Jumapili, 14 Juni 2015

TAWALA NAFSI YAKO

TAWALA NAFSI YAKO.

- Wakristo walio wengi wanafanya ibada za sanamu hata kama wameokoka, mara nyingi jambo hili husababishwa na kushindwa kuitawala nafsi. 


- Kushindwa kuidhibiti nafsi mara nyingi ndo chanzo cha kufanya ibada ya sanamu inapo anzia.
- Je nini maana ya ibada ya sanamu?
Wakolosai 3:5-6
- ( Uwepo wa Mungu na ibada ya sanamu ni vitu viwili tofauti yaani haviendani kabisaaa, kwa hiyo ili niweze kufanya ibada iliyo kamili kwenye uso wa Mungu, inatakiwa kwanza niitawale nafsi  yangu). 

- Mkristo asiyekuwa na uwezo wa kuitawala nafsi  yake, maisha yake ya kiroho hayawezi kuinuka bali yatadumaa. 

- Utakatifu katika maisha ya mwamini unaanzia pale ambapo anaanza kudhibiti nafsi yake, 

- Ibada  ya sanamu ndo kikwazo kikuu kinacho  yafanya maisha ya wakristo yadumae yaani yasinawiri. 

- Uponyaji wangu baraka zangu mara nyingi vinazuiliwa visidhibitike kwangu na hii inasababishwa na ibada ya sanamu ninayo ifanya, na ibada hii chanzo chake ni mimi ninavyo shindwa kuitawala nafsi yangu. 

- Nafsi katika umbo la kiroho ndio inayotoa muonekano wa mtu halisi na point hii inadhibitishwa na Luka 16: 19-31. Ndio maana lazaro na tajiri walifahamiana huko kwenye hukumu ya Mungu. 

- Ili niweze kuitawala nafsi ninahitaji niwe na ufahamu wa ndani wa kiroho ( Neno la Mungu ), kwa sababu nafsi imebeba mambo yafuatayo : 
i). Hisia 
ii). Akili 
iii). Utashi
-  Hivi vitu vitatu bila kina cha mafundisho huwezi vitawala yaani havitawaliki kirahisi, ndio maana wasomi wengi waliojiendeleza kiakili wanapinga kuhusu Mungu.

- Nisipo mwamini kiongozi wangu wa kiroho yaani mtumishi wangu,  hata Mungu angeniletea malaika kutoka mbinguni pia nisingemwamini zaidi ya hapo ningemkemea kama  pepo.



Hakuna maoni: