Jumapili, 7 Juni 2015

KIMBILIO NI YESU KRISTO PEKEE


KIMBILIO NI YESU KRISTO PEKEE
Hakuna kimbilio lingine pengine  popote nje na jina la Yesu Kristo.

Jamii kubwa ya waamini wanaokata tama wengi wao bado hawajafahamu 
ukweli kuhusu Maandiko Matakatifu.

Jina la Yesu Kristo liko tayari kumbeba mtu au kuficha aibu ya mtu ambaye moyo wake  ameufungua katika Neno la Mungu.

(Nikifundishwa Neno la Mungu vizuri nikaimarika kiufahamu siwezi kuwa limbukeni wa nyakati zozote ninazokutana nazo).

Kama kimbilio ni Yesu Kristo pekee inatakiwa nijiongeze kiufahamu ili niweze kuendana sambamba na Baraka zitokanazo na waliaminio jina hili, hapo nitakuwa nimeyarahisishia maisha  yangu hali ya wepesi katika kila hatua ya jambo  ninalolikusudia.
Wafilipi 2:1-10

Ili niweze kulilingana jina la Yesu Kristo na kila niliitapo linipe faida inatakiwa nifanye mambo yafuatayo kwenye maisha yangu:-
I)Upole wa roho, na upole wa roho huzaa hali ya uvumilivu katika maisha ya mtu
II) Haitakiwi majivuno katika maisha ya mcha Mungu
III) Hali ya unyenyekevu
IV) Upendo

(Mtihani wowote unaohusiana na mambo  ya kiroho nitaweza kuushinda kama nitakubali kukaaa chini ya mafunuo ya Roho Mtakatifu, kwasababu Roho Mtakatifu yuko maalumu kufunua siri yoyote au kutupasha habari katika yale  tunayokusudiwa siku zijazo haijalishi ni mazuri au mabaya , Biblia imethibitisha  neno hili katika kitabu cha 1Wakoritho 2:10).

Kinachofanya jina la Yesu Kristo lionekane linatenda mambo makubwa katika maisha ya mtu ni ile hali aliyonayo mtu ya mahusiano mazuri na Roho Mtakatifu kupitia Neno la Mungu .

Mahusianao mazuri na Roho Mtakatifu  ndiyo yanayolifanya jina Yesu Kristo  liwe hai na kuthibitisha  miujuza uponyaji na mambo mengine mengi , ndiyo maana huyu anaweza akalitumia jina la Yesu Kristo likaponya wagonjwa na watu wakafunguliwa , wakaponywa na mwingine anaweza  akalitumia jina la Yesu Kristo  lisitokee chochote. Je!hapo shida inakuwa ni nini?,
Shida inayosababisha mtu ashindwe kulitumia jina la Yesu Kristokufanya ishara mara nyingi inatokana na ufahamu mdogo anaokuwa nao katika kulijua Neno la Mungu.

Neema ya Mungu imetolewa bure kwa kila aaminiye , Hata neno hili Maandiko Matakatifu  yamelithibitisha katika kitabu cha Marko 16:15-18.

ANGALIZO 1:Ninapoukimbia uso wa Mungu yaani nikaacha kwenda kanisani kwa kuvunjika moyo  au kukata tama, shetani atayageuza maisha yangu jalala la matatizo ,ndiyo maana wakristo wengi leo hii wanahaha hawana pa kuelekea.

Kinachowafanya wakristo (waamini) wakate tama ya kumtafuta Mungu zaidi ni mambo haya yafuatayo:-
I)                   Wengi wao wamejeruhiwa na viongozi wao wa kiroho yaani wachungaji wao, Kivipi?
A)Kuzini nao
B)Kuwabebesha mimba
C)Kuvunja ndoa zao na maengine mengi

II)     Wengine wametapeliwa na viongozi wa kiroho na kufilisiwa mali zao , Kivipi?
A)   Bwana anasema umtolee sadaka Fulani.
B)    Nikopeshe kadhaa nitarejesha lakini ndio kwaheri yaani hiyo hairudi tena ,
Mambo kama hayaau mkristo aliyekutana na mambo kama haya yakamkuta kwenye maisha yake asipopata mshauri wa kiroho  mwenye ufahamu wa ndani wa Kimungu maisha yake hayawezi kurudi kawaida bali ataishi katika mazingira haya:-
A)   Kutokusamehe
B)    Visasi
C)    Chuki
D)   Lawama
E)    Manung’uniko
Je! Ikiwa ni kiongozi wa kiroho  umesababisha mambo kama haya kwa mwamini wako ambaye  unamhudumia kiroho, Damu ya mtu huyo itadaiwa mikononi mwa nani?
Jibu mwenyewe msomaji


(Nikiruhusu kukaa chini ya mwongozo wa Roho Mtakatifuhakuna mahali popote nitakapo tetereka,, nikitetereka  Roho atanirejesha kwa sauti ya upole na upendo).

Hakuna maoni: