Jumatatu, 6 Aprili 2015

KAA CHINI YA UTAWALA WA ROHO MTAKATIFU

PASAKA YA PILI: 6/4/15

MESAGE : KAA CHINI YA UTAWALA WA ROHO MTAKATIFU 
- kukaa chini ya utawala wa Roho Mtakatifu ni muhimu sana, kwa sababu maisha ya kila mkristo mwamini yanahitaji msingi halisi wa Roho Mtakatifu ili apate hali ya wepesi katika kukabiliana na kila changamoto(majaribu).

- Majaribu katika maisha yetu kama waamini  hayaepukiki, ila tunahitaji mahusiano mazuri na Roho Mtakatifu ili kutupa hali ya wepesi wa kuvuka. 
- mahusiano mazuri na Roho Mtakatifu ndiyo yanayo mpa mwamini kibali cha kuvuka katika ugumu bila kuathiriwa kiimani.
- Roho Mtakatifu ni nafsi muhimu kuwepo kwenye maisha ya mtu kabla ya kulitumia jina la Yesu Kristo, kwa sababu Roho Mtakatifu ndiye aliyekabidhiwa udhihirisho wa kila kitu katika maisha ya wanao mwamini Yesu Kristo.
- maneno haya yanadhibitishwa na Yohana 14:26
- ( nikishapatana na Roho Mtakatifu tayari ndani mwangu ninakuwa na mamlaka yenye uwezo mkubwa sana wa kulitumia jina la Yesu Kristo mahali popote na likatenda kazi )
- ili niweze kupata mtiririko wa Roho Mtakatifu inatakiwa niwe na kiu katika mambo yafuatayo: 
i). kiu ya kusoma Biblia mara kwa mara 
ii). kiu ya kuomba wakati wowote
iii). kiu ya kutenda mapenzi ya Mungu.

- Neno la Mungu lina tabia ya kuwaunganisha wanadamu wote pamoja, kwa sababu ndani yake limejaa upendo na msamaha. 
- ( nikiendelea kuambatana na Roho Mtakatifu nitakuwa ushuhuda mzuri kwa jamii iliyo nizunguka yaani kwa wale wote waliokuwa wananifahamu historia yangu ya kale.
- ( Neno la Mungu linaigeuza historia  ya mtu mara moja )  
- kazi ya Roho Mtakatifu kwenye maisha yangu kama mwamini ni kuhakikisha sitoki katika mfumo wa kumcha Mungu ndio maana jukumu  lake liliwekwa wazi katika Yohana 14:26. Baadhi ya majukumu yake ni :
a). Msaidizi  wa maisha yangu katika maeneo yenye ugumu ( majaribu, n.k)
b). kutufundisha, ina maana zaidi kutujenga katika misingi ya kumuishi Mungu(Neno).
c). kutukumbusha, ina maana zaidi kutusaidia kutokuathiriwa na mazingira tuliyo yapitia nyakati zilizo pita. 
-( haitakiwi nikumbuke mambo yaliyopita yasiyo faa, yanaweza kuniathiri imani yangu ikadhoofika upya ndio maana nabii Isaya alisema wazi Isaya 43:18.
- ili niweze kuepuka kuathirika kiimani inatakiwa nifanye bidii ya ziada katika kumtafuta Mungu ili nipate uwezo wa kumsikia Roho  Mtakatifu, hii itanisaidia maisha yangu yakiimani kupata tahadhari.

Hakuna maoni: