu kuna dalili za muunganiko kati ya Roho Mtakatifu na roho yake.

- Dhamana ya kuumba au kuangamiza inatoka ndani ya mamlaka iliyo lala ndani ya kinywa cha mwamini, kwa hiyo mkristo mwenye ufahamu akikitumia kinywa vizuri baraka zake na mafanikio yake hayatakuwa na mfano, maandiko hayajasita kusema juu ya jambo hili.
Mithali 18:20,21

UFAFANUZI KUHUSIANA NA KIPENGELE (c) KINACHO ZUNGUMZIA MOYO


-( somo hili litaendelea wiki ijayo...........)

Hakuna maoni: