13/9/2015 Somo la kwanza.
MAZINGIRA YA MWAMINI KUAMINI
A). Mfumo wa Neno
B). Mfumo wa tendo la Imani.
- Mazingira yangu katika kuamini inatakiwa niyaimarishe zaidi katika mahusiano na maandiko matakatifu, kwa sababu mahusiano ya mtu na maandiko ndiyo yanayo zaa matunda, jambo hili lipo wazi hata katika Biblia kwenye kitabu cha Mwanzo 1: 1 - wakati Mungu anaumba mbingu na nchi.
- Swali: Je Mungu aliumba Nuru katika mazingira gani?
Jibu: Mungu aliumba nuru katika mazingira ya Neno ndani ya Imani itendayo kazi.
- Tatizo linalo leta ugumu katika maisha ya wakristo tunaamini katika mwili sio katika hali ya kiroho ndio maana wakristo wengi tunakosa wepesi na mipenyo ingawa tuna bidii katika maisha, haya mazingira yalimkuta mwanafunzi wa Yesu Tomaso.
- Je nitajuaje mwamini huyu anaamini katika mwili na huyu anaamini katika roho?
ANGALIZO NO 2.
Maisha ya kimwili yanategemea sana maisha ya kiroho, kwa hiyo nisipo kuwa makini nikajiimarisha katika roho nikashindwa kwenye ulimwengu wa roho, basi katika mwili kuna hatari ya kufutika kwenye uso wa dunia, katika hili nahitajika kujipanga upya.
- Suala la kujiimarisha kiimani ni suala linalo mwongezea mwamini ufahamu katika kumjua Mungu, mara nyingi na hapo ndo unapotokea mwanzo wa wepesi katika maisha ya mtu.
Ayubu 22:21
- Nikipoteza amani katika moyo Wangu muunganiko wangu na Roho Mtakatifu utatoweka, hili jambo lilimkuta wazi wazi Yona Mtumishi wa Mungu.
- Mwanzo wa dhambi katika maisha ya mtu ni kupoteza uwezo wa kumsikia Roho Mtakatifu.
- Kitu cha kuchunga katika maisha yangu ni kuilinda sana sauti ya Roho Mtakatifu kuliko dhahabu na mali.
- Kanuni ya mwamini ni kumtukuza Mungu katika maumivu vile vile na katika raha unazo zipata.
- Kumjua sana Mungu kunampa mwamini nafasi ya kufurahia maisha na baraka za KiMungu katika mazingira ya kimwili kwa muda mrefu.
- Mema ya nchi hayaji katika maisha ya mtu bila mtu kuikana nafsi yake.
NINI KIFANYIKE ILI NIDUMU KATIKA IMANI
- Ili niweze kudumu katika Imani inatakiwa nifanye mambo yafuatayo nikiwa kama mwamini:-
i). Nikubali kuonywa
ii). Nikubali kukaa chini ya mwongozo wa maneno ya Mungu
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni