TAWALA FIKRA.
SEHEMU YA 2.
CHANZO CHA FIKRA ZA MTU KUPOTOKA.
- Chanzo cha fikra za mtu kupotoka ni kuwaza vibaya.
- ( Kuwaza vibaya kibibilia ni kumdhihaki Mungu,kwa sababu katika kuwaza vibaya hakuna Imani bali kuna uharibifu ).
- Kama ningelifanya Neno la Mungu kuwa chakula halisi cha roho yangu hakika nisingewaza vibaya nje na mapenzi ya Mungu hata kama ninaishi katika mwili.
- Tatizo linalotukumba wakristo wengi hatuiamini Biblia kama kweli ni Mungu anazungumza ndani yake, bali tunachukulia tu ni kitabu kinachotupa mwongozo wa kumwomba Mungu,lakini
kama ningefahamu uthamani ulioko ndani ya Biblia ningeishi maisha hata zaidi ya mfalme chini ya mbingu.
- Acha kuwa kivuli kwenye uwepo wa Mungu bali kuwa halisi.
- Neema ya Mungu niliyo pewa ni upako yenye uwezo wa kulazimisha chochote kikatokea ndio maana inatakiwa nijiimarishe katika uwepo wa Mungu.
- ( Nguvu za kiroho zinaongezeka kadri mwamini anavyo ongeza bidii ya kusoma Neno la Mungu)
- Kitabu chenye uwezo wa kuponya fikra za mkristo zilizo athirika na shida, mateso ni Biblia ndio maana ndani ya kitabu hiki kuna roho ya utiiisho.
- Huu ni wakati wa kulirejea Neno la Mungu kwa sababu umilele upo ndani ya Neno la Mungu, hata maandiko yamedhibitisha maneno haya. (Yohana 1:1-3 )
- Mtu anayesoma Neno la Mungu kabla ya kulala na akalitumia Neno hilo hilo kwenye kuomba anakuwa ameiunganisha roho yake na Mungu yaani ni rahisi kupewa maelekezo na Mungu katika maeneo yafuatayo :-
i ). Kuonywa dhidi ya namna anavyo kosea
ii ). Kupewa ndoto za kumwepusha na alicho kusudiwa na shetani.
iii). Kupewa taarifa kuhusu Kesho juu ya yatakayo tokea katika maisha yako, ndio maana kuna mtu mwingine unaweza kumsikia anasema, roho yangu ilikuwa inasita kupanda hili gari lakini nikalazimisha kupanda sasa ona tumepata ajali ,hilo husababishwa na watu wengi kutokuwa na roho ya kupambanua ingawa wanamwamini Mungu.
iv). Hakuna jambo linalo weza kukukumba bila taarifa.
- ( Amani ya kweli iko ndani ya Neno la Mungu )
- Matatizo yangu inatakiwa niyaeleze Neno la Mungu kwa sababu hakuna mwanadamu mwenye jibu la tatizo langu.
- Nikitambua ninaishi kwa sababu ya Neno la Mungu, inatakiwa niyachukue maisha yangu yote niyavalishe Neno la Mungu, Ee Yesu nisaidie katika haya maamuzi.
- Fikra za mkristo anaye mtegemea Mungu asipokuwa chini ya mwongozo wa Neno la Mungu maono yake hayawezi kutimia kwa sababu Neno la Mungu limepewa nafasi pekee ya kuyaelimisha na kuyabariki maisha ya kila anaye mwamini Mungu, vile vile ndilo linalo dhibitisha uumbaji wa kila kitu chini ya jua.
NAMNA YA KUDHIBITI FIKRA ZANGU ZISIPOTOKE.
- Ili niweze kuzidhibiti fikra zangu zisipotoke inatakiwa niutiishe moyo Wangu chini ya muongozo kamili wa Neno la Mungu, hii itanisaidia kama mkristo nitakapo kutana labda na majaribu, maana katika kipengele cha kujaribiwa watu wengi ndipo wanapo potokea hapo
- Haitakiwi niruhusu fikra zangu kupotoka kwa sababu ya majaribu ninayo kutana nayo, bali inatakiwa ni mwamini Mungu wakati wake katika maisha yangu yatatimia ndio maana akasema hadharani kupitia kinywa cha Nabii Yeremia 23: 23-24.
-( Nisipo tendea kazi mwongozo ninao pewa kuna hatari ya kudhalilika. )
- Kuanzia leo ninaanza kufanya maamuzi magumu, kwa sababu maamuzi magumu ndiyo yatakayo nifikisha kwenye mafanikio.
- Ikiwa ninafahamu chanzo cha maisha yangu ni Neno, inatakiwa nifanye mambo yafuatayo:-
a). Kuruhusu moyo wangu kuambatana na Neno.
b). Kuhakikisha jambo lolote ninalo lifanya katika maisha yangu kulipima kwanza katika Neno la Mungu ili nipate usahihi.
c). Kabla sijafanya maamuzi juu ya kitu chochote niliulize Neno kwanza, hapo nitaitwa mkristo niliye yaelekeza maisha yangu katika mwongozo wa Neno la Mungu.
- Bidii yangu katika kujifunza mambo ya KiMungu ndiyo itakayo nisaidia kuniunganisha kwa Karibu na baraka za KiMungu lakini inatakiwa niwe na tahadhari katika maeneo yafuatayo:-
a). Maneno ya kinywa changu
b). Mawazo ya moyo wangu
c). Matendo ya kila siku katika maisha yangu, hapa nikitimiza haya ndio unaokuwa mwanzo wa maisha yangu kupata kibali, vile vile na mwendelezo wa kubarikiwa tu Amen.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni