Jumapili, 17 Januari 2016

ACHA KUKATA TAMAA


ACHA KUKATA TAMAA.

- Kwanza kabisa inabidi nifahamu Kukata tamaa ni dhambi.

- Mtu yeyote anaye kata tamaa maana yake ndani mwake hamwamini Mungu kabisa.


- Kukata tamaa kuna dhihirisha  wazi moyo wa mtu ulivyo mbali na uwepo wa Mungu

- ( Kukata tamaa ni sehemu ya kumjeruhi Roho Mtakatifu, kwa hiyo ni vigumu kupata mpenyo katika maono uliyo nayo.)

- Bidii yangu niliyo nayo katika kumtafuta Mungu, ndio inayo tengeneza wepesi vile vile mahusiano ya karibu na baraka za Mungu.

- Bidii ya mkristo katika suala la kumcha Mungu ndio ambayo  ina ufanya moyo wa Mungu kuwa wazi kwake yaani kujifunua, kwa sababu bidii huambatana na tendo la uaminifu haya maneno ameyasema Ayubu 8: 5 na kuendelea.

- ( Kila jambo ninalo lifanya maana yake linahitaji mwongozo wa Roho Mtakatifu ndipo liwe na wepesi wa kuzaa baraka.)

- Ninapo liamini Neno la Mungu haitakiwi nilitilie mashaka, kwa sababu laweza kugeuka na kuwa adui yangu, na hili jambo liliwakuta wazi wana wa Israeli kama inavyo sema wazi katika Isaya 63:9-10

- Nikiwa ni mkristo mwenye Imani na Yesu Kristo inatakiwa niamini hata kama mbele yangu hakuna mpenyo kwa sababu Mungu si mwanadamu hata aseme uongo.

- Jambo lolote ninalo lifanya lazima nihakikishe liwe katika Imani ndipo litakapo dhibitika liwe katika uhalisia.

- Kukata tamaa kunaonyesha wazi jinsi ulivyo mjinga kwenye uwepo wa Mungu, kwa sababu mtu asiye liamini tamko la Neno la Mungu Biblia imemfananisha  ni sawa sawa na mpumbavu, vile vile mtu anaye kata tamaa hana anacho sikia kutoka kwa Mungu.

- Hata kama lile ninalo likusudia kutoka kwa Mungu halijadhibitika kwangu inatakiwa niongeze bidii katika kuamini.

- Jambo hili ni la kujichunga nalo sana, moyo Wangu ukisha ingiza hali ya mashaka maana yake tayari nimeangukia katika mikono ya uharibifu, hata ikitokea bahati mbaya nimejikwaa kwenye uso wa Mungu haitakiwi niukimbie uso wa Mungu, bali inatakiwa niurejee uso wa Mungu ili nipate Rehema sawa sawa na Neno lake linavyosema katika  Mithali 28:13


- Mwanzo wa mkristo kuanza kutembea na baraka za Mungu ni pale anapotubu dhambi.

Hakuna maoni: