Jumapili, 20 Machi 2016

INATAKIWA NIJIHADHARI NA ULIMI WA UONGO


Somo la leo :Jumapili

INATAKIWA NIJIHADHARI NA ULIMI WA UONGO.

- Nikiwa Kama mkristo ninaye mwamini Mungu inatakiwa nijihadhari sana na ulimi wa uongo, Kwa sababu ulimi wa uongo una hathiri mahusiano ya mtu na Mungu vile vile mahusiano ya ndugu na ndugu.


- ( Ulimi wa uongo ndio unao fanya Wakristo wengi wadumae kiroho, yaani Kwa ufafanuzi zaidi ulimi wa uongo unazuia mtiririko wa Roho Mtakatifu katika maisha ya mtu anaye mwamini Mungu)

- Nikitaka maisha yangu yachanue kuanzia jumapili ya leo inatakiwa kinywa changu kinene ukweli mbele za Mungu na mbele za watu ninao kutana nao kila siku.

- Ulimi wa uongo unayafanya maisha ya watu wengi kuwa magumu kwa sababu hakuna mapenzi ya Mungu katika uongo.

- Jambo linalo mkimbiza Roho wa Mungu katika maisha ya mtu ni roho ya uongo, ndio maana katika kitabu cha mithali 6 : 16 - 19 Biblia imeelezea Kwa undani vitu ambayo vinamfarakanisha mkristo mwamini na mapenzi ya Mungu.

- Nikitaka Mungu aanze kuwa dhahiri katika maisha yangu ni kudhibiti kinywa changu kinene kweli huo ndio mwanzo wa baraka za Mungu kujifunua katika maisha yangu.

- Ulipo uongo unaondoa utukufu wa Mungu katika maisha ya mtu.

- ( katika ukweli Mungu anaingilia Kati )

- Mungu anapenda ukweli katika kinywa cha anaye mwamini Kwa sababu yeye ni kweli.

- ( Katika ulimi wa uongo hakuna uponyaji wala hakuna baraka, vile vile wala hakuna mafanikio)

- Katika ukweli kuna ujasiri wa kukabiliana na changamoto yoyote ninayo kutana nayo katika maisha, ndo maana Biblia ikasema katika Yohana 8 : 31,32

- Ili maisha yangu yaweze kubadilika inatakiwa nijifunze kusema ukweli hata kama niko katika hali ngumu.

- Nikiendesha maisha yangu katika ukweli yatapata kibali mbele za Mungu na mbele za wanadamu.

- ( Ulimi wa uongo hauna hekima wala adabu)

- ( Ulimi wa uongo hauna tofauti na uchawi )

- ( Katika kweli kuna msamaha na Rehema za Mungu )

- Msaada ninao upata kutokana na ukweli ninao usema ndani mwangu unao baraka za Mungu ndani mwake.

- Ulimi wa uongo uliathiri maisha ya anania na safira mwishowe wakajikuta wamefarakana na utukufu wa Mungu, hata mpaka mauti inawakuta walikuwa wamefarakana na utukufu wa Mungu, mambo haya yameelezwa wazi katika kitabu cha Matendo ya Mitume 5 : 1 na kuendelea

- Inatakiwa nijifunze kusema ukweli ili Mungu awe dhahiri kwangu.

- Ninapo sema uongo kwanza ninajidanganya moyo Wangu yaani ninajijeruhi mwenyewe.

NAMNA YA KUKABILIANA NA ROHO YA UONGO

- Ufahamu wa Neno la Mungu unapokuwa katika moyo wa mtu, na Neno likaweka mizizi katika moyo wa mtu, ni vigumu kinywa cha mtu huyo kunena uongo, Kwa sababu moyo unapofurika maneno ya Mungu kinywa cha mtu kitanena utukufu wa Mungu tu.

- Maisha ya ukweli ni mazuri sana ingawa yanahitaji kuikana nafsi.

- Kama chanzo cha mafanikio yangu ni Mungu haitakiwi niukimbie uso wake siku zote.

- Ili niweze kuidhibiti roho ya uongo inatakiwa niruhusu hali ya moyo wangu kufundishwa Neno la Mungu ndio maana Biblia inasema katika Zaburi 119 : 9 - 11.

- Kuna umuhimu wa roho yangu kuimarishwa katika Neno Kwa sababu taarifa za Mungu tunazipata Kwa njia ya Neno, Kwa maana jinsi unavyo zama katika Neno ile sauti ya Mungu inakuwa wazi wazi kwako.

- Moyo ukiimarika katika Neno hata dhambi inakosa mpenyo wa kuingia kwa mtu.

- Tatizo linalo tukumba Wakristo hatuna muda wa kutosha wa kuweka mahusiano ya karibu na Neno la Mungu Kwa hiyo ni vigumu kupata taarifa ya Neno haraka, ndio maana huwa tunajikuta tayari tumeingia katika maumivu.

- Neno la Mungu liwe rafiki yangu na Mimi niwe rafiki wa Neno maumivu hayatanifika bali nitapewa taarifa kabla ya Mimi kuvamiwa au kuathiriwa na Jambo lolote, haya mambo Biblia imeyadhibitisha kimaandiko Amos 3 : 7

- Mungu hutufunulia Siri zake Kwa njia ya Roho Mtakatifu kupitia Neno lake.

Hakuna maoni: