Jumapili, 1 Mei 2016

IMANI IMARA INA UVUMILIVU

Somo la Leo: IMANI IMARA INA UVUMILIVU.

- Imani niliyo nayo inazidi Kuwa imara ninapo kuwa nina uvumilivu zaidi.

Nini chanzo cha uvumilivu au uvumilivu unaumbwa na nini? 
- Chanzo kikuu cha uvumilivu ni Neno la Mungu lililoko katika moyo wa mtu.
- Ninapo Kosa hali ya uvumilivu katika Imani yangu pindi ninapo peleka hoja mbele za Mungu maana yake ni kumfanya Mungu kuwa muongo( nina mkufuru Roho Mtakatifu )
Waebrania 10:38
- Kukosa hali ya uvumilivu katika moyo wangu kunatengeneza mazingira ya shetani kuharibu muujiza wangu. 
- Hali ya uvumilivu niliyo nayo mimi kama mkristo ndiyo inayo nipa haki mbele za Mungu ya kujibiwa maombi yangu.
luka 4:1-5
- Uvumilivu ndani ya mtu utaimarika endapo mtu atajiendelea kiroho.

Hakuna maoni: