Jumapili, 29 Machi 2015

MSAMAHA

SOMO LA LEO: 29/3/2015

MSAMAHA:-

Neno Msamaha lina maana nyingi vile vile lipo katika mazingira tofauti tofauti, 
a). Kuomba msamaha
b). Kusamehe
c). Kusamehewa



Ufafanuzi kuhusu kipengele ( a ) kuomba msamaha.

- Kuomba msamaha ni hali fulani ya kutubu au kujutia kosa vile vile ni kutambua nilipokosea. 
- kuomba msamaha kunaonyesha hali ya ukomavu wa kiufahamu katika maisha ya mcha Mungu.
- ( Nitaonekana ni mwenye hekima machoni pa Mungu na machoni pa ulimwengu huu  nikiwa mtu mwenye tabia ya kuomba msamaha ninapogundua kosa.)
- kuomba msamaha kunadhihirisha wazi hatua za mabadiliko katika maisha ya huyo mtu

Mfano mzuri katika Biblia ni Petro mtumishi wa Mungu, Luka 22:54- 62 
- Ishara aliyoionyesha Petro ya kulia kwa majonzi ni ishara ya toba au kutubu.
- Kutubu au kuomba msamaha ni hali inayomaliza hasira katika moyo wa mtu anayetendewa 
- roho ya kuomba msamaha ipo ndani ya mtu wa aina hii:

  i ). Ipo ndani ya mtu ambaye moyo wake umeelimishwa kupitia maneno ya Mungu tu, huyo ni mtu anayeweza kuchukua hatua ya ujasiri kuomba msamaha. 
-( kushindwa kuomba msamaha mara nyingi kunasababishwa na roho  ya uasi iliyopo ndani ya mtu,  vile vile siku zote mwenye kiburi hawezi kuomba msamaha).
- hali ya kuomba msamaha inadhihirisha hatua za ukuaji wa kiimani katika maisha ya mkristo.
( nikiwa sina tabia ya kuomba msamaha maisha yangu nayapalilia katika laana, ndio maana maisha ya wakristo wengi yanayumba yaani hayana msimamo kabisa).
- kutokuomba msamaha kunadhihirisha wazi kiburi kilicho jaa kwenye moyo wa mwamini. 
- kutokuomba msamaha ni hali fulani  ya kuficha dhambi na Biblia imesema wazi juu ya hili kama ilivyo andikwa Mithali 28:13 
- kuomba msamaha kunaonyesha wazi hali  ya kuungama dhambi
- mtu asiyekuwa na kawaida ya kuomba msamaha hana uwezo wa kuacha dhambi, kwa sababu kuomba msamaha ndiko kunako onyesha hatua za mabadiliko katika maisha ya mtu.
- mtu asiye tubu kwenye maisha yake hawezi kupata mpenyo na wepesi kwa sababu maisha yake yanakuwa yameambatana na laana na ndicho kinacho yatesa maisha ya wakristo wa leo.
- dhambi haiyaachi maisha ya mtu mpaka pale anapoitubu, na hapo hapo ndipo unapo anzia mwanga wa hatua mpya za mafanikio.
- ( ili dhambi iweze kuondoka kwenye maisha yangu lazima niitubu )

ATHARI ZINAZO TOKANA NA KUTOKUOMBA MSAMAHA :
 - Kwanza kabisa katika maisha ya kawaida kutokuomba msamaha pale unapomkosea mwenzako mara nyingi huwa kunajenga uadui kati ya jamii moja na jamii nyingine, vile vile huwa kunajenga hali ya hila katika uzao wa jamii husika, ndio maana unaweza ukakuta wazazi wetu walikosana na sisi tutaishi katika mfumo huo huo wa chuki.
- kutokuomba msamaha kunaathiri mtiririko wa  Roho Mtakatifu katika maisha ya mwamini.
- Imani ikiimarika dhambi nitaiona kama mavi lakini Imani ikipungua dhambi nitaishangilia eeh Yesu nisaidie nisipunguke kiimani kwa sababu ukipunguka kiimani kifuatacho ni kudhalilika. 
- nikiiruhusu Imani yangu kukua kila dhambi niliyo itenda inabaki historia katika uso wa dunia  lakini kwenye uso wa Mungu sina  doa. 
- ili niweze kuepuka hali ya kuathirika kiimani inatakiwa neno msamaha kuyaongoza maisha yangu vile vile itakuwa ni hatua za kuepuka laana zitokanazo na dhambi. 
- mfano mzuri ni Gehazi katika Biblia kilicho sababisha ukoma ukae kwake milele hakuomba msamaha hakujutia kosa, 2 Falme 5:20-27
- Laana inaambatana na mkristo asiyekuwa na ufahamu wa kuomba msamaha ( kutubu ).

- kuomba msamaha kunarejesha upya kati ya mtu na mapenzi ya Mungu. 

Hakuna maoni: