SABABU ZA WAKRISTO KUWA MASKINI. SEHEMU YA 3
- Utoaji ni upendo, mara nyingi mkristo aliyesimama katika Imani, Imani yake hudhibitishwa na mambo yafuatayo :-
i). Upendo ii). Imani iii). Utoaji iv). Huruma , haya mambo ndiyo yanayoifanya Imani ya mkristo izidi kustawi zaidi katika maisha ya kiroho
- Kanisa lisipofundisha utoaji maana yake linatengeneza kizazi cha umasikini, kwa hiyo ili tuweze kuliepuka hili inatakiwa viongozi wa kiroho walifundishe kanisa misingi hai ya utoaji yaani utoaji ulio sahihi.
- kama sijafahamu kanuni za utoaji ndivyo ilivyo, mkondo wa baraka hauwezi kutiririka katika maisha yangu, na hii mara nyingi inatokana na wakristo kutokuwa na ufahamu, ndio maana hata katika suala la uchumi huyumba sana lakini pia maandiko yamedhibitisha katika kitabu cha Hagai 1:9
- Nyumba ya Mungu ambayo Biblia inaizungumzia katika Hagai 1:9, kwa tafsiri ya Roho Mtakatifu nyumba ya Mungu ni :-
i). Yatima. ii). Wajane. iii) Masikini. iv) Madhabahu yaani kiongozi wangu wa kiroho kwa sababu miongozo ya kila kitu inatoka kwake.
Hii ndio nyumba kamili kibiblia ambayo inatakiwa nitumie mali zangu kuijenga.
- Mungu hawezi acha kunibariki nikiwa nina juhudi katika kuugusa moyo wake, je naugusaje moyo wa Mungu? Naugusa moyo wa Mungu kwa kuhudumia jamii tajwa katika mstari wa juu.
- Mara nyingi utoaji limekuwa ni jambo linalo leta maumivu katika maisha ya wakristo walio wengi, lakini utoaji ni jambo ambalo linaupendeza moyo wa Mungu vile vile ni jambo linalo uleta uso wa Mungu karibu na maisha yetu.hata biblia imesema katika Zaburi 126:6
- Chochote ninacho kitoa iwe kusaidia au kubariki kibiblia inaitwa ni mbegu, ndio maana mimi kama mwamini ninapo kwenda kupanda mbegu yangu katika shamba yaani ninapokwenda kumsaidia mtu inatakiwa nipande mbegu inayo eleweka na isiwe ile mbegu iliyo liwa na wadudu.
- ( Jinsi ninavyo jihandle na kujithamini kupitia mali zangu kama ningemhandle Mungu na kumthamini Mungu katika mali zangu ningekuwa na maisha ya juu sana katika maisha ya kimwili na kiroho).
- ( Ni vigumu kujua thamani ya kumtolea Mungu nikiwa bado sijatubu dhambi).
- Inatakiwa niwe makini sana ninapo mpa Mungu sehemu ya mali zangu, maana yake nikianza kutangaza kile nilicho mpa Mungu kwa jamii nyingine maana yake ninamsimanga Mungu sio yule mtu niliye mpa, kwa hiyo katika hili kunaweza kukazaliwa athari zifuatazo:-
i). Milango ya baraka kujifunga
ii). Kupoteza kibali kwenye uso wa Mungu na uso wa wanadamu
iii). Kupoteza mfumo wa kuisikia sauti ya Mungu katika maisha yangu ehh Yesu nisaidie nisianguke katika hilo anguko.
- Nikitambua mali nilizo nazo nimeazimwa na Mungu kwa muda haitakiwi nijivune kwa chochote, hata maandiko hili jambo yamelithibitisha katika 1Sam 2:6-8
- Utajiri wa Kimungu unakuja katika maisha ya mtu katika mazingira haya :-
i). Kuijali sana jamii ya wahitaji
ii). Kuithamini na kuilinda Neema ya Mungu inayo kusababishia baraka kwenye maisha yako kwa maana zaidi kiongozi wa kiroho kumtunza asipungukiwe na kitu, juu ya hili kuna maelezo.
MAELEZO KUHUSU KIONGOZI WA KIROHO:
- Inafahamika wazi kiongozi wa kiroho ni mjumbe wa Bwana katikati ya kanisa, yaani jamii kubwa ya waamini hutegemea neno linalotoka katika kinywa chake kuyaendesha maisha yao vile vile huamini kabisa hekima itokayo kinywani mwake pia mafunuo kwamba ni Mungu anasema,
- Ili niweze kuyalingana maneno ya Mungu inatakiwa nifanye mbinu zozote zile za ziada zitakazo ufanya moyo wa kiongozi wangu wa kiroho kuwa na furaha muda wote kuhusu mimi.
mfano katika hali ya kibinadamu baba akiwa ana tabia ya kuwatuma watoto wake wawili kila mmoja sehemu yake wakanunue vitu sehemu tofauti, katika watoto hao wawili mmoja anatabia ya kurudisha chenchi kwa baba na mwingine anatabia ya kuficha na kudanganya kwamba imeisha, je moyo wa baba utamthamini mtoto yupi?
Jibu hili inatakiwa nijibu mimi msikilizaji
ANGALIZO NO 1
- Thamani ya kitu kwa mtu asiyekuwa na ufahamu siku zote hawezi kuiona wakati kitu hicho kipo, bali anakuja kugundua thamani ya hicho kitu wakati kitu hicho hana uwezo nacho tena kukipata.
UFAFANUZI KUHUSIANA NA
ANGALIZO HILI
- Mfano mzuri ni kiongozi wangu wa kiroho anayeniongoza mimi leo wakati huu alionao wa sasa labda anauhitaji wa pesa, na kwa wakati huu ndipo ambapo mimi kama mwamini inatakiwa nijenge msingi wangu wa kupanda mbegu katika maisha ya kiongozi wangu wa kiroho kwa sababu siku za usoni hatakuwa tena na uhitaji wa pesa, kwa hiyo hata nitakapo mletea siku za usoni nitakuwa ninaongezea tu mahali ambapo pamesha jaa, kwa hiyo baraka ya wakati huo haiwezi kulingana na baraka ya wakati huu anapo hitaji.
- ( panda mbegu kwa mtu wakati anahitaji , maana yake wakati anahitaji ndio wakati wa kutengeneza msingi wa baraka za badae)
2 wakorinto 6:9
- ( Ninapo toa ili kumwimarisha mtumishi wa Mungu kiuchumi ili mambo yake yasikwame maana yake ninauimarisha ufalme wa Mungu, kwa hiyo kitu ambacho Mungu atakifanya ni kufungua mikondo ya baraka na wepesi kwa kila nitakacho kigusa ili nisipungukiwe chochote)
- ANGALIZO:-NO 2.
Sadaka ya fungu la 10 sipaswi kukaa nayo nyumbani kwa sababu shetani anaweza akanijaribu kupitia hilo, ili niweze kuepuka hiyo laana ya kula fungu la 10 inatakiwa pale tu linapoingia inatakiwa niliwasilishe kwenye madhabahu ya Bwana hata kama sio siku ya ibada.
- Mfano mzuri kwenye Biblia wa mwanamke aliye pata urejesho wa maisha yake kwa sababu ya utoaji ni Dorkasi : Matendo ya mitume 9:36- 43.
- Utoaji wowote ninao ufanya huwa ninaugusa moyo wa Mungu kwa hiyo hata kukiwapo sababu yoyote ya kulaumiwa Mungu huifunika aibu hiyo
- Maisha yangu yakiwa yamejaa matendo mema na wakati huo huo naijali jamii ya wasio kuwa nacho yaani masikini baraka za Mungu zitatengeneza chem chem katika maisha yangu, na wote tunafahamu sifa za chem chem,
i). Kuhusu sifa ya chem chem huwa haikauki hata kama ni kiangazi
- Sababu ya Petro kukubaliana na ujumbe aliotumiwa kuhusu Dorkasi ni nini? kuna mazingira kadhaa yaliyo tumika
(a). Ni kibali alicho kuwa nacho Dorkasi kwenye uso wa Mungu, na kibali hiki kilitokana na mazingira yafuatayo:-
i).alikuwa akitoa sadaka kwa masikini.
ii). alikuwa akiijali jamii ya yatima na wajane, kwa hiyo hata Petro alipotumiwa ujumbe ulikuwa dhahiri kwake kwa sababu roho aliyekuwa anatumika na Petro ndio yule ambaye Dorkasi alikuwa akimtendea vyema.
- Utoaji una nafasi kubwa sana kwenye uso wa Mungu kwa sababu utoaji umebeba mambo kadha wa kadha ndani yake:
i). Umebeba huruma
ii). Umebeba Msamaha
iii) Umebeba Imani iv). Umebeba Unyenyekevu v). Umebeba uthamani wa kutambua kitu fulani vi). Umebeba Upendo na hapo ndio top.
- Inatakiwa nione uthamani wa mwenzangu wakati ana njaa na sio wakati amesha shiba
Roho wa Bwana katika kanisa tuna mtambua katika mazingira yafuatayo: -
A).madhihirisho ya Roho Mtakatifu , na madhihirisho haya yamegawanyika katika maeneo yafuatayo:
i) . Ufunuo wa Neno la Mungu ndani ya kanisa
ii. Madhihirisho ya uponyaji Kwa watu walio wagonjwa.
iii) madhihirisho katika ishara mbalimbali n.k
B). Kuwahudumia masikini, yatima na wajane.
SOMO HILI LINAENDELEA WIKI IJAYO ..........
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni