Jumapili, 10 Aprili 2016

10/4/2016 UMUHIMU WA NENO LA MUNGU KATIKA IMANI NILIYONAYO KAMA MKRISTO

UJUMBE WA LEO
10/4/2016

UMUHIMU WA NENO LA MUNGU KATIKA IMANI NILIYONAYO KAMA MKRISTO

Mimi kama mkristo nisipojua uthamani wa Neno la Mungu ni vigumu kupiga hatua katika maisha ya kiroho.

Maisha tunayoyaishi duniani yamegawanyika katika sehemu kuu mbili, na sehemu zote mbili zinatawaliwa na Neno la Mungu.
A)Ulimwengu wa damu na nyama
B)Ulimwengu wa Roho
Yohana 1:1-3
Mwanzo 1:26.

Mwanadamu aliumbwa kwa mfano wa Mungu ,hii ina maana kabla mwanadamu kuumbwa (mwanadamu wa damu na nyama )alianza kutokea katika ulimwengu wa Roho kwanza.

Siwezi kudumu katika majaribu ninayoyapitia kwa muda mrefu ikiwa kinywa changu kinatamka hali ya kushindwa.

Imani niliyonayo ina kinywa ambacho kinapata nguvu kwa njia ya Neno la Mungu.

Imani niliyonayo ikizungumza ndani yangu na mimi binafsi nikatoa ushirikiano lazima nitapokea muujiza, hii ni sawa na kusema jinsi ninavyokuwa na bidii katika kukiri ndivyo ninavyorahisisha upokeaji wa haja yangu kwenye uso wa Mungu.

(Nikijiwekea mikakati ya kusoma Biblia sauti ya Mungu inafunguka ndani yangu yaani waziwazi).

Tatizo la wakristo kushindwa wanatumia sana akili zao kupambana na majaribu na sio kutumia imani kupambana na majaribu lazima utashindwa tuu.

(Hata kuja kanisani kuka chini kusikiliza Neno la Mungu ni karama inayotoka kwa Mungu.

Hakuna maoni: