UJUMBE WA LEO: 15/3/2015
IMARISHA MSINGI WAKO
- Nini maana ya msingi?
Mfano: hakuna Nyumba inayoweza kujengwa bila kuanzwa na msingi, vilevile katika hili kuna ufafanuzi zaidi.Kivipi? Jibu: kuna tofauti kati ya msingi wa Nyumba ya kawaida na msingi wa Nyumba ya ghorofa, ki kawaida nyumba ya kawaida Msingi wake ni M 1, na nyumba ya ghorofa msingi wake ni M 2
- Imani ambayo ni sawasawa na msingi wa nyumba ya kawaida ambayo tumeambiwa ni futi tatu ni imani niliyonayo katika dini niliyozaliwa nayo,yaani nimezaliwa nikamkuta baba na mama ni dini fulani na mimi nikaendeleza dini hiyo,ukweli ni kwamba msingi wake bado ni dhaifu.
- Imani ambayo ni sawasawa na msingi wa ghorofa ambayo nimeambiwa kina chake kinaenda futi 6, ni Imani ambayo Yesu Kristo aliianzisha chini ya jua, na ukweli ni kwamba siku zote ni imani yenye matokeo mazuri vile vile msingi wa Imani hii unahitaji kina zaidi, ndio maana imefananishwa na msingi wa ghorofa hata maandiko matakatifu
yamedhibitisha maneno haya,Luka 6:47-48.
- nini maana ya kwenda kwa Yesu Kristo? Sambamba na Neno linavyo sema katika Luka 6:47
- Maana ya kwenda kwa Yesu Kristo ni kumwamini na kumkiri hiyo ndiyo hatua ya kwanza,na vile vile wokovu tunaupata kwa kuamini na kukiri sambamba na Neno lililoandikwa katika Warumi 10:9
- ( nivigumu kufunguliwa nikiwa sijamkiri Yesu Kristo na kumwamini hata uombewe na nani hautoki kwenye kitanzi,)
-Je hatua ya pili ni ipi baada ya hatua ya kwanza?
Hatua ya pili ni kuyasikiliza Maneno ya Mungu yaani kwenda kanisani kusikiliza mahubiri, vilevile kuyasoma maneno ya Mungu, kwa sababu kuyasoma ni sehemu ya kuusikilizisha moyo Neno la Mungu, jambo hili limenenwa pia katika maandiko Warumi10:17
-Je hatua ya 3 baada ya yapili na ya kwanza ni ipi? Luka 6:47
- Hatua ya Tatu ni kuyatendea kazi maneno ya Mungu, jambo hili hata Biblia haikuacha kulifunua kimaandiko Yakobo 1:22-23.
- Hatua ya Tatu ni muhimu sana kwa kila mwamini anayetarajia kupata baraka zake kwa Yesu Kristo
-ninaamini ndio, nahudhuria kanisani kusikiliza Neno la Mungu sawa, lakini kama siyatendei kazi maneno ya Mungu mpenyo kwangu hauwezi kupatikana ndio maana maisha ya wakristo wengi wanaotafuta baraka za Mungu zimejificha mbele yao sababu ndo hiyo
- Baraka za Mungu zinaendana na mtu yeyote yule anayefuata kanuni, sheria na misingi ya maandiko matakatifu.
-( Dini ya mbingu ni wokovu )
Hatua ya nne ni ipi,baada ya kwanza, ya pili, na ya tatu?
- Hatua ya nne ni sambamba na mtari wa 48,luka 6:48 na hii inadhihirisha wazi baraka za Mungu, Mungu wa Ibrahimu, Mungu wa Isaka, na Mungu wa Yakobo zitaambatana na mwamini atakayesimama katika hatua nilizoziandika katika point zilizopita.
( hatua ya nne ni kuimarisha Msingi )
Maana ya neno msingi katika tafsiri ya kiroho
- Msingi katika tafsiri ya kiroho ni neno la Mungu,
- jina la Yesu Kristo linapata nguvu ya kufanya mambo makubwa kwenye maisha ya mtu mwenye msingi wa Neno la Mungu.
- Msingi wa Neno la Mungu ndio unaolinda maisha ya mwamini katika baraka zake au katika maisha yake.
- kadri jinsi Mkristo anavyo zidi kuimarika katika msingi wa Neno la Mungu ndivyo mambo makubwa ya Kimungu yatakavyo funguka katika maisha yake.
- Mkristo aliyeimarika katika msingi wa Neno la Mungu mfano wake tumeuona wazi katika Luka 6:48.
- Msingi wa Mkristo mwamini ukiimarishwa vizuri katika Neno la Mungu ( Biblia) majaribu ambayo atakutana nayo kwenye maisha anayo nafasi ya kuyashinda.
- Msingi ulio imara katika maisha ya mwamini haujengwi na vitu vinavyo onekana bali visivyo onekana vitu vya rohoni ambavyo ni neno la Mungu.
- Nikiimarika vizuri katika msingi wa Neno la Mungu napata uwezo mkubwa wa kuidhibiti nafsi
- Nikijiimarisha katika misingi ya Neno la Mungu changamoto za kiroho nitazishinda
- Wokovu wa Mkristo unaimarika kadri ambavyo anazidi kuboresha msingi na msingi ni Neno, kwa hiyo kumbe nitakavyozidi kuzama kwenye kina cha Neno la Mungu ndivyo baraka za rohoni zitakavyo jiunganisha na mimi.
- Nikiwa na msingi ulio bora vitu vya kimwili haviwezi kuniathiri imani yangu, na Neno la Mungu ndio msingi wa mkristo mwamini ulio bora, hata Biblia imeyasema hayo katika Mathayo 24:34-35.
- kama nitaamua kujijenga katika msingi ulio bora ambao ni Neno la Mungu itanisaidia kupita katika nyakati zote bila kujeruhika kiimani.
- ( Bidii yangu katika kumtafuta Mungu ndiyo itakayo sababisha matokeo mazuri katika maisha yangu ya kesho )
- Ili niweze kushinda vita vya kiroho inatakiwa niboreshe msingi wa Neno ninaloliamini. Mathayo 24 : 35 Biblia inadhibitisha uhai uliyopo katika Neno la Mungu.
- kinacho nifanya nishindwe kusoma Biblia mchana, asubuhi na jioni ni kwamba mimi mwenyewe Samweli nikiwa na akili timamu ninakwepa kuyaishi maisha matakatifu kwa sababu Biblia inaagiza hivyo
- ( Biblia inanijua hata kama mimi ninaisoma ndio maana ninapo anza kuisoma kila kitu inaelezea maisha yangu kwa uwazi )
HATUA ZA KUIMARISHA MSINGI WANGU AMBAO NI NENO LA MUNGU.
- Neno la Mungu linahitaji maandalizi ya kutosha ili liweze kujiimarisha kwenye moyo wa mwamini
- Je maandalizi ya namna gani ?
i ). Maandalizi ya kwanza ni kuisikiliza Neno la Mungu mara kwa mara hapo ninausaidia ufahamu wa moyo wangu kuwa katika mfumo wa kuelewa na kukumbuka kile ambacho Neno linasema.
- (amka kiufahamu bado nafasi ipo )
- Mkristo aliye amka kiufahamu ndio mwenye uwezo wa kuidhibiti nafsi
- changamoto ya kesho ni kubwa kuliko ya jana kwa hiyo nikilifahamu hili inatakiwa niimarishe msingi wangu katika Neno la Mungu.
- Maisha yangu leo yanayumba kwa sababu msingi niliojengewa jana ni mbovu kwa hiyo haya ninayo yapitia leo ninalipa gharama ya kumlingana Mungu.
- inatakiwa nijiimarishe katika misingi ya Neno la Mungu zaidi ili kila neno ninalolisikia nje nilipime na Neno la Mungu ndipo nitakapo fahamu usahihi wa jambo ukoje.
ii). Kujisomea maandiko matakatifu ( Biblia )
- Kusoma Biblia kuna sehemu kubwa sana ya kuimarisha ufahamu wa rohoni wa mkristo kwa hiyo kadri jinsi nitakavyo zidi kusoma Biblia ndivyo nitakavyo zidi kupata ufahamu wa kuzitambua siri za Mungu.
- nikitaka kuimarika vizuri katika ufahamu wa rohoni nikubali kufundishwa
- kile ambacho kumbu kumbu yangu inaniletea ndicho kinachukua nafasi ya kuniongoza moyo wangu kwa wakati huo kwa hiyo katika suala hilo bila kuwa makini naweza kujikuta ndoto zangu hazitimii.
- Kila mwenye mwili ana mapungufu haijalishi ni mchungaji au ni mwumini, ndio maana tunasisitizwa kuimarisha misingi ya Neno la Mungu katika maisha yetu ili tuzilingane baraka za Mungu.
- ili tuzilingane Baraka za Mungu tukubali kuambiwa ukweli kwa sababu mtu anayekubali kuambiwa ukweli ni rahisi kushaurika, vile vile mtu anayekubali kuambiwa ukweli ni rahisi kufanikiwa ndio maana Yesu akayaweka wazi katika maandiko matakatifu Yohana 8:32
- nikiwa ni mkristo mwenye upeo wa kumsikia Mungu akisema maisha yangu ya kimwili na kiroho hayawezi kunajisika
- ( maisha ya ukweli kwa mtu yanaleta muunganiko kati ya mtu na baraka za Mungu)
- ninazikosa baraka za Mungu kwa sababu sina tabia ya kuyaishi maisha ya ukweli na hii ipo wazi kwa sababu Tabia ya mtu ni jumla ya mazoea yake.
- kabla mwamini hajawekwa huru na kweli inatakiwa yeye binafsi aandae mazingira ya kweli hiyo kumfungua
- kilicho jaa moyoni mwangu muda huu ndicho kitakacho nipa matokeo ya kile ninacho kitaka kwenye uso wa Mungu.
- iIi moyo wangu usiwe chanzo cha kuninyima baraka za Mungu inatakiwa niujengee msingi wa kusikiliza neno la Mungu mara kwa mara na kulisoma hapo itakuwa rahisi kudhibiti hali ya udanganyifu unaotoka katika moyo wangu.
- nikishafahamu mahali hapa kunaweza kukawa chanzo cha mimi kutoka katika dhiki niliyonayo inatakiwa nifuate mambo yafuatayo : ( a ) taratibu za mahali hapa ( b ) kanuni za mahali hapa ( c ) misingi ya mahali hapa ( d ) sheria za mahali hapa, hapo itakuwa rahisi kupata mpenyo.
- Ili moyo wangu uweze kunipa haki inatakiwa niuimarishe kwanza kwenye misingi ya Neno la Mungu ndipo utapata hofu ya kutokukiuka mapenzi ya Mungu
- mwamini mwenye uwezo wa kuulinda moyo wake anayo nafasi kubwa ya kuimiliki baraka za Mungu
somo hili litaendelea wiki ijayo........
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni