Jumapili, 3 Mei 2015

AMINI KATIKA NENO LA MUNGU - SEHEMU YA 3

AMINI KATIKA NENO LA MUNGU 
SEHEMU YA 3
-hakuna kitu chochote chini ya mbingu duniani na mbinguni kisicho dhibitishwa na Neno la Mungu.

- Kazi ya Neno la Mungu katika maisha ya mtu ni kuielimisha roho yake katika kumjua Mungu vile vile kuweka hali ya mwendelezo ndani ya ufahamu wake ili adumu katika kumtegemea Mungu siku zote. 

- kama nyakati na majira zinabadilika katika hali ya kibinadamu basi ujue wazi zinabadilika vivyo hivyo katika mambo ya kiroho, kwa hiyo ili niweze kuendana na nyakati sahihi inanilazimu kuhudhuria vipindi vya mafundisho bila kukosa ndipo nitakuwa nina uwezo wa kukabiliana na kila changamoto itakaojitokeza kwa sababu changamoto ya jana ni tofauti na changamoto ya leo ndio maana hata maandiko yananisisitiza kupitia kitabu cha 1Timotheo4:16

- nikikubali roho yangu ielimishwe na Neno la Mungu itanipa hali ya wepesi wa kufahamu namna ambavyo Mungu anatenda kazi na watumishi wake katika nyakati hizi. 

- ( nikiwa nafahamu nyakati na majira zinabadilika basi kila siku nitabuni mbinu mbalimbali za kumsogelea Mungu )

- jambo la kufahamu katika ucha Mungu wangu baraka za Mungu kuja kwenye maisha yangu zinakuja kwanza kwa njia ya kiroho kabla ya kuja kimwili ndio maana Biblia imenisisitiza sana kwamba nafsi  yangu niitunze katika mafundisho ya maneno ya Mungu, hiyo ni dhahiri kwamba baraka za Mungu zinakuja kwa njia ya kiroho. 

- jambo la kuwa na tahadhari nalo ninapo tamkiwa mimi  ni mzima au ninapoponywa haitakiwi tena niaanze kutazama historia ya tatizo nililokuwa nalo kabla ya kuombewa bali inatakiwa nitazame neno lililotoka katika kinywa cha mtu wa Mungu na wakati huo huo nikizidi kuitunza  nasfi yangu kupitia mafundisho  ya Neno la Mungu vile vile kudumu katika hiyo misingi ya neno la mungu ndio maana biblia imeyaweka wazi katika  cha 1Timotheo 4: 16

- ninapo kuwa kwenye uwepo wa Mungu ninasikiliza neno la Mungu kupitia mtumishi wa Mungu aliyepewa dhamana hiyo nikajiingiza katika hali ya utafiti labda kutokana na mambo niliyo yaona yakitendeka na sikuyaamini maana yake ninajisababishia laana, kwa sababu kitendo cha mimi kufanya utafiti wa kuchunguza kazi za Mungu zinazo dhibitika kwa njia ya Roho Mtakatifu,shetani anaweza kuitumia njia hiyo kuniwekea hali ya kupinga madhihirisho hayo, na hapo maandiko yalishaweka kila kitu wazi kupitia kitabu cha Luka 16:27-31
- kujiimarisha katika Neno la Mungu kuna mletea mwamini faida  ya kuisikia sauti ya Roho Mtakatifu pale anapo  sema nae. 

MAMBO MUHIMU KATIKA UJUMBE WA LEO. 
- jambo la kwanza katika ujumbe wa leo ambalo ni muhimu ni kuulazimisha moyo wangu kuliheshimu na kulitii Neno la Mungu ninalo lisikiliza kwa njia ya Roho Mtakatifu, kwa sababu Biblia hii hii ninayo isoma kila siku imetoa maelezo ya kutosha  kuhusiana na Neno la Mungu ninalolisikiliza hata kitabu cha Mithali kimesema, Mithali 30:5-6
- umuhimu wa kuamini katika Neno la Mungu unaisaidia imani aliyonayo mtu kuwa na nguvu ya kukabiliana na majaribu na si kutetemeka akiingia kwenye matatizo, kwa sababu Biblia imedhibitisha dhamana ya Imani katika maisha ya mtu anaye mwamini Yesu Kristo, hata jambo hili Biblia haikusita kuisema wazi 1 Petro 1:5.
- Imani niliyo nayo kwa Yesu Kristo ndiyo inayonipa ujasiri wa kukabiliana na jaribu la aina yoyote bila kuvunjika moyo au kukata tamaa.
- Mtumishi wa Mungu anayeithamini kazi ya Mungu na kujua nini maana ya wito wake hawezi kukimbilia kufanya vyake kwanza yaani kununua magari ya kifahari, kujenga magorofa, kuweka vitega uchumi mbalimbali, na wakati huo huo kundi lake linanyeshewa na mvua kwa  maana zaidi halina sehemu stahili ya kumwabudia Mungu huyo mtu wa Mungu anakuwa bado hajafahamu uthamani wa wito wake. 
- Nikitaka Mungu acheke kwenye maisha yangu na kicheko cha Mungu ni baraka kwangu inatakiwa nihakikishe nyumba ya Mungu imekaa katika hali inayostahili yaani nyumba ya Mungu isiwe na uhitaji wowote yaani kamili. 
-( katika kuisikiliza kweli ingawa ninapata maumivu lakini msaada upo hapo hapo)
- umuhimu mwingine wa kusimama katika Neno la Mungu unaisaidia Imani yangu kukomaa katika mambo ya kiroho kwa hiyo hata katika lile jambo ninalo lihitaji kutoka katika uso wa Mungu nisipo lipata kwa wakati bado jambo hilo haitaniathiri imani yangu  kivyovyote kwa sababu imani inayo tegemea msingi  wa Neno la Mungu huwa ina tabia moja hutazama vya rohoni tu na si vya kimwili jambo hili hata Biblia imelitilia mkazo katika 2 Wakorinto 4:18
- vinavyo onekana huwa vina tabia moja ipi ? huja na kutoweka lakini visivyoonekana huwa ni vya   milele yaani havinaga mwisho na ndilo kusudi la Mungu tuweke hazina zetu katika vile visivyo onekana,  sambamba na maandiko matakatifu katika Mathayo 6:21 
- ninasisitizwa sana kuimarisha imani yangu kuimarisha imani yangu katika misingi wa Neno la Mungu ili vinavyo onekana visipate nafasi yakutawala maisha yangu   kwa sababu hazina ya kweli na ya baraka ipo katika misingi ya visivyo onekana. 

NINI KIFANYIKE ILI NIWEZE KUDUMU KATIKA MANENO YA MUNGU
- mimi kama mwamini ili niweze kudumu katika maneno ya Mungu inatakiwa nijiandalie mazingira ya kuutiisha mwili wangu kwanza kabisa humweshimu Mungu.
- kwa nini kuutiisha mwili umweshimu Mungu? mwili una asili ya dhambi ndio maana hauna nafasi katika kuurithi ufalme wa Mungu, kitu hiki lazima nikijue ili niweze kusaidika zaidi. Je ni kitu gani? mwanadamu halisi ni roho sio mwili, mwili ni hekalu la ile roho ya mwanadamu pamoja na Roho ya Mungu ndani yake vile vile mwili ndio unaotoa taswira halisi au sura halisi ya mwanadamu kwamba huyu ni fulani na huyu ni fulani 
- Nafsi inatoa taswira ya mtu katika umbo la kiroho na hii ni kwa sababu roho haina umbo maalum, vile vile mwili unatoa taswira  ya umbo la mtu katika hali ya kimwili na kujua  huyu ni fulani na huyu ni fulani. 
- Neno la Mungu ninalisikiliza katika hali  ya kimwili lakini linanijenga na kuniimarisha  katika mazingira ya kiroho. 
- mwanadamu mwenye mwili Biblia inampa heshima kama hekalu, lengo kuu ni nini ? hata kama tunaishi katika hali ya kimwili inatakiwa mwienendo  yetu yote na maisha  yetu yote   tuyaendeshe katika mazingira ya kiroho, ndio maana Biblia imesema katika kitabu cha 1wakorinto3:16 na Wagalatia 5:25

Hakuna maoni: