Alhamisi, 25 Desemba 2014

UJUMBE WA LEO. 25/12/2014. SABABU ZA YESU KRISTO KUZALIWA.

UJUMBE WA LEO.
25/12/2014.
SABABU ZA YESU KRISTO KUZALIWA.

Ziko sababu nyingi sana za Yesu Kristo kuzaliwa ,lakini kuna sababu moja kuu iliyopelekea kuzaliwa katika mwili.


A)Sababu kuu ya Yesu Kristo  kuzaliwa katika mwili  na kuuacha utukufu aliokuwa nao mwanzo ni ili aje awe sadaka  ya ukombozi kwa kila  atakaye mwamini.

(Hakuna sadaka nyingine yoyote ya ukombozi chini ya jua  nje na Yesu Kristo).

Kuzaliwa kwa Yesu Kristo ndiko kunakoonyesha picha halisi ya kuurithi ufalme wa Mungu katika haki na kweli.

Ninasherekea kwasababu ninakumbuka siku ambayo sadaka ya ukombozi ambayo ni Yesu Kristo alipozaliwa.

Katika Luka Mtakatifu 1:30 ninaona thamani ya Neno la kinabii

(Kuzaliwa kwa Yesu Kristo kulitokana na Neno la Kinabii).

(Wakristo wengi wanapoteza Baraka zao (miujiza) na hii inatokana na kutokuamini sauti ya Mungu kupitia Mtumishi wake).

(Kitendo cha mimi kupewa unabii maana yake nimepata Neema machoni pa Mungu , na hili limethibitishwa wazi katika Luka 1:30).

Jambo hili ni la kuwa nalo makini sana inabidi nipambane katika kuikuza imani yangu ,kwasababu  nikipewa Unabii na wakati huo huo imani yangu iko chini ninaweza kujikuta  nimepeperusha muujiza wangu,kwahiyo ili Neno la Kinabii liyabadilishe maisha yangu  inatakiwa nifanye mambo yafuatayo:-
A)Kufanya mwendelezo wa kuongezeka kiimani .
B)Kuulazimisha moyo wangu kukubali hali ya kufundishwa Neno la Mungu
C)Mimi binafsi kuruhusu ndani mwangu hali ya kukua kiimani .

UFAFANUZI  KUHUSU KIPENGELE ‘A’.
Maana  ya neno mwendelezo ni kutia bidii  ya kujikumbusha na kurudia  mara kwa mara kile kitu ambacho tayari nimesha fundishwa kuhusu Mungu ,kwa mfano katika hali ya uhalisia  ninapopanda mti nikauacha bila kuuwekea mazingira ya kupata lishe Je! Utakuwa?
Mzaingira yatakayofanya  mti ukue uwe na afya njema ni haya:-
I)Mbolea
II)Maji
III)Kuzungushia majani makavu katika shina ili yatunze unyevu wa umande.
(Jinsi ninavyomshukuru Mungu katika mwanga mdogo, mwanga mkubwa utanizukia ).

Mkristo asiyetafuta mwendelezo wa kukua kiroho ni rahisi akajikuta amemkufuru Roho Mtakatifu
(Mwendelezo katika maisha yangu ya kiroho ndio utakayo yakomboa  maisha yangu katika mitego ya shetani)

Bila mimi binafsi kuruhusu hali ya mwendelezo wa kukua kiimani ni vigumu kuushinda udhaifu nilionao.

1Timotheo 1:12…..inaonyesha wazi madhaifu yaliyokuwa yakilitesa kanisa lakini kwa Neema ya Mungu likapata ukombozi , na hii ni kwasababu likaruhusu hali ya mwendelezo wa kukua kiimani  katika maisha yao.

UFAFANUZI WA KIPENGELE ‘B’
Lazima niruhusu moyo wangu kufundishwa Neno la Mungu , hii itanisaidia masikio ya kiroho  kusikiliza mwongozo wa Mungu  anaosema kuhsu  mimi.

Ninapoenda kanisani lazima moyo wangu utamani kusikia kitu kipya kitakachonipa hali ya mwendelezo wa kukua  kiimani ,hapo maisha yangu ya kiroho nitakuwa nimeyakomboa.

Kuruhusu moyo wanhgu kulisikiliza Neno la Mungu ni jambo la thamanin sana  kuliko fedha na dhahabu.

Moyo wangu ukipata ufahamu vizuri wa Neno la Mungu  nitapata faida zifuatazo:-
I)Faida ya kwanza kuwa karibu na uwepo  wa Mungu , hii itanisaidia kumiliki Baraka za rohoni na za mwilini.
(Moyo wa mkristo  ukipevuka vizuri kuhusu Mungu maisha yake yataitwa haki)

II)Faida ya pili kina cha maarifa ya rohoni kitaongezeka , na hapo ndipo  mwanzo wa kupata uwezo wa kupambanua katika Roho ,na ndilo jambo la msingi ambalo waamini tunaliksda kutoka kwa Mungu. 

Hakuna maoni: