JIENDELEZE KIROHO
- Kujiendeleza kiroho kuna msaidia kila amwaminie Mungu kuwa chini ya utawala halisi wa Roho Mtakatifu, kwa sababu maisha
ya mkristo aliye okoka yanahitaji mwongozo wa Roho Mtakatifu, hili jambo Bibilia imelielezea kwa kina kupitia. Yohona 14:25,26
- ( Roho Mtakatifu ananitegemea mimi nimpe mwongozo atende juu ya jambo fulani ).
- Kushindwa kumtumia Roho Mtakatifu kunatokana na udhaifu wa kiimani alio nao Mkristo kwenye ulimwengu wa Roho.
- Imani ni daraja linalo weka mahusiano kati ya mtu na Mungu, ndio maana katika suala la Imani Mungu hakuliwekea mipaka kwa waaminio, hata Biblia inaelezea kwa kina hili jambo. Mathayo 17:14-20
- Tatizo la Imani za wakristo zinashindwa kufanya kazi kwa sababu zimepigwa upofu na dhambi
- Jambo la kufahamu nikiwa mwamini nikitaka kupata muunganiko wa matendo makuu ya KiMungu inatakiwa kwanza niisafishe dhambi iliyoko katika maisha yangu, hapo ndio mwanzo wa mamlaka iliyoko ndani yangu kutenda kazi.
- Mkristo atakaye ishi maisha ya ukweli huyo ndio mkristo atakaye ugusa moyo wa Mungu, baraka za KiMungu kwake hazitakuwa na maulizo
- Jinsi Imani ya mtu inavyo kua kwenye ulimwengu wa Roho ndivyo inavyo leta muunganiko wa Mungu na mtu kuwa Karibu zaidi.
- Kujiimarisha vizuri katika Roho ndio njia pekee inayo leta muunganiko kati ya mtu na Mungu kwa sababu Mungu huitegemea Imani iliyoko ndani ya moyo wa mwamini kumpa ujumbe.
- Hivi kwa nini Yesu Kristo aliwaelezea wanafunzi wake wazi wazi bila kificho kuhusiana na muujiza walio shindwa kutenda kama inavyo sema Mathayo17:16,17
- Upungufu wa Imani ulioko katika maisha ya mkristo hata kama ameokoka ni kizuizi namba moja kinacho yafanya maisha ya mkristo yakose mwelekeo kwenye ulimwengu wa Roho, vile vile maisha ya mkristo huyo hayawezi kushinda hali ya uvamizi isipo kuwa ameiboresha Imani upya kupitia Neno la Mungu.
ANGALIZO no 1
Nikiwa ni mkristo niliye okoka inatakiwa kila jambo ninalo lifanya liwe lina mwongozo wa KiMungu, tofauti na hapo nikilazimisha nihakikishe niwe tayari kulipa gharama.
- Maisha ya dhambi ndiyo yanayo Funga masikio ya kiroho nisisikie Mungu anasema nini na mimi.
- Kuna umuhimu wa kubuni mbinu za kujiongeza kiimani, hata Yesu Kristo mwenyewe aliwapa siri wanafunzi wake wazi wazi kama inavyo sema katika maandiko matakatifu,
Mathayo 17:14 - 21, lakini katika mstari wa 21 ndipo amefunua wazi ni mbinu gani zitakazo mfanya mkristo Imani yake iimarike katika Roho.
- Maisha ya mkristo yana anza kuchanua kwenye ulimwengu wa Roho kabla ya mwilini, kwa hiyo itatakiwa nifanye mambo yafuatayo na mambo hayo ndio yatakayo ifanya Imani yangu kuongezeka zaidi kwenye ulimwengu wa Roho
i). Kusoma Biblia
ii). Kufunga
iii). Kuomba
Hizi njia tatu kwa lugha ya kiroho zinaitwa mazoezi ya kiroho.
UFAFANUZI KUHUSIANA NA KUSOMA BIBLIA
- Kwanza kabisa inabidi nifahamu Biblia ninayo isoma usiku na mchana ni Neno la Mungu,kwa hiyo inao uwezo mkubwa wakunijua mimi hata kama ninaisoma .
- Biblia ni njia pekee inayo elezea siri za Mungu kwa undani katika maisha ya wanao mwamini Mungu.
- Ili kilicho andikwa ndani ya Biblia kiwe halisi kwangu inatakiwa nihakikishe ninatumia hekima na busara wakati wa kuisoma Biblia kwa sababu Biblia ni Mungu anazungumza.
- Biblia inahitaji mtu ambaye ana utulivu ndani ya moyo ndipo ambapo utaielewa.
- Ndani ya Neno la Mungu kuna uhai na uzima kwa mkristo anaye amini haya maneno hata Biblia imeyazungumza katika kitabu cha Waebrania 4:12,vile vile kuna maonyo na urejesho.
- Haitakiwi niukimbie uso wa Mungu kwa sababu nina udhaifu fulani, bali inatakiwa ninyenyekee chini ya neno la Mungu ili nipewe mbinu ya kuushinda udhaifu Wangu.
- Ninapo enda kinyume na kile ambacho Neno la Mungu linanielekeza maana yake ninapingana na mapenzi ya Mungu, ehh Yesu nisaidie.
- Kusoma Biblia kunasaidia kuleta muunganiko na Roho ya mafunuo.
Maelezo kuhusiana na usomaji wa Biblia yameishia hapa.
UFAFANUZI KUHUSIANA NA KUFUNGA
- Kufunga ni njia inayo msaidia mkristo kupata hali ya utiisho kwa sababu maisha tunayo ishi chini ya mbingu yapo katika mamlaka ya mwili, ndio maana paulo mtume alizungumza wazi katika kitabu cha Wagalatia 5:25, hii yote ni kwa sababu ya kuwapa ufahamu wakristo wanao mwamini Yesu Kristo, ili wayatambue mapenzi ya mwili kabla hayajaleta athari katika maisha yao ya kiroho.
- Mungu anamheshimu sana mkristo anae unyima mwili wake haki yake kwa sababu ya Mungu, na haki ya mwili ni:
1. Starehe
2. Chakula
3. Usingizi
- Ukiyatii mapenzi ya mwili hauwezi kuyatimiza matakwa ya Mungu, kwa sababu katika mwili huwa kunapatikana mambo ambayo yako kinyume kabisa na mapenzi ya Mungu hata katika Biblia imeyasema katika Wagalatia 5: 19
- Mkristo anaye taka kuwa mpya kwa Mungu na anaye taka kuyazika matendo ya mwili wake ili awe ni mkristo mwenye kuthaminika na kusikilizwa na Utatu Mtakatifu inatakiwa asimame katika msingi huu, na msingi huu una patikana katika Wagalatia 5:22-26
- Mungu anazungumza na kila mwamini anae simama sambamba na mapenzi yake.
Mwisho wa maelezo kuhusiana na kufunga.
UFAFANUZI KUHUSIANA NA KUOMBA
- Maombi ni mazungumzo kati ya mkristo mwenye Imani na Mungu
- Ili maombi ya mkristo yawe na nguvu ni kuhakikisha maombi hayo yamesimamia misingi ya Neno la Mungu, inaonekana wazi katika Yohana 17:1-26 ni sehemu ya maombi aliyo yaomba Yesu Kristo au kwa lugha nyingine alikuwa akilifundisha Kanisa misingi ya maombi yao yasimamie Neno la Mungu
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni