Somo la leo: 13/12/2015
MAOMBI YANAYO POKELEWA NA MUNGU.
- Kwanza kabisa inatakiwa nifahamu kwamba Mungu ni Roho, kwa hiyo inatakiwa muombaji awe anaishi katika mazingira ya
rohoni ingawa ameuvaa mwili sambamba na Neno
Wagalatia 5:25 na Yohana 4:24
- Yohana 4:24 inadhihirisha wazi muombaji anatakiwa awe anaishi maisha ya ukweli yaani maisha ambayo ni sambamba na mapenzi ya Mungu.
- ( Maisha ya ukweli ndiyo yanayo vuta baraka za Mungu katika maisha ya mtu )
- ( Kuishi maisha ya haki inatakiwa niikane nafsi yangu ).
- ( Roho Mtakatifu anatembea na mkristo anaye ishi maisha ya haki, vile vile anaye jirudi haraka akigundua amekosea, ndio maana katika Isaya 1:17-18
- Kumtunza Roho Mtakatifu katika maisha yangu inatakiwa niidhibiti nafsi, yaani kujinyima vitu ambavyo ninaviona nina haki kuvitumia.
- Nikitaka kuambatana na Roho ya kutenda mema ndani mwangu, inatakiwa nifanye mambo yafuatayo:
i). Kujifunza Neno la Mungu
Maelezo kuhusu no.( i )
- Kujifunza Neno la Mungu kunaleta msaada wa kuielimisha Roho ya mkristo aliye okoka iwe na mambo yafuatayo :
a). Utu
b). Imani
c). Aibu
d). Huruma. n.k
- Kama wewe ni mkristo uliye okoka inatakiwa uieshimu nafsi ya Mungu kwenye maisha yako hapo ndipo utaziona baraka za Mungu zikitiririka kama mafuriko ya mto.
- Hata kama nina kipindi kigumu namna gani inatakiwa Tumaini langu liwe kwa Yesu Kristo kwa sababu msamaha wa dhambi unatoka kwake, uzima wa milele unatoka kwake,baraka na utajiri vinatokana kwake, na kila ambacho macho yangu yanakishihudia ni mali yake kwake, kwa hiyo sina sababu ya Kukata tamaa bali kulitazama Neno linasema nini. ..."??????
- Nikijituliza chini ya nafsi ya Mungu, baraka nitakazo zipata kila mmoja atanitungia jina
ii). kukubali kuonywa
Maelezo kuhusiana na no.ii
- Tatizo linalo kumba Kanisa la leo sana sana jamii ya waaminio, hawataki kuonywa au kukosolewa wanapo kosea.
- Ukweli ni kwamba kila mwanadamu anaye ishi mwilini amepungukiwa na utukufu wa Mungu, hilo liko wazi lakini mkristo anapo kubali kuonywa au kukosolewa dhidi ya udhaifu alio nao mara nyingi huwa ndio mwanzo wa yeye kupiga hatua katika mafanikio.
- Mkristo anaye kubali kukosolewa huwa anafunikwa na uwepo wa Mungu, ndio maana kitabu cha 2 Timotheo 2:14 anasema wazi.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni