Jumapili, 8 Mei 2016

HATUA ZA MABADILIKO


IBADA YA JUMAPILI:

HATUA ZA MABADILIKO.

- Nikiwa Kama mkristo ninaye mwamini Mungu inatakiwa maisha yangu yaendane na hatua za mabadiliko, kwa sababu namcha Mungu katika hali ya kiimani, kwa hiyo lazima maisha yangu niyaendeshe katika hali ya kiimani pia.



- Mabadiliko katika maisha ya mtu anaye mwamini Mungu yanaanza pale ambapo mtu anaamua kuruhusu ndani mwake hali ya kukubali kufundishwa Neno la Mungu.

- Nikikubali kufundishwa Neno la Mungu ndio mwanzo wa hatua za mabadiliko katika maisha yangu, kwa sababu jinsi ambavyo Imani yangu inaongezeka ndivyo mabadiliko ya kimwili na kiroho katika maisha yangu yanapokuwa dhahiri.

- ( Imani yangu inapo kuwa dhaifu lazima kutakuwepo na udhaifu katika maeneo yote ya maisha yangu kwa sababu Biblia imeweka wazi ).
Waebrania 10: 38-39
Mithali 2:6

ANGALIZO 1:-Neno ninalo litamka liwe zuri au baya kibiblia ni ahadi nimeiweka lazima litatimia tu hivyo inatakiwa nijifunze kujitamkia maneno mazuri ya Baraka hata Kama nipo katika kipindi kigumu.

- Mabadiliko katika maisha ya mkristo yanaanzia pale ambapo mkristo amejielewa hata katika matamko anayo jitamkia ni picha halisi ya maisha yake ya kesho.
Yeremia 1 : 11,12.


ANGALIZO 2:- Mtu anaye mwamini Mungu akitamka Neno kwenye kinywa chake maana yake ameumba, Kwa hiyo inategemea ni Neno gani unalo litamka katika kinywa.

- ( Juhudi za kumtafuta Mungu zinatakiwa ziwe katika maarifa).

- ( Kila Jambo linalo nitokea katika maisha lina kusudi maana kwenye uso wa Mungu, kinacho takiwa ni mimi kutazama Neno la Mungu tu ndilo lenye jibu.)

- Jinsi ninavyo mwamini Mungu inatakiwa hata kunena kwangu na kutenda kwangu kuendane sambamba na mapenzi ya Mungu.

Je unafahamuje umesamehewa dhambi?

- Ninafahamu nimesamehewa dhambi pale ambapo moyo Wangu umeamini Kuwa Yesu Kristo ni Bwana na kinywa changu kinapokiri kwamba alikufa akafufuka na hiyo ndio toba ya kweli.
Warumi 10:9-10.
Yohana 1:12

Je unasamehewa dhambi Kwa njia gani?

- Ninafahamu nimesamehewa dhambi Kwa njia ya Imani.
Waebrania 11:6

- Maisha ya mkristo yanayo tegemea Imani hata angepita kwenye mazingira ya aina gani kinywa chake hakiwezi kuzungumza kinyume na mapenzi ya Mungu.
Mfano mzuri ni :- Ayubu 2: 9-10.

- ( Ufahamu wa Neno la Mungu ni zaidi ya pesa na mali )

- Ninapata ufahamu zaidi jinsi ninavyo ingia katika kina cha Neno la Mungu, Kwa sababu ufahamu wa kuyaendesha maisha yangu unatokana na kina nilicho nacho katika kumjua Mungu katika Neno lake.

- Maisha ya mkristo anaye mtegemea Mungu inatakiwa awake nguvu nyingi katika kuhangaikia vya rohoni sambamba na Neno linavyo sema.
 2wakorinto 4:18

Hakuna maoni: