Jumapili, 29 Novemba 2015

NAMNA YA KUYAREJEA MAPENZI YA MUNGU


NAMNA YA KUYAREJEA MAPENZI YA MUNGU.

- Huu ni ukweli wakristo wengi walio okoka wanatembea nje na mapenzi ya Mungu, juu ya hili tunahitaji rehema na Neema za Mungu.

- Ni vigumu kuzilingana baraka za Mungu nikiwa nina tembea nje na mapenzi ya Mungu.

- Ukweli ni kwamba baraka za Mungu zinamtambua mtu ambae yuko katika mtiririko wa ucha Mungu, sasa basi kinacho wakuta wakristo wengi wanazitamani sana baraka za Mungu lakini wakati huo huo wako nje ya system ya Mungu.

- Nikitaka kubarikiwa na Mungu inatakiwa niyarejee kwanza mapenzi ya Mungu, kwa hiyo kitendo cha kuyarejea mapenzi ya Mungu kwa lugha nyingine ni kutambulikana na Utatu Mtakatifu, ndio maana Biblia ikasema.  Yohana 1:12.

- Tatizo langu mimi nina muomba Mungu na wakati huo huo niko nje na mapenzi yake, ndio maana hata maombi yangu hukawia kujibiwa.

- (Maisha yanahitaji ufahamu wa kiroho zaidi)

-  Mkristo ambaye siku moja anatamani auone uso wa Mungu inatakiwa ahakikishe maisha yake yanaenda na kama  Neno la Mungu linavyo sema, kwa lugha nyingine huyu anaweza akaitwa mkristo aliyeko katika system ya Roho Mtakatifu.

- Kama ninataka Mungu anitambue na niwe na haki za kubarikiwa kama wana wa ufalme, inatakiwa niyaishi maandiko.

- ( Kuyaishi maandiko ni kujinyima vitu ambavyo ni haki yako kuvipata, na jambo hili linahitaji zaidi Neema ya Mungu ) 

- Pigo lililo wapata wana wa Israeli ni pale ambako hawakutaka kumwamini Mungu na Musa pia wakajikuta wanaangukia katika dhambi ya kutokuamini, ambayo kibiblia inaitwa kumkufuru Roho Mtakatifu ndio maana Roho Mtakatifu aliwageuka.
Kama inavyo sema katika Isaya 63:9-10

- Maangamizo mengi yanayo wakuta wakristo tena jamii ya waaminio ni kujikwaa kwa Roho Mtakatifu.

NINI KIFANYIKE ILI NIRUDI NIAMINIKE UPYA

- Ili niweze kuaminika upya kwenye uso wa Mungu inatakiwa nifanye mambo yafuatayo:-

    a). Kudhibiti nafsi, kwa sababu nafsi ya mtu imekuwa kichocheo kikuu kinacho fanya maisha ya mtu kuharibikiwa, na mara nyingi kuna mambo ambayo nafsi imeyabeba, na mambo haya bila kina cha Neno la Mungu kwenye moyo wa mtu huwezi kuyatiisha.
    i). Nafsi imebeba hisia, 
    ii). Nafsi imebeba akili   iii). Nafsi imebeba Utashi 

- Ili Roho Mtakatifu asiwe adui yangu inatakiwa nitendee kazi mwongozo wa Neno la Mungu

- Nikiwa kama mkristo inatakiwa hazina ya moyo Wangu niielekeze katika Neno la Mungu kwa sababu pesa,magari,majumba, mali za kimwili zina mwisho lakini Neno la Mungu halipiti wala halina mwisho milele na milele, ndio maana hata Mungu akasema wazi katika kitabu cha Yeremia 1:12

  b). Kutawala Moyo

- Ni vigumu kuutawala moyo Wangu kama sina vitu hivi vifuatavyo :-

  i). Ufahamu wa rohoni 

  ii). Maarifa ya Neno la Mungu. 

- Biblia ilishadhibitisha kwamba moyo ni mdanganyifu katika Yeremia 17:9 sasa basi ikiwa mimi ni mkristo ninaye mtafuta Mungu inatakiwa nielekeze moja kwa moja nia ya moyo Wangu katika Neno la Mungu, ili niweze kupambanua mawazo ya moyo Wangu kabla ya kuchukua hatua juu ya jambo lolote ninalo kusudia kulifanya.


Hakuna maoni: