Jumapili, 24 Januari 2016

KAA KATIKA UWEPO WA MUNGU


KAA KATIKA UWEPO WA MUNGU

- Nikiwa kama mkristo ninaye mwamini Mungu inatakiwa niruhusu hali ya kukua kiufahamu kwa sababu baraka za Mungu huja kwa njia ya ulimwengu wa Roho, kwa
hiyo nisipo kuwa na ufahamu wa haraka wa kupambanua naweza kujikuta napishana na baraka za Mungu, yaani wakati wa mimi kubarikiwa najikuta niko nje ya uwepo wake, lakini ukweli ndio huu baraka za Mungu zi dhahiri juu ya mtu yeyote ambaye ameutia moyo wake ufahamu kuhusu Mungu, ndio maana kitabu cha Waefeso 1:3 inadhibitisha wazi baraka za Mungu jinsi zilivyo wazi katika maisha ya mtu ambaye ameokoka.

- ( Baraka za Mungu zilishakuwepo tayari au kwa lugha nyingine zipo tayari, shida ni kwamba mimi binafsi nina kosa upeo wa kupambanua ili ziwe halisi kwangu). 

- Ili niweze kuumiliki uwepo wa Mungu, inatakiwa niwe na mtembeo wa Roho Mtakatifu.

- Mtembeo wa Roho ndio unao weza kudhibitisha makusudi ya Mungu katika maisha ya mtu.


- Kuumiliki uwepo wa Mungu kunahitajika ufahamu wa kina wa Neno la Mungu, kwa hiyo hii point inaonyesha dhahiri umuhimu wa kujifunza Neno la Mungu. 1 Wakorinto 2:10.

Hakuna maoni: