Jumapili, 10 Mei 2015

AMINI KATIKA NENO LA MUNGU :- SEHEMU YA 4

AMINI KATIKA NENO LA MUNGU. - SEHEMU YA 4. 
- Je kwa nini inatakiwa niamini zaidi katika neno la Mungu? 

 Jibu:- Inatakiwa niamini zaidi katika Neno la Mungu kwa sababu Neno la Mungu ( Biblia ) ndio utambulisho pekee unaoweka muunganiko  kati ya Mungu na mwanadamu.

- ( Wakristo wengi tunashindwa kwa sababu hatujaamua kuutumia utambulisho wetu ambao ni Neno la Mungu  sawa sawa kivipi? )

- Mfano:- Kama Biblia ni utambulisho wangu kwenye uso wa Mungu na hapo hapo mimi ni mwamini na ikapita siku moja bila kuisoma Biblia, maana yake siku hiyo sijazungumza na Mungu kabisa, sasa ikiwa sijazungumza na Mungu siku hiyo maana yake kuna ambaye   nitakuwa nimezungumza naye kwa siku hiyo na atakuwa ameichukua siku yote, je imani yangu itakuwa katika hali gani? na wakati huo imani  yangu inalitegemea Neno la Mungu.

- ( Kama ninafahamu kwamba Biblia ni Neno la Mungu na mbingu na nchi vimeumbwa kutokana na Neno basi Biblia na iheshimiwe )

- Ninapo shika Biblia kuisoma inatakiwa nihitaji kwanza msaada wa Roho Mtakatifu kwa sababu nikiisoma Biblia nje na Roho Mtakatifu maana yake ninakuwa ninaisoma Biblia katika hali ya Kimwili, kwa hiyo nikiingia katika kuanza kuielezea nitaielezea kama historia na wote tunafahamu  historia haina kitu kipya.

- Siku zote ukitaka kuielewa Biblia au kupata mafunuo ya Neno la Mungu isome katika hali ya kiroho yaani katika mazingira ya kiimani. 

- Agizo kuu la Yesu Kristo kwa jamii ya kizazi hiki  liko katika Yohana 8: 31-32

- Jamii ya wakristo waamini mara nyingi inaathirika sana katika matatizo mbali mbali hii ni kwa sababu hawana muda wa kuzingatia mafundisho ya Neno la Mungu, na inafahamika wazi hakuna ambaye anaweza kuzingatia jambo na akaacha kufanikiwa. 

- Nazungumza kibinadamu mwanafunzi asiyezingatia masomo ya mwalimu wake shuleni matokeo yake huja amefeli. 

- ( katikati yetu atafanikiwa yule anaye yazingatia mafundisho ya Neno la Mungu anayo yasikiliza ).

- Neno la Mungu limepewa dhamana ya kumrithisha mwamini baraka yoyote anayo ihitaji kutoka kwenye uso wa Mungu ndio maana jambo hili linahitaji Imani zaidi. Yohana 14: 23. 

- Kama kweli Mungu akiweka makao ndani ya mtu huyo mtu atakuwa ni mwanadamu sawa  lakini atakuwa  si mwanadamu wa kawaida na ndicho ninacho kitafuta mimi Yesu nisaidie.

- (Mungu anaweka makao ndani ya mkristo kutokana na mkristo huyo anavyo weka bidii katika kuyazingatia maneno ya Mungu. )

- Unapoyazingatia maneno ya Mungu kibiblia unaitwa mtu unayeyatendea  kazi maneno ya Mungu. 
- Ili Mungu aweke makao katika maisha ya mwamini inatakiwa mwamini huyo aishi sambamba na hayo maneno ya Mungu yanavyo agiza. 

- Waamini  wengi wamepoteza hali ya mafanikio, uponyaji, miujiza kwa sababu baada ya kutamkiwa hurudi katika mazingira ya kujinasi kwa hiyo jambo hilo huyafanya maisha ya mwamini kudumaa na kukosa mwelekeo. 

- Ili niweze kuyatunza maisha yangu na mpaka muujiza wangu udhibitike machoni pangu, inatakiwa nifanye mambo  yafuatayo :- 
i.) Kumsikiliza Mungu namna ambavyo anasema na moyo wangu kuliko rafiki,ndugu na n.k, kwa sababu mkweli ni Roho Mtakatifu. 
ii.) Kutafuta ushauri kwenye Neno la Mungu hapo ndipo nitakapo patia usahihi wa mambo  
-(Nikitafuta ushauri kwenye Neno la Mungu nitajibiwa kwenye haki na  kweli )

- Muunganiko wa mwamini na Neno ndio unao tengeneza mazingira haya :-
a). Imani. b). Baraka. c). Uponyaji. d). Rehema. e). Uaminifu. f).Utoaji. g). Huruma 
h). Msamaha.
i ). Utu wema 
Kwa hiyo mtu wa aina hii Kibiblia anaitwa mwamini aliye amua kuikana nafsi yake kwa ajili ya upendo wa Mungu. 

- Neno la Mungu ni upendo wa Mungu kwa wanadamu wamwanio,ndio maana hata maandiko yanasisitiza  tuwe makini sana kisitokee kitu kikatutenga na upendo huo, hii ni kwa sababu  upendo huo uliletwa kwetu kwa gharama.  Warumi 8: 35 - 37

- Mambo haya ni ya kuwa na tahadhari nayo sana  Ee Yesu nisaidie yasije yakanikuta, na kama tayari yamenikuta Ee Yesu nisaidie nibadilike leo. 
i ). Ninapo mvunja mwenzangu moyo kuhusu Mungu maana yake nimeusaliti Upendo wa Mungu. 
ii.) Ninapo zini au kutamani maana yake nimeusaliti upendo wa Mungu. 
iii.) Ninapo acha kuwaheshimu wazazi wangu na viongozi wa kiroho yaani kutokwenda katika miongozo wanayo nipa vile vile nimeusaliti upendo wa Mungu. 
iv.) Ninapo farakanisha ndugu na ndugu na kutengeneza chuki  katika ya mtu na mtu pia ninakuwa nimeusaliti upendo wa Mungu. 
v.) Ninapo wanena vibaya watumishi wa Mungu na kuwazushia mambo vile vile kuchangia maneno wakati wanatukanwa pia nimeusaliti upendo wa Mungu, kwa hiyo nisipo chukua tahadhari mapema kubadilika katika maisha haya laana itaanzia kwangu mpaka kwa kizazi changu kijacho na hakuna atakaye weza kuitengua mpaka nitubu  Ee Yesu nisaidie nisiwe miongoni mwa hao watu.

- Athari nyingi zinayakumba maisha ya wakristo waamini kwa sababu sio wote wanapata bahati wa kuyasikia mafunuo ya  Roho Mtakatifu kupitia Neno lake. 

 MAMBO  YAKUFANYA ILI NENO LA MUNGU LIWE HALISI KWANGU.
- Neno la Mungu likiwa halisi kwangu siwezi kubaki na maisha niliyo nayo lazima yatapata mabadiliko. 

- Nikitaka Neno liwe halisi inatakiwa nifanye mazoezi ya kiroho kila iitwapo leo yaani nijilazimishe kusoma Biblia hata kama moyo hautaki vile vile nijilazimishe kuomba na kusikiliza Neno la Mungu hata kama mwili unakataa kutoa ushirikiano.

- Nini maana ya mwili kukataa kutoka ushirikiano katika Neno la Mungu?
i).Ni ile hali ya kuingia kanisani badala ya kusikiliza mafundisho ya Neno la Mungu Unaanza kulala usingizi.
ii.) Ni ile hali ya kuingia kanisani badala ya kusikiliza Neno la Mungu unaanza kukumbuka madeni unayo daiwa, matatizo uliyo yaacha nyumbani, watu ulio gombana nao, na namna ambavyo utalipiza kisasi. 
iii.) Kuacha kusikiliza Neno la Mungu na kuanza kukagua washirika wenzangu wamevaa nini na hapo hapo kuanza kuwatolea hukumu, na mengine yanayo fanana na hayo. 
- Mfano katika Biblia wa Mtumishi wa Mungu ambaye Neno la Mungu lilikuwa halisi kwake ni Yoshua, na je ni mazingira yapi yaliyotokana na uhalisia wa Neno? Yoshua 1: 5 - 8

1.Imani 2. Ujasiri 3. Uaminifu 4. Ufahamu.  n.k

Hakuna maoni: