UJUMBE WA LEO
UMUHIMU WA IMANI.
Umuhimu wa imani katika
maisha ya mkristo ni lazima , kwasababu
maisha ya kila mwenye mwili yanategemea imani,na hili jambo liko wazi kila
mwenye mwili Mungu amempa kiasi cha
imani , ndio maana unaweza ukamkuta mtu hana hata ukaribu na Mungu lakini anasema tumuombe Mungu tutafanikiwa , hicho
ni kiasi cha imani alichopewa na Mungu moja kwa moja.
Ili mkristo
anayemtegemea Mungu aweze kutoka hatua moja kwenda hatua nyingine
kiroho inategemeana na bidii aliyonayo katika kuikuza imani yake.
(Kushindwa kwangu mimi
kunatokana na mambo ya kiroho kuyatazama kimwili lakini ukweli unajulikana , mambo ya kiroho hujulikana kwa
jinsi ya rohoni.)
Imani inapofika katika
kiwango cha juu mamlaka niliyonayo huwa hai na hapo ndio sehemu ya kutumia
kinywa changu vizuri ,kwasababu kila nitakachokitamka kitatimia ,sasa wakristo
wengi wanapokuwa katika kiwango hicho hujisahau na kutamka udhaifu.
(Nikitaka maisha yabadilike
nibadilishe ukiri wangu.)
Mathayo 18:18-20
(Mathayo 18:18 ni picha
halisi ambayo Biblia inamzungumzia mtu
anayeishi sambamba na Neno la Mungu au mwenye kulitendea kazi Neno la
Mungu, mtu wa aina hii mamlaka ya kinywa chake itakuwa hai , kwahiyo lolote
atakalotamka muda wowote lazima
lithibitike , kwasababu Yeremia1:2 kuna kitu pia Biblia imezungumzia.
(Hata kama nina ugumu wa
maisha kiasi gani haitakiwi nipoteze
muunganiko na Neno la Mungu ,
kwasababu thamani ya maisha ya mkristo kwenye uso wa Mungu inatokana na bidii
aliyonayo katika Neno la Mungu) .
Neno la Mungu ndilo lenye
uwezo wa kuibadilisha tabia yangu isiyompendeza Mungu, kwasababu lina uwezo wa
kunijua hata kama mimi ninalisoma.
Jinsi ninavyopunguza bidii ya
kulisogelea Neno la Mungu ndivyo ninavyoongeza uvamizi kwenye ulimwengu wa
roho.
Yeremia 1:11-12.
Roho ya maono inakuwa dhahiri
katika maisha ya mtu jinsi anavyozidi
kuzama katika kina cha Neno la Mungu ,
ndio maana watu wengi adui hatupi nafasi ya kutosha wa kulilingana Neno la Mungu.
Imani inayotokana na Neno la
Mungu ni imani yenye uwezo wa kukabiliana na jaribu la aina yoyote bila kukata tamaa na ikapata ushindi , kwasababu ni imani
ambayo inakuwa imeatamiwa na upendo halisi wa Kimungu.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni