Jumapili, 2 Agosti 2015

JIIMARISHE KATIKA ROHO



SOMO LA LEO
2/8/2015
JIIMARISHE KATIKA ROHO
Inatakiwa nijiimarishe katika roho kwasababu adui ninayepambana naye yupo katika roho,ndio maana kushindwa kwa mkristo  kunaanzia katika roho na ukiona hali  hiyo imedhihirika kimwili jua wazi mtu huyo  kiroho amekufa kabisa (anakabiliwa na kifo cha kiroho).


Katika maisha ya kiroho ufahamu ni suala la msingi sana.

Kujiimarisha kiroho kwa tafsiri nyingine  ni kujiimarisha kiimani , na hii ni kwasababu Imani ni kitu kamili cha rohoni.

Mfumo wa mawazo ukisha tetereka kwa mwamini mwelekeo wa Imani unapotea, na hapo ndiyo unakuwa  mwanzo wa mwamini  kuwaza vibaya , linda mfumo wa mawazo yako utakuwa umeitunza Imani .

Nikiruhusu hali ya kuwaza vibaya nitakuwa nimeathiri mfumo wa Imani ,kwahiyo nitaamini kinyume pia  ndiyo maana Biblia ikasema wazi katika Nuhumu 1:9.

Mawazo ni aina Fulani ya mipango inayotengenezwa ndani ya moyo wa mtu, ndiyo maana kile ambacho mtu anakinena  ndani ya kinywa chake  amekidhamiria kabisa.

Ni vigummu kuyatambua mawazo ya mtu anayoniwazia  akiwa hajafungua kinywa kunena au kuongea, ndivyo ilivyo ni vigumu kuyatambua mawazo ya Mungu anayokuwazia ikiwa sio msomaji wa Biblia wala msikilizaji wa Neno la Mungu.

Kushindwa kwangu kwingi kunatokana na kutokutambua mawazo ya Mungu anayoniwazia , ndiyo maana naweza kujikuta nimejikwaa  kwenye uwepo wake na kupoteza mtiririko wa Baraka zangu.

Ninaharibikiwa  kwasababu bado sijatambua mapenzi ya Mungu  ni yapi katika maisha yangu, ndiyo maana nahitajika kujiimarisha kiufahamu.
(Ufahamu wangu ukikua kuhusu Mungu nimeyaponya maisha yangu ya kiroho  na hili jambo walikutana nalo Meshaki , Shedraki na Abednego
Danieli 3:1-30

SWALI
Katika Danieli 3:15 ndani ya huo mstari kuna  maneno gani
JIBU:
Kuna maneno ya kushawishi

Mwamini aliyefunikwa na uwepo wa Mungu mahali popote anapokanyaga anakuwa tayari amepatawala katika roho , kwahiyo hali hii humsaidia mwamini kugeuza mawazo ya  adui yake kwenda sambamba na jambo analolikusudia  yeye, nah ii lilithibitika dhahiri mwisho wa safari ya Meshaki Shedraki na Abednego mawazo ya adui yao ambaye ni Mfalme Nebkadreza yalibadilishwa yakaendana sambamba na mawazo ya Watumishi wa Mungu  kama inavyosema  katika  msatari wa 29-30.

(Sababu itakayomfanya adui  yangu kugeuza ufahamu wake na kukaa chini  ya miguu yangu ni mimi kujiomheza kiufahamu Zaidi wa Neno la Mungu).

Katika Danieli 3:16, 17 unadhihirisha wazi maneno ya kiufahamu , maneno ya kiimani , maneno ya hekima maneno ya uaminifu kwa wanae mtumaiania , mtu wa aina hii hawezi kushindwa na changamoto yoyote atakuwa mshindi tu.

Hakuna maoni: