30/8/2015
SOMO LA LEO : TAWALA FIKRA
- Nikiruhusu fikra zangu zitafakari matatizo, basi Imani yangu itakuwa na nguvu ya kulazimisha matatizo hayo kuwepo yaani kuwa halisi katika maisha ya mtu, kwa sababu Imani ya mtu inatenda kazi kutokana na jinsi anavyo amini na vile vile anavyo tafakari katika fikra zake.
- ( Kiungo kikuu cha dhambi katika maisha ya mtu ni moyo, kwa sababu kitu ambacho moyo utakitafakari ndicho ambacho kitadhibitika, ndio maana Biblia ikasema wazi katika Yeremia17:9)
- Inatakiwa nijiwekee mazoea ya kulitafakari Neno la Mungu mara kwa mara katika moyo wangu, ili kinywa changu kiweze kutoa hekima na busara, kwa sababu hakuna hekima yenye nguvu popote pale nje na Neno la Mungu ( mapenzi ya Mungu ).
- ( Hekima ni Neema inayotoka katika Neno la Mungu )
- ( Ili niweze kuyatambua mawazo ya moyo Wangu, inatakiwa niwe na mahusiano mazuri na Neno la Mungu, kwa sababu hali yakutafakari katika moyo wa mtu inatokana na namna ambavyo anafikiria juu ya jambo fulani ).
- ( Maumivu yaliyoko katika maisha yangu yanatokana na jinsi ninatafakari kinyume na Neno la Mungu.)
- Afya za wakristo wengi zinaathirika kwa sababu ya Imani kushuka, Imani ikiwa juu kamwe hakuna jaribu la magonjwa lenye uwezo wa kutikisa mwili wa mtu ( Afya ya mtu ) ndio maana inatakiwa niwe mtu wa kulitafakari Neno la Mungu mara kwa mara kwenye moyo Wangu ili shetani asipate nafasi ya kuingiza udhaifu ndani mwangu.
- Kuanguka ni rahisi kuliko kusimama na ndivyo ilivyo kuugua ni rahisi kuliko kupona, kwa hiyo ili niweze kushinda hali ya kuathirika inatakiwa niboreshe mahusiano yangu mimi na Neno la Mungu, na hii inatokana na Biblia kunidhibitishia kwamba Neno la Mungu ni tiba ya afya yangu. Mithali 4: 20-23.
- ( Neno la Mungu ni ulinzi kamili kwa Afya ya mkristo anaye mwamini Yesu Kristo )
ANGALIZO No. 1
Bila Neno la Mungu chini ya jua hili kuna hatari ya kuishi kama mtumwa wa matatizo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni