Jumapili, 13 Septemba 2015

NAMNA YA KUYAEPUKA MAJARIBU

13/9/2015 Somo la pili.
NAMNA YA KUYAEPUKA MAJARIBU 

- Kuna njia moja ya kuepuka majaribu, na njia hiyo ni kufuata matakwa ya maneno ya Mungu yaani Neno la Mungu, katika hili
kunahitajika kina cha ufahamu katika kulijua Neno.

- Inatakiwa nifahamu njia mojawapo zinazoweza kusababisha majaribu katika maisha yangu:-
 A). Kupimwa Upendo nilio nao kwa Mungu.
 B). Uonevu wa shetani
 C). Mungu ananifundisha kitu,

- Nikitaka kufahamu mambo haya kwa kina nisome kitabu cha Yakobo 1: 2

- Kufurahia hali ya jaribu unalo kutana nalo katika maisha, ni kitendo kinacho onyesha Upendo halisi alio nao mkristo kwa Mungu, yaani kibiblia nitaitwa mtenda Neno Yakobo 1:2.

- ( Jaribu linapokuja katika maisha yangu maana yake lina niandalia mazingira ya baraka kubwa katika maisha yajayo ,kwa hiyo haitakiwi  ninene kwa upumbavu ninapo kuwa katika kipindi cha kujaribiwa ).

- (Jambo la kufahamu, hakuna jaribu linalo kuja kwangu likapita uwezo wa Imani yangu, bali kila jaribu linakuwa chini ya Imani yangu , kinacholeta shida ni mimi kushindwa kuifanyia Imani yangu mazoezi ili muda wote iwe na uwezo wa kukabiliana na majaribu.
1 wakorinto 10:13 ). 

ANGALIZO No. 1
- Kama sifanyi mazoezi ya Imani nikaja kukutana na majaribu hapo ndipo Nitatambua uthamani wa kumtafuta Mungu.

- ( Nikiwa mzembe katika masuala ya KiMungu, kuna hatari ya kuwa mlango wa matatizo )

- Nikitaka kushinda jaribu yaani vita vya kiroho, haitakiwi niruhusu hali ya kupoteza utulivu ndani yangu kuhusu Mungu.

- Ili niweze kushinda kila aina ya jaribu, ni kulinda utulivu ndani ya moyo Wangu usivurugike, kwa sababu utulivu ukivurugika ndani ya moyo shetani huingiza mawazo mabaya na ndio mwanzo wa uharibifu unapo anzia. 


- Neno la Mungu ndilo lenye uwezo wa kusema ukweli kuhusu maisha ya mtu hapa chini ya jua.

Hakuna maoni: