NYENYEKEA CHINI YA UWEPO WA MUNGU
- Ili maisha ya mwamini yaweze kumvutia baraka kutoka kwenye uso wa Mungu, anahitaji hali ya unyenyekevu katika moyo wake kwa sababu hali ya unyenyekevu ndiyo inayo tengeneza mazingira ya mtu kubarikiwa
au kufanikiwa au kufunguliwa kwenye uwepo wa Mungu, kwa maana zaidi unyenyekevu ni tendo linalo andaa mazingira ya mwamini kupokea kitu chochote anachokitaka kutoka kwenye uso wa Mungu.
- (Unyenyekevu ni hali ambayo inatafutwa na mtu binafsi na katika hili kunahitajika mbinu ya ziada.)
- Unyenyekevu ni jambo ambalo lisiloonekana la maana katika macho ya watu wengi lakini unyenyekevu ni hali inayo mpa mwamini heshima kwenye uso wa Mungu.
- Jinsi ninavyo kuwa mnyenyekevu katika kuutafuta uso wa Mungu, ndivyo uwepo wa Mungu utakavyo zidi kujidhihirisha katika maisha yangu, mara nyingi jambo hili limekuwa likileta shida hata kwa viongozi wa kiroho, ndio maana utamkuta kiongozi wa kiroho anapinga nguvu anayotumika nayo mwenzake,
Hapa shida ni nini?
a ). Waamini wengi hawana hali za unyenyekevu katika mioyo yao na hili ndio jambo linalo mzuia Roho Mtakatifu kujidhihirisha.
- Ili niweze kumfahamu kiongozi wa kiroho yaani Mchungaji ambaye maarifa ya Mungu yametoweka ndani mwake;-
( i ) ni pale ambapo ataacha kutangaza ujumbe wa Bwana katikati ya kundi ambalo ni wahitaji, ataanza kuongea hadithi na kuwapinga wachungaji wengine, kwaa hiyo nikimsikia mtu wa aina hii tayari nijue maarifa ya Kimungu yameisha toweka ndani mwake.
- Ili niweze kusimama katika hali ya unyenyekevu nahitajika nitendee kazi mambo yafuatayo :-
i ). Inatakiwa niwe mtu wa kupenda kusikiliza Neno la Mungu mara kwa mara hata wakati mwingine kupitia media, hiyo inatengeneza mfumo wa utulivu katika moyo wa mtu anaye mtafuta Mungu.
- Jambo ninalolipa kipa umbele katika maisha yangu aidha katika kulitazama au katika kulisikia ndilo linalotengeneza mfumo wa utawala katika moyo wangu.
- Inatakiwa nijiwekee mfumo wa ninacho kitazama na ninacho kisikiliza kiwe sambamba na mapenzi ya Mungu, hapo nitakuwa nimeuandaa moyo wangu katika hali ya unyenyekevu, na ndio njia ya kuzilingana baraka za Mungu
hata kitabu cha Mithali kimezungumza, Mithali 12:1
- Mafundisho ya Neno la Mungu ni nidhamu ya Roho Mtakatifu kwa waaminio, ndio maana Biblia inatusisitiza sana tudumu katika mafundisho ya Neno la Mungu, kwa sababu ndipo tunapopatia nidhamu ya kumheshimu Mungu vile vile itakayo tusaidia kubebeana udhaifu sisi kwa sisi.
- ( kizazi cha leo ukitaka kukiponya kinahitaji ukweli na uwazi na sio mafumbo )
ii ). Inatakiwa niwe mtu wa kupenda kujisomea Biblia vile vile vitabu vilivyo andikwa na watumishi wa Mungu.
- Kupenda kujisomea Biblia itanisaidia mimi kama mwamini kuupa moyo wangu muunganiko na uwepo wa Mungu, ndani ya hili nitapata faida kuu zifuatazo:-
( a ). Roho ya kusamehe ( b ). Roho ya uvumilivu ( c ). Roho ya upendo ( d ). Roho ya kuendelea kumcha Bwana, mkristo mwamini akisha kuwa na vitu vinne tajwa hapo juu ni rahisi kwenye uso wa Mungu akaitwa mtakatifu.
iii). Inatakiwa niwe mtu wa kupenda kusikiliza Neno la Mungu, au mafundisho ya Neno la Mungu yatokayo kwa kiongozi wangu wa kiroho, mara nyingi hii itanisaidia kuniimarisha katika msingi wa kumcha Bwana katika kina cha Imani.
MBINU YA KUPATA HALI YA UNYENYEKEVU.
- Mbinu halisi itakayo nisaidia mimi kama mkristo ninayemwamini Yesu Kristo ili nipate hali ya unyenyekevu :
( i ). Kufunga ( ii ). Kuomba, hata maandiko yamedhibitisha maneno haya:- 2Nyakati 7:14-16, Ezra 8:21-23
- ( kama sina hali ya unyenyekevu ndani mwangu ni vigumu kuyalingana mapenzi ya Mungu)
- Baraka za Kimwili zitakuwa dhahiri katika maisha ya mtu pale ambapo mahusiano ya mtu huyo na Mungu yatakapo imarika, lakini jambo hili huwa mara nyingi linahitaji uvumilivu sana mpaka baraka za Mungu ziwe dhahiri.
ANGALIZO NO.1
Inapotokea bahati mbaya nimekosea kwenye uso wa Mungu mimi kama mwamini haitakiwi nikimbilie kujihukumu bali inatakiwa nikimbilie toba ili inirejeshe kwenye uwepo wa Mungu.
- Dhambi anayo ifanya mwamini kwa makusudi yaani ikawa ina mwendelezo kila siku katika jambo hilo hilo , hiyo inaweza kuleta madhara yafuatayo maisha yake:-
( 1 ). Kufa kiroho ( 2 ). Kupoteza hali ya kuisikia sauti ya Roho Mtakatifu, na hii ndio imegharimu maisha ya watu wengi na kuyaweka katika matatizo, eeh Yesu nisaidie.
( 3 ). Kupoteza mtiririko wa kuomba na hii mara nyingi inawaumiza watu wengi, wakristo walio wengi waliopoteza mtiririko wa kuomba kwa sehemu kubwa dhambi ndio inayo changia kwa sababu dhambi ikiisha ingia katika moyo wa mtu huwa inavuruga utulivu ndani ya moyo wake na hapo ndipo utayari wa mtu kwa Mungu unapo haribikia.
- ( Dhambi ikiisha uvaa moyo wangu haiwezi ikanipa nafasi ya kumcha Mungu katika roho na kweli mpaka pale nitakapo itubu dhambi ile, vile vile nikaruhusu moyo wangu kukubaliana na maandiko matakatifu kama yanavyo sema katika Zaburi 103:12 )
-Tatizo linalo wakumba wakristo jamii ya waaminio pale wanapotubu kuhusu dhambi bado mioyo yao inakuwa haiamini kwamba kweli Mungu amewasamehe na huko ndiko kujikwaa kwa Roho Mtakatifu au katika lugha ya kibiblia inaitwa kumkufuru Roho Mtakatifu kwa sababu usipo amini Mungu amekusamehe maana yake umemtuhumu kwamba ni muongo amepingana na maneno yake.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni