Jumapili, 24 Mei 2015

SABABU ZA WAKRISTO KUWA MASKINI SEHEMU YA PILI

UJUMBE WALEO
SABABU ZA WAKRISTO KUWA MASKINI
SEHEMU YA PILI
Watu wengi sanasana jamii ya waaminio huwa wana utayari mdogo wa kutii ,vilevile kutendea kazi Neno la Mungu pale wanapopewa mwongozo, ndivyo hata mafanikio yanavyyokuja kwa kusuasua.


Mafanikio ya kiuchumi katika maisha yangu yanakuja kwa njia moja  ya utoaji ,kwasababu namna ninavyotoa kusaidia wahitaji ndivyo ambavyo ninaongeza kiwango change cha kupokea kutoka kwenye uso wa Mungu , juu ya hili utoaji ni thamani kubwa na inayoleta moyo wa Mungukaribu na uchumi wa mtu.

Utoaji ni sehemu kamili ya ibada kwenye uso wa Mungu.

Baraka za Mungu zinajifunga kwenye maisha ya waamini sanasana jamii ya waaminio walio wengi hawana hulka ya utoaji, ndio maana hata Mungu mwenyewe haoni sababu ya kuwabariki  na maneno haya yanathibitishwa wazi katika Maandiko Matakatifu.
Ni vigumu kupokea Baraka za Bwana ikiwa mimi  mwamini sijaandaa mazingira ya kubarikiwa .

(Hakuna maombi yatakayo imarisha uchumi wangu nje na utoaji
Matendo ya Mitume 10:1-4)

Sababu za sadaka ya mkristo kusikika kwenye uso wa Mungu na kuwa ukumbusho maana yake mkristo huyo ametoa katika mazingira haya:-A)Ametoa kuwasaidia maskini Wagalatia2:10.

Tatizo la watu wengi wanatoa nje na utaratibu wa Roho Mtakatifu, ndio maana utoaji wao hauwazalii Baraka .

(Mimi kama mwamini inatakiwa nitafute watu wa kuwasaidia ili nipate chanzo cha Baraka kuja kwenye maisha yangu
2Mambo ya Nyakati 20:20.

Nikisahau kuujenga mwili wa Kristo kwa kutoa basi nijue wazi shetani atajenga msingi wake kwenye maisha yangu  na msingi wa shetani utakuwa umegawanyika katika makundi haya:-

Ukweli ni kwamba kama familia yangu yenyewe siwalishi vizuri mimimwenyewe sijithamini katika kuvaa vizuri,Je! Nitakuwa na uwezo gani wa kukumbuka yatima na wajane ‘’Eee Yesu nisaidie’’.

Mimi kama mkristo mwamini kuna vitu ambavyo inatakiwa nile navyo sahani moja ili niweze kuuteka moyo wa Mungu
I)Mtumishi wa Mungu :kuhusu Mtumishi wa Mungu ndipo jicho la Mungu lilipo kwasababu yeye amebeba dhamana ya Mungu.
II) Yatima na wajane.

(Hakuna lingione lolote ninaloweza kulifanya likamgusa Mungu nje na utoaji , kwasababu utoaji ndio umebeba dhamana ya utakatifu katika maisha ya mtu Malaki 3:10).

ANGALIZO 1:Kipengele cha utoaji shetani amewapiga wakristo wengi upofu ili wasitambue uthamani wa utoaji kwenye maisha yao ,kwasababu yeye anafahamu fika Baraka itokanayo nautoaji Yeremia 23:23,24.

Mungu akiwa ana faida na maisha yangu hawezi kuruhusu mimi niondoke mapema duniani ,kwahiyo atanipa nafasi endelevu ili niweze kuyafurahia mema ya nchikama alivyosema katika kitabu cha Isaya 1:19.

(Siku zote maisha ya visasi hayaruhusu mafanikio katika maisha ya mtu, nikitaka kupona juu ya hiliinatakiwa nijiunganishe na Neno la Mungu katika mazingira haya:-
i)Kusoma Biblia
ii) Kusikiliza Neno la Mungu katika mfumo wa Roho Mtakatifu
iii) Kutafuta neno linalotoka katika kinywa cha Mungu kupitia Mtumishi wake

B)Ametoa kuwasaidia yatima na wajane
1Yohana 3:17
Yakobo 1:26,27

(Baraka za Mungu zinatoka kwa Mungu kuja kwenye maisha ya mkristo anayemwamini Yesu Kristo huja kwa njia ya utoaji na hapohapo ndipo unapopimwa uthamani wa dini ya mkristo).

(Nikitaka kufurahia maisha ya wokovu inatakiwa nitembee katika kanuni za Roho Mtakatifu.’’Eee Mungu nisaidie’’).

Mkristo akianzisha njia za utoaji Mungu hufungua mlango ili asipungukiwe pale anapotoa , kwasababu upendo huwa unadhihirisha picha wazi ya Mungu aliyeko ndani ya mtu.

Kama ninahitaji mapenzi ya Mungu yathibitike kwenye maisha yangu inatakiwa niibebe nafsi  ya mwenzangu kama nafsi yangu , hata hili neno Yesualiliagiza mwenyewe kupitia kinywa cha Paulo Mtume katika 1 Yohana 3:17.

(Hakuna mabadiliko ysa kiuchumi yatakayotokea kwenye maisha  ya mtu mpaka andiko litimizwe).

(Lazima nyuma ya imani yangu kuwepo na tendo ndipo mambo mengine yaweze kuthibitika  Yakobo 2:26.)

(Nikianza kutenda kwa uaminifu kwenye uso wa Mungu maana yake nitafuta historia yote ya mabaya yaliyokuwa yakinihukumu na kunishtaki kwenye uso wa Mungu  Isaya 43:18)


Hakuna maoni: