Jumapili, 5 Aprili 2015

NATAMANI KIU YA KUMTAFUTA MUNGU

UJUMBE WA PASAKA LEO TAR. 5/4/2015

NATAMANI KIU YA KUMTAFUTA MUNGU.

- Waamini wengi suala la kumtafuta Mungu wamelifanya ni kama desturi, ndio maana bado maisha yao ya kiroho yana ugumu sana katika mafanikio ingawa wanajuhudi ya kumtafuta Mungu.

- Mkristo mwamini ndani mwake akiwa ana kiu ya kuyatenda mapenzi ya Mungu ni jambo ambalo linaweza kupata wepesi zaidi na likafanikiwa kwa sababu ndani ya kiu kuna nguvu ya ushawishi.
- ( Yesu kristo naomba  unisaidie niwe na kiu ya kuyatenda mapenzi  yako )
- kiu ya kuyatenda mapenzi ya Mungu ndio itakayo niunganisha au kunipatia wepesi wa kumsogelea Mungu. 
- bidii  ya mtu inaletwa na ile hali ya kiu aliyo nayo mtu kwenye moyo wake. 

- kiu ya kumtafuta Mungu itaniletea faida nyingi sana na mojawapo ya faida hizo ni : 
a). kuufanya moyo wangu kuwa na bidii katika kumcha Mungu 
b). kuyawekea tahadhari maisha yangu ya kiroho 

- (maisha yangu ya kiroho yatakuwa salama kama nikipevuka macho ya kiroho (macho ya kiimani), hii itanisadia kunipa hali ya usahihi katika ucha Mungu )

- kiu ya kumtafuta Mungu kwenye moyo wangu itaanza pale ambapo mimi Samwel nitakapo ruhusu hali ya kutendea kazi maneno ya Mungu.

- (ukweli unamfanya Mungu ajidhihirishe katikati ya kundi.)

- ( nisipo yaingiza maneno  ya Mungu ninayo fundishwa kwenye vitendo maana yake muunganiko wangu na Roho Mtakatifu haupo, kwa sababu tukirudi katika maandiko kitabu cha  1 Wakorinto 2:10 tunaona picha wazi mfumo wa Roho Mtakatifu namna ulivyo.

- ikiwa mkristo hana tabia ya kuyatendea kazi maneno ya Mungu mlango wa  Roho Mtakatifu  wa kumletea ujumbe unajifunga, ni mfano wa kaburi lililo jengwa kwa tyris kwa nje lakini kwa ndani ni mifupa mitupu, ndivyo alivyo  mkisto asiye yatendea  kazi maneno ya Mungu.

-  Ukweli ni kwamba Roho Mtakatifu ana tabia ya kujifunua kwa mkristo mwamini mwenye tabia ya kuyatendea maneno ya Mungu kazi na si vinginevyo , ndio maana jamii nyingi ya wakristo waliookoka wanatembelea hisia 

- sauti ya Roho Mtakatifu ikijifunga ndani ya mtu uhalisia unatoweka hisia ndizo zinasimama. 

- ( ukimkuta mkristo ambaye tayari mlango wa Roho Mtakatifu umejifunga ambaye uhalisia umetoweka biblia mtu huyo humwita mzushi, na ndio wakristo walio jaa katika kipindi hiki, ndio maana anaweza kusimama mahali popote na  kumtukana mwamini mwingine vibaya na asione aibu, ni kwa sababu pia kuna mambo matatu yanakuwa yametoweka ndani mwake,  jambo la kwanza imani,la pili utu ,la tatu muunganiko na Roho Mtakatifu.  Tito 1:16)

- naweza nikiwa niko kwenye uwepo wa Mungu nasikiliza Neno la Mungu mara kwa mara lakini kumbe sina tabia ya kuyatendea maneno ya Mungu kazi kwa hiyo matendo yangu lazima  yatamkana Mungu na kibiblia ninaitwa muasi. 

- nikitaka kuepuka kuitwa muasi kwenye uso wa Mungu udhaifu nilioukumbatia nianze kuupinga kuanzia sasa Roho Mtakafifu ataniwekea wepesi. 
- Neno la Mungu linalo lenga mapenzi yangu hilo ni neno ambalo lina nafasi kubwa ya kuniletea mabadiliko katika maisha yangu.

Nikitaka kiu ya kumtafuta Mungu iumbike ndani mwangu natakiwa nifanye mambo yafuatayo:
i). kwanza kabisa mimi mwenyewe kukemea vile vile kujizuia katika udhaifu unaonitoa nje na mapenzi ya Mungu



Hakuna maoni: