Jumapili, 23 Agosti 2015

IMANI,ROHO,NENO

 23/8/2015
SOMO:          IMANI,ROHO,NENO.

- Imani,Roho,Neno kibiblia huu ni utatu Mtakatifu, kwa sababu Imani ina mwakilisha Yesu Kristo, Roho ana mwakilishi Roho Mtakatifu, Vilevile Neno ana mwakilishi
Mungu Baba, hata ubatizo tunao upata kama waamini yaani ubatizo wa maji mengi umesimama katika misingi mitatu; Mungu Baba, Mungu Mwana, Mungu Roho Mtakatifu.

- Mwongozo wa Mkristo katika maisha ya kumcha Mungu ni Neno, na hapa ndipo ninatakiwa niimarishe Imani yangu katika kina zaidi.

- Roho Mtakatifu yupo mimi kumtumia na hili kimaandiko liko dhahiri, ( Waebrania 1:14 )

- Neno nililo tamkiwa na Mtumishi wa Mungu ndani yake kuna Roho ya uumbaji kama nikiliamini kwa sehemu kubwa litayabadiisha maisha yangu, kwa sababu ndani ya hilo Neno ninalo tamkiwa kuna uvuvio wa nguvu za Mungu kupitia Roho Mtakatifu.

- Neno nililo tamkiwa na Mtumishi wa Mungu inatakiwa niliamini, nilihifadhi, pia niliingize kwenye vitendo ndipo litachanua na kuzaa baraka, na maneno haya yameelezwa wazi katika Yakobo 1:22-23.

- Ikiwa sina tabia ya kuliingiza Neno la Mungu nililo tamkiwa na Mtumishi wa Mungu katika vitendo, neno hilo haliwezi kunizalia matunda, kwa sababu linakosa ushirikiano wa Imani ya muusika na wote tunafahamu chanzo cha Imani ni kusikia.

- Imani ya mwamini inapata uwezo wa kutawala katika roho ikiwa mkristo analisikiliza Neno la Mungu kupitia masikio ya kiroho.

UFAFANUZI KWA UFUPI KUHUSU IMANI.

- tukisoma kwenye Waebrania 11:1 inaonyesha wazi kwamba Imani ni kuwa na uhakika wa mambo yatarajiwayo ni bayana ya mambo yasiyo onekana.

- Imani ni kutaria yasiyo weza kutarajiwa na hii haina tofauti na tafsiri ya kwanza.

- Imani ni nguvu, ni uweza.

- Inafahamika wazi kwamba kitu chenye nguvu kina msingi, vile vile kitu chenye uweza kina mamlaka, kwa hiyo hii inadhihirisha wazi Imani ni mamlaka ya Neno la Mungu.

- Ninapo soma Biblia na kuliamini Neno la Mungu ndipo ninapo pata mamlaka ya Imani itendayo kazi.

- ili niweze kupata mamlaka ya Imani itendayo kazi, na niweze kuimiliki idumu kwenye maisha yangu inatakiwa nifanye vitu vifuatavyo ; 
  i). Kuidhibiti nafsi.
  ii). Kujinyima vitu ambavyo ninaviona ni haki yangu
  iii). Kukubali kutembea na Roho muda wote.

- Nikiweza kusimama katika hii misingi mitatu, uwepo wa Mungu utakuwa mafuriko katika maisha yangu, na ndivyo inavyotakiwa iwe katika maisha ya mtu anaye mwamini Yesu Kristo.

- i). Maelezo kwa ufupi kuhusiana na kuidhibiti nafsi:-
Kuidhibiti nafsi  ni hali fulani ya kuilazimisha kuyatenda mapenzi ya Mungu, vile vile kuinyima uhuru katika vitu inavyo vipenda vilivyoko nje na mapenzi ya Mungu.

- Biblia imesisitiza katika suala zima la kuitunza nafsi, kwa sababu ndani ya nafsi kuna hali ya udhaifu mwingi sana, na nikitaka kuidhibitisha hili tutazame ndani ya nafsi kuna nini.
 1. Hisia 
 2. Akili
 3. Utashi 
- na wote tunafahamu madhara halisi ya hisia ya kwamba hisia huja hisia huondoka.

- Katika mfumo wa nafsi ulivyo kunahitajika kina cha ufahamu wa Neno la Mungu ili kuitawala na maneno haya yalisemwa dhahiri katika 1 Timotheo 4:16

- Uwezo wa kuitunza nafsi idumu katika mapenzi ya Mungu, kuna njia kuu mbili :-
 A). Kusoma Biblia katika Imani, na maneno haya yamedhibitishwa kupitia. Mithali 4:20
 B). Kulisikiliza Neno la Mungu vile vile kulifanya kuwa sehemu ya maisha yangu, na maneno haya pia yamedhibitishwa kuanzia Warumi 10:17.

- Nikiilazimisha nafsi yangu kusikiliza Neno la Mungu mara kwa mara maana yake ninaiambukiza tabia za KiMungu yaani inapata kuwa asili moja na Mungu, ndio maana hata kitabu cha Wakorinto hakikusita kusema maneno haya. 1 Wakorinto 6:17.

( ii ). Maelezo kwa ufupi kuhusiana na kujinyima vitu ambavyo ninaviona ni haki yangu

- Kwanza kabisa inatakiwa nifahamu vitu ambavyo ni haki yangu kuvipata katika hali ya kimwili
 1). Starehe ya mwili 
 2). Chakula ,
- Kwa hiyo nisipo kuwa na ufahamu wa kupambanua juu ya vitu hivi viwili, kwa maana zaidi Nitafahamu nyakati za kila jambo linatakiwa wakati upi, naweza kujikuta ninajitaabisha mwisho wa siku naukosa ufalme wa Mungu Ee Yesu nisaidie juu ya jambo hili.

- Nikitaka kutambua nyakati za kila jambo inatakiwa nijikite zaidi katika kina cha ufahamu wa Neno la Mungu.
- katika hili Yesu nisaidie, ikiwa mwenye haki ataokoka kwa shida na yule asiye mjua Mungu ataponea wapi?

iii). Maelezo kwa ufupi kuhusiana na (iii) inayo sema kukubali kutembea na Roho muda wote :-

- Mkristo mwenye uwezo wa kutembea na Roho ni yule aliyefanywa kiumbe kipya, kwa maana zaidi ni mkristo aliyevua vazi la kale na kuvalishwa  vazi jipya yaani aliyeokoka. 
2 Wakorinto 5:17

-Ikiwa mimi ni mkristo ninaye sema nina mwamini Yesu Kristo ikiwa sijatubu dhambi kwenye uso wa Mungu ninakuwa sitambulikani, ni sawa na mwanamume aliyevalishwa nguo za kike lakini ndani ni mwanamume.

- Roho wa Mungu anaishi katika maisha ya Mkristo anayeishi maisha ya ukweli, huyo ndiye mwenye uwezo wa kunong'onezwa na Roho siri za mbingu kwa sababu Roho huyajua yote hata mafumbo ya Mungu. (1 Wakorinto 2:10.)

- Methali ya BAB G POWER inasema hivi vya kimwili haviujengi ufalme wa Mungu bali vya kiroho ndivyo vinavyo ujenga ufalme wa Mungu, kwa hiyo lazima nijikite zaidi katika vitu vya kiroho.

- Methali ya pili ya BAB G POWER 
Mungu hakutwi na mapinduzi na ikiwa ni hivyo inatakiwa maisha yangu yote niyazamishe kwake kwa  asilimia Mia moja.

Ufafanuzi kwa ufupi kuhusiana na Roho :-

- Roho Mtakatifu ni nafsi ya tatu ya Uungu ambayo ipo katika umoja wa Utatu Mtakatifu, vilevile nafsi hii ndiyo ambayo imekabidhiwa jukumu la kuhudumia, kubariki, kuponya, kugawa vipawa mbali mbali kwa jamii ya wanao mwamini Yesu Kristo yaani waliookoka.

- Ili niweze kuyalingana maisha ya kutembea na Roho Mtakatifu, inatakiwa nifanye mambo yafuatayo :- 
 A). Niwe mnyenyekevu 
 B). Niwe mwaminifu
 C). Niwe mwombaji

Maelezo kwa ufupi kuhusiana na unyenyekevu (A) :-

- Unyenyekevu ni hali fulani ambayo inayavaa maisha ya mtu kulingana na jinsi ambavyo ufahamu wa mtu umekua katika kumjua Mungu. 

- Pointi ya juu inamaana kwamba unyenyekevu ni tendo analo litafuta mtu kwenye uso wa Mungu ili kuwa sehemu ya maisha yake, hii inamaana kwamba unyenyekevu si jambo la kuomba Mungu akupe bali ni tendo la kuweka bidii ili liwe sehemu ya maisha yangu.

- Ili maisha ya mkristo yaendane na hali ya unyenyekevu inatakiwa arudi chini ya muongozo  wa Neno la Mungu, kwa sababu katika Neno ndipo ilipo kweli yote, hata Yesu kuwaeleza wayahudi wadumu katika kweli, kama ilivyo andikwa katika Yohona 8:31-32, lengo lake lilikuwa ni kwamba waliyafahamu sana maandiko lakini hawakujua kweli iliyoko katika maandiko na wakakosa unyenyekevu na upeo wa kutambua kuwa  anayesema nao ndiye masihi.

- ( Kuabudu kwangu inatakiwa kuwe katika misingi ya rohoni, ndipo mapenzi ya Mungu yatatimia kwa wepesi katika maisha yangu ).

Maelezo kwa ufupi kuhusiana na uaminifu (B) :-

- Katika maisha ya mtu anaye mwamini Mungu uaminifu ni tendo ambalo humgusa Mungu sana kupitia maisha ya mtu, kwa sababu uaminifu ndio unao onyesha uhalisia wa mtu aliye Mbeba Mungu katika maisha mwake.

- Uaminifu ndio unao mfanya mtu kuwa halisi kwa Mungu, hii ipo wazi uaminifu wa Yesu Kristo ndio uliompa wepesi wa yeye kushinda majaribu.

TAHADHARI
Ninapo ingia kwenye maombi haitakiwi shetani awe na hati ya mashitaka  yangu atakayo nishitaki nayo kwenye uso wa Mungu ili azuie maombi yangu yasilete majibu bali inatakiwa niyalingane mapenzi ya Mungu kabla sijaingia kuomba ili yalete majibu kwenye uso wa Mungu.

- ( ishu si kutazama makosa niliyo yapitia bali kutazama mapenzi ya Mungu ni yapi na kusonga mbele hapo nitamfanya Mungu kuwa kweli sambamba na Neno lake linavyosema Zaburi103:12 )

- ( Mambo yote yatapita lakini Neno la Mungu lina ushindi, kwa hiyo lazima nijiimarishe katika misingi ya Neno hili ).

Maelezo kuhusiana na uombaji (C). :-

- Uombaji mara nyingi ni tendo ambalo huruhusu uvuvio wa nguvu ya Mungu katika maisha ya mtu, kwa maana zaidi mtu ambaye ni mwombaji ni rafiki wa Roho Mtakatifu.

- Mara nyingi Mungu hujifunua kwa waamini kupitia njia ya uombaji, lakini kinacho wagharimu waamini walio wengi ni kukosa upeo wa kupambanua kusikia sauti ya Mungu katika maisha yao, jambo hili liliwakuta Roda na wenzake katika nyakati zile wakati Petro yuko gerezani. Matendo ya mitume 12:5-17

- Jambo la kuwa nalo makini nijitahidi sana niwe na uwezo wa kupambanua sauti ya Roho Mtakatifu anaposema na mimi nyakati za maombi au kuomba.

- Nikimwomba Mungu katika hali ya upofu wa kiroho ni vigumu kupambanua nyakati za kujibiwa, ndio maana maisha ya jamii ya waaminio imekumbwa sana na laana ya malalamiko, yaani watu wananungunika kuliko kumwamini Mungu.






Hakuna maoni: