MADHARA YATOKANANYO NA KINYWA
KWA WAAMINI WANAO MCHA MUNGU
Mamlaka ambayo Mungu amenipa inatakiwa
niitumie katika kubariki sio kulaani watu wengine.
Mkristo ambaye anamcha Mungu
inatakiwa awe na tahadhari sana katika
maneno ya kinywa chake, kwasababu katika maneno hayo ndipo anapopatia wepesi wa
kubarikiwa au ugumu wa kuharibu maisha yake.
Jinsi ninavyoamini moyoni
mwangu , ndivyo inavyotakiwa katika kinywa changu ninene, hapo kuna Baraka
Warumi 10:10.
Kama moyo wangu unaamini
katika mapenzi ya Mungu vivyo hivyo hata kinywa changu kinatakiwa kikiri
mapenzi ya Mungu.
Nikiwa mimi ni mkristo
ninayemcha Mungu,ninayempenda Mungu inatakiwa niulinde moyo wangu kupitia Neno la Mungu, kwasababu
kitendo cha moyo wangu kukosa utulivu
kinywa change hakiwezi kuwa sambam,ban a
mapenzi ya Mungu, ndio maana unaweza
kukutana na mkristo aliyeokoka
lakini maneno ya kinywa ni aibu
hata kuyasikiliza.
TAHADHARI
Jambo lolote nisilokuwa na
uwezo nalo kulifanya haitakiwi nimahidi mtu
kwamba nitakufanyia ,kwasababu jambo hilo laweza kuwa mtego kwangu wa
kufunga Baraka zangu siku zote,Hata Biblia imesema katika Mhubiri 5:2.
Kitu cha kuchunga sana nikiwa
kama mkristo shetani anajitahidi kuchunguza
maneno ya kinywa change ilia pate sababu ya kuharibu maisha yangu, ndio
maana Biblia ikatoa tahadhari hii Mithali 6:2.
Juu ya jambo hili Yesu
anisaidie , ninavyonena kinyume na kinywa changu ninaandaa mazingira ya
mgandamizo ambao utayafanya maisha
yangu yapoteze mwelekeo wa Baraka za Mungu, kwahiyo hata kama nimekutana na ugumu kiasi gani katika maisha inatakiwa nikiri
mapenzi ya Mungu peke yake, kwasababu hata kama
Mungu hajafanya haitabadilisha maisha yake.
Mabaya huja katika maisha ya
mtu anayemwamini Mungu kumpima kiwango chake cha kumwamini Mungu,kwahiyo wakristo walio wengi hii siri hawaijui, ndio maana wengi
huangukia katika dhambi ya kumkufuru
Mungu kwa bvinywa vyao.
Jambo la kujua
Kuna magumu mengine au mabaya
mengine au majaribu huja katika maisha yetu kwa lengo zuri la kukusogeza karibu na uwepo wa Mungu ,hata
Biblia imetoa maelezo juu ya hili Yakobo 1:2-3.
(Haitakiwi nisubiri maumivu
ndio nimtafute Mungu kuna gharama zake).
Kila jaribu linalopita katika
maisha yangu ndani yake kuna Baraka za Mungu,ndio maana inatakiwa nisitetereke
katika imani.
Kinywa cha mkristo ambacho hakineni kweli hakina muunganiko wowote nba Baraka
za Kimungu,kwasababu Mungu ni kweli na wote wamwaminio inatakiwa waishi katika kweli.
Anenaye kweli huupendeza moyo
wa Mungu na nafsi ya Mungu huwa karibu na mtu anayenena kweli.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni