....
Visit Us on Facebook
Ijumaa, 18 Machi 2016
SADAKA
Somo la leo : Ijumaa
SADAKA
- Sadaka ni kitu chochote ninacho kitoa mbele za Mungu Kwa Imani na Upendo ili kujenga Ufalme wa Mungu.
- Sadaka ni harufu ya manukato, ndio maana tendo la utoaji huwa linauumiza moyo sana.
- ( Utoaji wenye Baraka umesimama katika misingi ya Imani )
- Sadaka ni silaha Tena kubwa sana kwenye ulimwengu wa Roho Kwa sababu ni tendo linalo fanyika katika mazingira ya kiimani
- Uchumi wa mkristo aliye okoka huwa unakuwa zaidi kutokana na bidii anayokuwa nayo katika suala zima la utoaji Kwa sababu katika utoaji kuna kanuni zake.(1 Samwel 7 : 7-13 )
- Ulipo udhaifu Wangu ndio mlango ambao shetani anautumia kuyaathiri maisha yangu.
- Dhambi inapo ukalia moyo wangu maana yake itanipotezea ujasiri wa kusimama mbele za Mungu, yaani hata kama nitasimama kuomba bado ndani mwangu kutakuwa kuna wimbi kubwa la mashaka.
- ( Katika hii point ya juu ndio maisha ya Wakristo yalivyo )
- Ndani ya sadaka kuna nguvu ambayo ina uwezo wa kumtiisha adui yangu, kwanza naitoa Kwa imani pili nainuia.
- ( Katika Sadaka yangu ninayo mtolea Mungu Inatakiwa niinuie ndipo itakapo weza kuniletea matokeo )
- ( Biblia inasema Imani pasipo matendo imekufa, Kwa hiyo utoaji wa Sadaka ni tendo la Imani )
Waebrania 13 : 2
- Jambo la kufahamu na Kuwa makini nalo kila mtu ninaye mnyooshea mkono na kumsaidia Baraka yangu iko mikononi mwake, Kwa hiyo Kwa kulitambua hili natakiwa niongeze bidii ya utoaji hata maandiko yanasema ni heri kutoa kuliko kupokea.
- Kumjengea Bwana madhabahu mimi sio wa kwanza bali ni jambo ambalo lilisha fanyika na ambalo litaendelea kufanyika kwa sababu ni tendo linalo endelea vizazi na vizazi.
- Mfano mzuri 2 Samweli 24 : Soma sura nzima.
- Kutokana na 2 Samweli 24:25 ni picha halisi kwamba kuna mambo mengine katika maisha yetu ambayo tunayaona yanakuwa kroniki inatakiwa tuyatolee Sadaka ndipo wepesi upatikane.
- ( Kitendo cha kuitangaza sadaka yangu Kwa jirani yangu kibiblia maana yake nitakuwa nimeuza utu wangu kwa adui, vile vile Kitendo cha Kanisa kuitangaza sadaka iliyo patikana katika wiki Kanisa linakuwa limeuza utu wake Kwa adui ).
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni