SOMO LA LEO
9/8/2015
SAFISHA MOYO ILI BARAKA ZA MUNGU ZIPATE MPENYO
Moyo ndio njia kuu ambayo Mungu anaitumia kuzungumza na
mtu,ndio maana Maandiko Matakatifu yanatusisitiza sisi ambao ni waamini
kuilinda mioyo yetu ,hii ni kwasababu moyo wa mwamini ukijeruhika moja kwa moja hupoteza mawasiliano na Mungu.
(Hekima na busara zinatokana na moyo wa mwamini kuwa safi na
wazi machoni pa Mungu.)
Moyo wa mwamini ukiwa ukiwa safi hupata Neema machoni pa Mungu yaani kuisikia sauti
yake waziwazi ndio maana Biblia ikasema katika kitabu cha Mithali 4:23.
Moyo wa mtu anayemwamini Mungu unaweza ukwalindwa kwa njia
zifuatazo:-
I) Kuusikilizisha moyo wake Neno la Mungu , na hili jambo
linatakiwa liwe ni tendo endelevu.
II )Kuhakikisha unasikiliza mafundisho yenye mafunuo ya Roho
Mtakatifu, mafundisho haya huwa hayapingani na Biblia yaani kilichoandikwa ndani ya Biblia.
ANGALIZO 1:Kama sisomi Biblia maisha yangu yanakuwa hatiani
muda wowote, kwasababu sitakuwa na ufahamu wa kupambanua hata kama
ninadanganywa mimki nitakubali tu na ndipo kifo
cha watu wengi kinapo anzia.
(Moyo wangu usipo safishwa kwa Neno la Mungu ni vigumu
kukubaliana na kile ambacho Mungu anasema kwa maana Zaidi ,kwa sehemu
utakubaliana na sehemu utakuwa na mashaka
na Biblia imesema wazi juu ya hili Warumi 14:23.)
(Moyo ukikosa utulivu tayari ni ugonjwa ‘Eee Yesu niepushe
na hili janga)’.
ANGALIZO 2:Ninapo ingiza shaka katika Neno la Kinabii
ninalotamkiwa na Mtumishi wa Mungu maana yake ninaharibu mfumo mzima wa Baraka
zangu kwenye uwepo wa Mungu.
NINI KIFANYIKE NIWEZE KUUTUNZA MOYO WANGU?
Kwanza kabisa kabla ya kupata mbinu ya kutunza moyo wangu
inatakiwa nifahamu tabia za moyo wangu kupitia Biblia.
Tabia za moyo wa mtu zinaelezwa kama ifuatavyo katika kitabu
cha Yeremia 17:9.
Udanganyifu ulioko ndani ya moyo wangu ni vigumu kudhibiti
ikiwa sina kina cha maarifa ya Neno la Mungu.
(Nikilipokea Neno la Mungu katika hali ya Roho Mtakatifu
hisia haitakuwa na uwezo wa kuathiri moyo wangu, ndio maana ninahitajika
kulisikiliza Neno la Mungu kupoitia masikio ya kiroho, masikio ya kiroho
humsaidia mwamini kupoata mabadiliko
kupitia kile anachokisikiliza 9Neno la Mungu).
Moyo uluiofunguliwa na ambao unahitajika awe nao mwamini
anayemwamini Yesu Kristo ni kama ifuatavyo kupitia Maandiko Matakatifu
Wagalatia 5:22-26.
Moyo uliofunguliwa ndani yake kuna kitu kinachoitwa Roho ya
Munguna hiyo ndio inayohitajika kwa kila mtu amwaminie Mungu.
Moyo uliofunguliwa kwa Neno la Mungu ndani yake kuna mambo
yafuatayo:-
i)Roho ya Upendo
ii)Roho ya Furahas
iii)Roho ya Amani
iv)Roho ya Uvumilivu.
v)Roho ya Utu wema
vi)Roho ya Fadhili
vii)Roho ya uaminifu
viii)Roho ya Upole kiasi
Roho iliyofunguliwa ina uwezo wa kubeba madhaifu ya
kila namna, nah ii ndio ilikuwa tabia ya
YESU KRISTO
Ikiwa mimi ni mwamini na hapohapo bado roho yangu
haijafunguliwa ni vigumu kuyatimiza mapenzi ya Mungu , na hili ni jambo
limeaathiri kanisa la leo.
WAKRISTO WA LEO WAMEATHIRIKA ZAIDI KIIMANI NDIO MAANA
WANASHINDWA KUZITAMBUA SIRI ZA MUNGU
Kuna siri ambayo
kanisa la leo halijagundua ndio maana jamiikubwa
ya wakristo hawana mpenyo katika maisha yao ingawa wanaomba na kuombewa.
Mambo yote ninayoyahitaji ya kimwili yawe ya ziada lakini
roho yangu inatakiwa iwe safimuda wote machoni pa Mungu, kwasababu muujiza wa
kwanza katika maisha ya mtu ni kuwa na uhakika kwamba jina lakelipo katika
kumbukumbuya vitabu vya uzima wa milele.
Tunaporudi katika suala la Baraka hapo inategemea kiwango
cha akaunti yangu jinsi inavyosoma kulingana na jinsi ninavyowekeza kwenye
uwepo wa Mungu.
(Kama uchumi wangu hakuna mkono wa Mungu ndani ya hayo ni
mafanikio ya muda mfupi muda wowote yanaweza kufilisika ).
(Tabia haiponyeki
ukiwqa nje na uwepo wa Mungu bali
tabia inaponyeka ukiwa mbali na uwepo wa
Mungu ).
Katika suala hili nahitaji umakini hapas nitaepuka mambo yaliyo mengi.
Ninapoingia kwenye uso wa Mungu kuomba labda jambo Fulani
inatakiwa nihakikishe , kwasababu majibu ya mtuyanakuja.
MAELEZO KWA UFUPI
KUHUSU SUALA LA UCHUMI
Ukweli ni kwamba sualka la uchumi ni jambo ambalo halihitaji maombezi kwa kuombea bali ni jambo
linalohitaji kudumu katika kanuni ya
utoaji kama Maandiko yanavyosema Malaki 3:8-10, Luka12:34. Luka 16:10 Matendo
ya Mitume10:1-5 ,Matendo ya Mitume10:9:36-40 NA 2Wakorintho 9:6-8
Utoaji wangu inatakiwa autambue Mungu asiutambue mwanadamu
ndipo utakuwa na Baraka.
Utoaji nisehemu inayoufanya moyo wa Mungu kuwa na furaha na
mtu.
Utoaji una nguvu ya kutiisha mauti.
Ninaposimama kwenye uso wa Mungu kuomba kuhusiana na suala la uchumi Mungu
anatazama kiwango ninachokihitaji kwenye
uso wake Je! Kinaendana na utoaji wangu?
Ninaposimama kusapoti
kazi ya Mungu maana yake ninaweka muunganiko na Mungu katika roho yaani kibiblia
ninaitwa mtu ambaye ninamkopesha
Mungu na jambo hili hata Biblia
imesema katika Miithali 19:17.
Ninapotoa pesa yangu kusapoti jambo lolote ndani ya
kanisa linalohusiana na faida za Mungu
,Kibiblia ninaitwa mtu ambaye ninamkopesha Mungu sehemu ya mali yangu na
inafahamika wazi vyote nilivyo navyo na vinavyofanya watu waniheshimu na
kuniogopa vinatokana na Mungu Je! Nikitoa
sehemu yangu kumpa Bwana ni faida gani nitakayoipata? Katika hili inatakiwa
nilijibu swali hili mwenyewe.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni