Jumatatu, 20 Julai 2015

KUBALIANA NA WAKATI ULIOKUSUDIWA

19/7/2015

KUBALIANA  NA WAKATI WA BWANA ULIOKUSUDIWA

Tatizo kubwa linalotugharimu sisi waamini bado hatuna maarifa ya kutambua ni nyakati zipi ambazo Mungu amekusudia kufany jambo Fulani katika maisha yangu , ndiyo maa na wengi hujikuta tumeshadumbukia katika matatizo na hapo hapo hatuna uwezo wa kujitoa pale.



(Mwamini bila maarifa ni sawa na gari linalotembea gizani haliwaki taa Je! Matokeo yake ni nini?)

Ikiwa mimi ni mwamini ninayemwamini Mungu inatakiwa niipalilie imani yangu mpaka iyatambue makusudi ya Mungu ni yapi katika maisha yangu.

(Imani ndiyo mwanga wa maisha ya mkristo ndiyo maana inatakiwa niweke bidii katika kujiendeleza zaidi kwenye Neno la Mungu)

Mkristo mwenye uwezo wa kuyatambua makusidi ya Mungu katika maisha yake ni Yule ambaye Mungu amemkusudia Baraka zake za kiroho na kimwili.

Kuna gharama sana ya kupata muujiza ambao tayari nimeupoteza kwenye uso wa Mungu ,ndiyo maana nahitaji niwe na umakini wa hali ya juu sana ,Hata Biblia imetoa tahadhari kuhusiana na pointi hii Ufunuo 2:25.

Ili niweze kuwa mkristo salama au safi inatakiwa niyazingatie kwa umakini maneno ya Mungu, kwasababu ndiyo yanayothibitisha makusudi ya Mungu katika maisha ya mtu.

Ili makusudi ya Mungu yaweze kutimia katika maisha yangu inatakiwa nifanye mambo yafuatayo:-
I) Nijiongeze katika ufahamu wa rohoni yaani wa Neno la Mungu ,ndiyo maana hata Maandiko Matakatifu yakasema Mithali 4:1-6.

Nikitaka kufanikiwa inatakiwa niwe makini kufuataisha mwongozo wa Mtumishi wa Mungu anaonielekeza .

Nikitaka kufanikiwa inatakiwa niwe makini kusikiliza mausia ya Mungu anaonielekeza kupitia Neno la Mungu Isaya 41:8-10.

Ili makusudi ya Mungu yawe hai kwenye maisha yangu inatakiwa niamini kila neno lililoandikwa kwenye Maandiko Matakatifu kwamba li hai kwenye maisha yangu .

Wakristo wengi wanapoteza miujiza yao kwasababu mioyo yao hukiuka miongozo  au hutilia shaka miongozo wanayopewana Watumishi wa Mungu lakini ukweli ni kwamba Biblia imezungumza wazi kabisa kuhusu mtu anayetilia shaka maneno ya Mungu kama ilivyoandikwa Warumi 14:23. Na Yakobo1:8

(Siku nitatambua makusudi ya Mungu ndiyo mwanzo wa mafanikio yangu).

(Mungu huthibitika dhahiri kwa mwamini mwenye msimamo katika imani )
*Mwisho wa ufafanuzi wa namba moja ya kirumi (I)

II) Nitoe muda wa kujifunza Biblia ;Biblia ni maneno ya Mungu yenye uvuvio wa uzima ndani yake , ndiyo maana ndani ya Biblia kuna imani ya kuyatiisha kila mamlaka ya mbinguni ,duniani , nakuzimu.

Mwamini anayetoa muda wa kujifunza Biblia roho yake itapata Neema ya kushirikishwa siri za Mungu , vilevile atapata Neema ya mwili wake kuponywa chini ya mamlaka yaNeno la Mungu.

(Maneno ya Mungu ndiyo yanayothibitisha uponyaji halisi katika maisha ya mtu ndiyo maana Mtumishi wetu hatujawahi kumuona akiwapa wagonjwa dawa hutamka neno na kuponywa).

Maneno ya Mungu ndiyo yatakayonipa ufahamu wa kutambua makusudi ya Mungu ni yapi ,ndiyo maana Biblia ikazungumza katika kitabu cha Isaya 60:1-22

Isaya60 :1-22 ndiyo makusudi ya Mungu katika maisha yangu ndani yaJumapili ya leoTarehe 19 Mwezi 7 mwaka 2015, na neno hili litakumbukwa siku mafanikio yangu yatakapotimia.

SWALI :Je! Ni njia gani inayoweza kutumika ikatimia kwamtu?
JIBU :Nikuamini kila neno lililoandikwa kwenye Maandiko Matakatifu kwamba ni hai kwenye maisha yanguWaebrania 4:12

SWALI:Ni njia gani inayosababisha madhihirisho ya Roho Mtakatifu katika maisha ya mtu?
JIBU: Ni ile hali ya muunganiko wa Neno la Mungu na imani ya mwamini.

Hakuna maoni: