Jumapili, 28 Juni 2015

JIIMARISHE KATIKA UAMINIFU


JIIMARISHE KATIKA UAMINIFU
- Uaminifu nitakao uonyesha  mimi kama mwamini kwenye uso wa Mungu, ndio utakao
sababisha hali ya wepesi wa baraka za Mungu katika maisha yangu.

- Baraka za Kimungu zinaambatana na mkristo aliye mwaminifu katika sehemu kuu mbili, 
a). Katika maneno yake
b). Katika matendo yake

- Nikiwa mkristo ninaye mwamini  Yesu Kristo maisha yangu yakakosa uaminifu kibiblia nitaitwa mpinga Kristo, kwa sababu mkristo aliye kamilika katika imani maisha yake lazima  yadhihirike katika maeneo yafuatayo:-
i). Katika Imani
ii). Katika Tendo
Jambo hili hata maandiko yameliweka wazi Yakobo 2:26 

- (Maisha ya wakristo wengi  hayana mafanikio kwa sababu wanayanajisi katika dhambi yaani hawataki hali ya ukamilifu)

- (Kama nimeamua kumcha Mungu inatakiwa nimche Mungu katika hali ya uaminifu)

- (Kanisa likiwa halijengwi katika misingi ya Neno la Mungu maana yake unatengeneza kizazi cha jehanamu)

- Mkristo mwenye ufahamu wa Neno la Mungu lazima maisha yake yastawi na kunawiri kwa sababu yanakuwa yapo katika mfumo wa uaminifu, na mkristo wa aina hii kibiblia huitwa mtu anaye ongozwa na Roho Mtakatifu. 

- Analo lisisitiza Yesu Kristo katika maandiko ni watu kujifunza Neno la Mungu, kwa sababu chanzo cha uaminifu kwenye maisha ya mwamini ni pale ambapo anaongezeka katika ufahamu wa rohoni.  Yohana 8:31-32

- (Maisha ya ukweli ndiyo yanayo lazimisha uso wa Mungu kuyabariki maisha ya mtu)

- uaminifu umegawanyika katika maeneo yafuatayo ;-
1. Kuna uaminifu katika utoaji
2. Kuna uaminifu katika kuomba.
3. Kuna uaminifu katika kufunga
4. kuna uaminifu katika mahudhurio  ya vipindi vya kanisani. 
5. Kuna uaminifu katika maisha yangu ya kila siku na hapo ndipo nyeti zaidi. 

- Wakristo walio wengi uaminifu wao upo katika mazungumzo ya mdomoni na sio katika matendo  yao ndio maana mara nyingi  hujikuta wanapishana  na baraka za Mungu. 

- ANGALIZO NO. 1
Kinywa changu kinapo funguka nikazungumza mtu mwenye ufahamu ndiko anapopatia picha ya kufahamu moyo wangu unawaza nini dhidi yake au dhidi ya mtu mwingine, ndio maana maandiko yanasisitiza katika Malaki 2: 7 nikiwa kama mtu ninaye mwamini Mungu lazima nifikirie mara mbili mbili kabla ya kunena chochote, juu yaa hili nikiweza kulidhibiti nitaitwa mkristo mwenye kipawa cha kuidhibiti nafsi.

- Uaminifu katika maisha ya mcha Mungu ndio utakao msaidia kuongozwa na maarifa ya Kimungu katika maisha yake. 

- Nikiwa mwaminifu katika mazingira yote haitakuwa rahisi kwangu kupotoka kwa sababu moyo wangu utakuwa umekaliwa na mapenzi ya Mungu, kwa hiyo kila kitakacho toka katika kinywa changu kitakuwa ni uzima kwa yule asikiae. 

-  Baraka ya kwanza itokanayo na uaminifu na kuyavaa maisha ya mtu ni kibali mbele za Mungu na mbele za wanadamu.  

- Ndio maana maono ya Yohana Mungu alimsisitiza kuhusu uaminifu Ufunuo 2:10 

- Mungu alisisitiza suala la Uaminifu katika Ufunuo wa Yohana 2:10 kwa sababu uaminifu ndio unaotengeneza mazingira ya mtu kuishi katika maisha ya ukweli na ndicho kimpendezacho Mungu. 

UFAFANUZI KUHUSIANA NO.1  UAMINIFU KATIKA UTOAJI

Somo hili litaendelea wiki ijayo........

Hakuna maoni: