- Wakristo wengi wametubu dhambi,na inafahamika wazi mtu ambaye ametubu dhambi ameokoka,lakini cha ajabu wakristo hao hao wanaishi maisha ya dhambi.
- katika hali ya kawaida dhambi ni mfano wa vitu hivi :
i.) Uongo ii.) Tamaa iii.) Uzinzi iv.) Masengenyo v.) Wivu vi.) Hasira n.k , lakini kibibilia dhambi ni majumuisho ya kila aina ya uovu, ndio maana Bibilia ikafunua zaidi kwa kina kwamba dhambi ni ibada ya sanamu. (Wakolosai 3:5)

- Hii ipo wazi changamoto ninayo ipitia katika jambo lolote nililo na uhitaji nalo inatokana na makosa niliyo yafanya awali yaani kipindi kilicho pita na ambayo bado ninaendelea kuyafanya ingawa nilisha tubu dhambi.
- ( Mungu ni kweli siku zote wala haleti maumivu kwa anae mpenda, bali maumivu hutokana na tamaa iliyoko ndani ya mtu mwenyewe, mambo haya yamedhibitishwa kwenye Biblia. (Yohana 10:10-11)
- Kwa nini inatakiwa mimi ninae mwamini Mungu niikimbie dhambi?, hii ni kwa sababu ili niweze kuzilingana baraka za Mungu inatakiwa niishi maisha matakatifu kama yeye alivyo Mtakatifu. Na maandiko yamefunua kwa kina zaidi katika (1Petro 1: 13-16 )
- ( baraka za Mungu lazima nizilingane ndipo ziwe sehemu ya maisha yangu, katika hili kunahitajika kuikana nafsi ).
- ( Hakuna jambo linalo kuja kwa bahati mbaya katika maisha ya mtu bali kila jambo lina makusudi maalumu)
- Katika hili inategemea makusudi haya yanatokana na Mungu, kama yanatokana na Mungu basi ndani yake kuna baraka na kuinuliwa mbele ya watesi wangu, ndio maana katika (Zaburi 35:1,2) imeainisha wazi.
- Na kama makusudi haya yanatokana na shetani, basi kazi yake ni kunidhalilisha na kunitia aibu, ndio maana inatakiwa niwe na mahusiano ya karibu na Neno la Mungu ili niwe na upeo wa kupambanua alama za nyakati.
- ( Mithali 6:32-33 )
- Mwamini akiamua kuishi maisha ya utakatifu ni kitu kinachowezekana kwa sababu ni jambo ambalo lipo ndani ya uwezo wake kwa asilimia 75 kama ataamua. ( 1Petro 1:13-16)
- Suala la mimi kuwa Mtakatifu ni jambo linalo wezekana iwapo nitaamua maisha yangu yote nitayazamisha ndani ya Neno la Mungu, kwa sababu Neno la Mungu lina ufahamu zaidi wa kiroho kwa hiyo ni rahisi likayatambua mawazo na hila za mwovu kabla maisha yake hayajaathiriwa.
- Kuna mambo 3 katika Kanisa la leo yamekuwa kronoki, na mambo haya yamepoteza nguvu za Kanisa " Yesu tusaidie sisi na kanisa letu kuanzia leo tufanye mabadiliko"
A) Uzinzi (Mithali 6:32-33).
B). Rushwa ( kumbukumbu 16:19-20).
C). Uongo. ( 1Petro 3:10 )
Hizi ni aina tatu za dhambi ambazo zimelikalia kanisa la leo.
A) Uzinzi (Mithali 6:32-33).
B). Rushwa ( kumbukumbu 16:19-20).
C). Uongo. ( 1Petro 3:10 )
Hizi ni aina tatu za dhambi ambazo zimelikalia kanisa la leo.
UFAFANUZI KWA UFUPI KUHUSU DHAMBI YA UZINZI.
- Uzinzi ni dhambi inayo tendeka kwa jinsia mbili tofauti, yaani jinsia ya kike na jinsia ya kiume, na jinsia hizi mbili zinakuwa haziko katika ndoa.
- Uzinzi ni dhambi inayo tendeka kwa jinsia mbili tofauti, yaani jinsia ya kike na jinsia ya kiume, na jinsia hizi mbili zinakuwa haziko katika ndoa.
- Uzinzi ni dhambi anayoifanya mtu akiwa hajapagawa pepo hii inamaanisha kwamba ni tendo analolitenda mtu akiwa na akili zake timamu, ndio maana jambo hili hufanywa kwa kificho sana lakini jicho la Mungu linaona " Ee Yesu tuhurumie"
-Mwanadamu unaweza kumficha lakini Roho wa Mungu anayatambua mawazo ya moyo, hii inaelekea nisipo fanya mabadiliko mapema nyakati za kudhalilika zinakuja kwa sababu ya kilicho andikwa katika ( 1 Wakorinto 2:10 )
- Dhambi ya uzinzi inaondoa heshima aliyo nayo mtu kwenye uso wa Mungu, ndio maana jamii kubwa ya watu wana pigwa na magonjwa yasiyo kuwa na tiba, na chanzo cha yote ni uzinzi, uasherati, zinaa na n.k, na vyote hivi vinatokana na mfumo mzima wa tamaa.
- Ni vigumu kuishinda dhambi ya uzinzi ikiwa roho ya mtu haijafunguliwa kwa sababu kama roho ya mtu haijafunguliwa haiwezi kuyatambua mapenzi ya Mungu ni yapi katika maisha yake.
- Ili niweze kufahamu roho ya mtu iliyofunguliwa ni kutokana na mambo haya:
i). Bidii aliyo nayo ya kujifunza Neno la Mungu ( Biblia )
ii). Uaminifu anao uonyesha katika kutendea kazi Neno analo fundishwa vilevile analolisoma katika Biblia, ndio maana Mungu kupitia kitabu cha ( Ufunuo wa Yohana 2:10 ) akasema.

- Ili niweze kubadilika katika ile tabia ambayo imekuwa ni shida kwangu kuiacha inatakiwa nitumie mbinu za ziada je mbinu za ziada ni zipi?
i). Ni kutafuta mtu wa Mungu mwenye kina kirefu na mahusiano ya karibu na Mungu ili akufungue ( akufanyie deliverance ), hata Biblia imetuelekeza ijapokuwa mioyo yetu ni migumu na mizito kuelewa (2timotheo 1:6).

- Katika jambo hili la kwenda kufunguliwa ni jambo ambalo linahitaji ufunge macho ukubali kudhalilika ili upone, ndio maana ukisoma katika mstari wa saba
- Tendo la kuamua kujiweka wazi machoni pa Mtumishi wa Mungu ili nisaidike linadhihirisha moyo wangu namna ambavyo umechoka dhambi.
- Nikiona moyo wangu unachukia (unakasirika) wakati wa kuonywa hiyo ni picha wazi ya kwamba ingawa nina kwenda Kanisani lakini bado sina hamu ya kubadilika.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni