Somo la leo :
KWA NENO LAKO.
- Kwanza kabisa inatakiwa moyo Wangu utambue kwamba Neno la Mungu linaishi au li hai kwenye ulimwengu wa Roho, ndio
maana ninaweza kulitumia Neno hilo katika Imani na likafanya muujiza kwa sababu Imani ni kitu cha rohoni.
Luka 5:1- 8
- Neno la Mungu linaisaidia Imani ya mtu kuwa hai kwenye ulimwengu wa Roho, kwa lugha nyingine Neno linaisaidia Imani kuandaa mazingira ya kupokea baraka za Mungu.
- Moyo Wangu unapo kuwa wazi katika kufanya kazi ya Mungu au kusaidia kazi ya Mungu iende mbele, kibibilia natengeneza mafuriko ya baraka zisizo weza kuzuiliwa na kitu chochote, lazima moyo wangu uwe na tahadhari na hilo, kwa sababu watu wengi wameingia kwenye matatizo, watu wengi wameingia kwenye magonjwa yanayo watesa mwanzo mpaka mwisho, hiyo ni kwa sababu ya kumzuilia Mungu kitu anacho kitaka kutoka kwao, Luka 5:1-7 ni picha halisi ambayo Yesu Kristo alikuwa akilifundisha Kanisa kuhusu utoaji Mfano mstari wa 2!unaelezea wazi namna ambavyo Petro hakuhoji kwa kumzuilia Bwana juu ya hitaji alilokuwa akilitaka kutoka kwake vile vile inaonyesha wazi baraka aliyo ipata Petro chanzo chake ni kutoa.
- Baraka inayo toka kwenye uso wa Mungu lazima niiandalie mazingira ya utoaji, kwa sababu utoaji wangu ndio unaoleta muunganiko kati ya mimi na baraka za Mungu, vile vile lazima niruhusu ufahamu Wangu kuelewa jambo hili, je jambo gani ? Jinsi ambavyo baraka za Mungu huanza kwenye maisha ya mtu kujidhibitisha huwa kama mkulima alimavyo shamba.
- Jinsi ninavyoruhusu moyo Wangu kuamini zaidi Neno la Mungu ndivyo Imani yangu inavyo zidi kupata kina kirefu katika Roho.
- Maisha ya baraka zitokanazo na Mungu yanahitaji mambo yafuatayo :-
Zaburi 51:16
i) unyenyekevu wa moyo
ii). Utoaji na
iii).Uvumilivu
- (Uchumi wa mkristo unalindwa na utoaji)
- ( Kina cha Neno kinamsaidia mkristo kujua ukweli kuhusu Mungu, vile vile kwa kila mtu anaye kutana nae)
- Baraka zote ninazo zihitaji chanzo chake ni kwenye ulimwengu wa Roho, maneno haya yanadhibitishwa na Waefeso 1:3.
- Namna ya kujiunganisha na baraka za Mungu ambazo alikwisha nibariki kwenye ulimwengu wa Roho kama inavyo sema katika Waefeso 1:3 inadhibitishwa na kitabu cha
Zaburi ya 126:5,6.
- Zaburi ya 126:5 ni maneno halisi ya mtumishi wa Mungu Daudi akilieleza Kanisa na kulidhibitishia kwamba utoajia unahitaji kujikana nafsi vile vile hauhitaji ushauri kwa mtu mwingine isipokuwa nafsi yako na nafsi ya Mungu.
- ( Tendea kile kitu ambacho moyo wako unaridhia kina baraka).
- Nafsi ya mwanadamu bila Neno la Mungu ina vitu hivi ndani yake :
a) hila b) hasira c) visasi n.k
- lakini nafsi ya Mungu ina: a).Huruma b). Ina rehema c). Ina msamaha, ndio maana inatakiwa moyo Wangu niunyenyekeze zaidi kwenye Neno la Mungu ili nafsi ya Mungu iwe sehemu ya maisha yangu hapo nitayafurahia maisha.
- Kinacho ikimbiza nafsi ya Mungu katika maisha yangu ni dhambi juu ya hili nahitaji kuponywa ufahamu.
- ( Kutoka ndani ya jaribu ambalo tayari lipo katika maisha yangu nahitaji ufahamu wa kina wa Neno la Mungu,kwa hiyo kutokana na sentensi hii inatakiwa nianzishe jitihada za kulazimisha moyo Wangu kufundishwa Neno la Mungu ili uelimike kuhusu Mungu).
- Nikifahamu kanuni za mkulima anavyolima shamba sina haja ya kutilia Shaka baraka za Mungu katika maisha yangu.
- Haitakiwi niingize mashaka katika baraka za Mungu ambazo ameisha nikusudia mimi kwa sababu Bibilia imemfunua mtu mwenye mashaka namna alivyo kama ilivyo andikwa katika Yakobo 1:6b.
- Baraka za Mungu zina hitaji mtu jasiri mvumilivu.
- Neno la Mungu linatazama mtu mwenye Imani ili litimize makusudi ya Mungu juu ya maisha yake.
MAFANIKIO YA WATU WENGI YAMEZUILIWA NA MANENO WANAYO TAMKIWA.
- Maneno mengine ambayo wakristo hutamkiwa huwa kama uchawi na maneno haya yamefunga sana mafanikio ya wakristo wengi, ndio maana watu wameokoka lakini wana maisha magumu, na mara nyingi maneno haya hutamkwa na watu ambao hawana Roho ya kusamehe.
- ( Mtu ambaye hana Roho ya kusamehe hawezi kuwaza mema ndani mwake kwa sababu moyo wake unakuwa umejaa visasi na hila).
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni