Ijumaa, 18 Septemba 2015

MOYO

SOMO LA MKESHA :- 18/9/2015

BY :- MTUMISHI BAB G POWER


MOYO 

- Moyo wangu hauwezi kutenda haki kama hauna ujuzi wa kweli wa maandiko matakatifu.

- Nguvu ya Roho katika maisha ya mtu, inatokana na roho ya mwamini kuwa msafi.

- Ni vigumu kuusafisha moyo nisipoweka mikakati ya kuufundisha maneno ya Mungu.

- Nikiona moyo wangu unaniwekea uzito wa kusoma Maneno ya Mungu nifahamu wazi kwamba umesha tawaliwa na ufalme wa giza, kwa hiyo ili kuepuka athari za kuharibikiwa inatakiwa nijilazimishe kusoma  Biblia hata kama niko na mazingira magumu.

- Makosa tunayo yafanya kama wakristo ni kukubali kwa haraka mawazo ya moyo wangu bila kuruhusu ufahamu wa Neno la Mungu kupambanua ili kupata usahihi wa mapenzi ya  Mungu ni yapi katika hilo ninalo wazia. 

- (Nikiwa ni mtu wa kuliuliza Neno la Mungu kabla ya kutoa maamuzi, siwezi kukwama kwenye maisha, kwa sababu Jibu litokanalo na Neno la Mungu ni kweli siku zote).

- Ufahamu wangu ukiwa ni mdogo, hata uelewa utakuwa mdogo, vile vile ujuzi katika Maneno ya Mungu utakuwa mdogo pia, Wakristo wa kizazi hiki wako namna hii.

- Swala la Kukuza ufahamu ni la muhimu sana kwa mtu ambaye ameamua maisha yake yaongozwe na Mungu.

- (Mtu mwenye malalamiko mengi katika kinywa chake, ni mvivu wa kufikiria.) 

- Mvivu wa kufikiria hana upeo wa kuona mbali, ndio maana watu wengi hufa na visasi katika mioyo yao.

- ( Kuwa na kisasi na shetani, kwa sababu ndiye chanzo cha dhiki yangu )

- Shetani wa kwanza yuko ndani ya moyo wangu, kwa hiyo inatakiwa nipambane nae mpaka atoe utawala wake katika moyo wangu, ndipo nitapata nafasi ya kutafakari Neno la Mungu kwa usahihi.

- Neno la Mungu linaleta faida katika moyo wa mwamini ambaye ni Safi. Zaburi 51:17

- Nikitaka kushinda vita vya kiroho kwa kishindo haitakiwi niruhusu moyo wangu kutafakari hali ya ugumu niliyonayo au majaribu ninayo pitia. 

- Mkristo atakayeweza kushinda vile vile kupata baraka za Mungu kweli kweli ni yule atakaye ufundisha moyo wake kuwa na uvumilivu.

 - Kitu ambacho anafanya mtu haijalishi kibaya au kizuri, maana yake amekubaliana na moyo wake, sasa basi suala la kukosa amani katika kitu hicho ni kiashiria tosha kwamba kiko kinyume na mapenzi ya Mungu.

- Tunashindwa kuwa na uvumilivu kwa sababu macho ya kiimani yana upofu.

- Nikimwambudu Mungu katika upofu wa kiimani ni vigumu Kuabudu
 katika usahihi, yaani Kuabudu sambamba na mapenzi ya Mungu. 

NINI KIFANYIKE ILI MOYO WANGU UWE KATIKA HAKI ?

- Ili Moyo wangu ubaki katika haki inatakiwa nifanye mapinduzi ndani mwangu yenye maamuzi magumu, maana yake nini? Itatakiwa nikubali kupata hasara ya mambo mengine kwenye maisha, ili kuilinda hekima ya Roho Mtakatifu iliyoko ndani mwangu.

- Inatakiwa Yesu awe Bwana katika nyakati zote, yaani katika Mapito na katika furaha, hapo utaitwa Mkristo ambaye umekua kiimani. 

- Inatakiwa niwe makini na kinywa changu, kwa sababu kila jaribu linalo kuja lina kusudi la Mungu nyuma yake, kwa hiyo suala la kulinda moyo ni muhimu sana. 

- Watu wengi ni wavivu katika kutendea Maneno ya Mungu  kazi, ndio maana swala la wao kuongezeka au kukua kiroho ni gumu. 

- Mafanikio ya mtu yanakuja au kuongezeka kutokana na anavyozidi kukua kiimani( kiroho ).

- Mafanikio ya mtu yanatokana na bidii aliyo nayo mtu katika maeneo mawili:- 
   i). Kutendea kazi mwongozo.
   ii). Kuyaweka Maneno ya Mungu katika vitendo.

- Hakuna mwamini atakaye weka maneno ya Mungu katika vitendo akaacha kufanikiwa hayupo, kwa sababu vitendo huonyesha ukomavu wa ufahamu alio nao mtu. 

- ( Imani yangu ikiwa imeimarika katika Mungu haiwezi kuruhusu matendo yaliyo kinyume na mapenzi ya Mungu).

- Nikijiona bado nina madhaifu katika matendo nijue wazi inatakiwa nijiongeze kiufahamu zaidi ili niweze kuendana na Baraka za Mungu. 

- Wakati mwingine makosa tunayo yakosea kwenye uso wa Mungu ni chanzo cha kuchelewesha baraka zetu.


Hakuna maoni: