UJUMBE WA LEO
10/4/2015
NAMNA YA KUISHI KATIKA HAKI
Ili niweze kuishi katika haki ya Mungu ambayo ndiyo Mungu anahitaji kuiona katika maisha ya wanaomwamini
Yesu Kristo,inatakiwa nikubali mimi mwenyewe kupata hasara ya mambo ya kimwili kwaajili
ya Mungu.
Nisipo kubali kupata hasara kwa mambo ninayoyapenda ambayo
yapo kinyume na kweli ya Mungu ni vigumu Baraka za Mungu kuambatana na mimi.
(Ukweli ni kwamba
nisipokubali kupata hasara katika mambo ninayoyapenda ni vigumu kupata
mpenyo wa mafanikio).
Warumi 14:15-19
Paulo Mtume alipoingia katika kanisa la Warumi alikuta jamii
ya waaminio wakihukumiana kwaajili ya vyakula kama ilivyoandikwa Warumi 14:17,Lengo
kuu alilokuwa nalo Mtumishi wa Mungu ni
kuifanya jamii ya waaminio kuwa na msingi katika Neno na si kuhukumiana katika
vitu vinavyoonekana.
(Siku zote vitu vya mwilini havina utukufu kwa Mungu).
(Nikiwa nina imani na maneno ya Mungu ,Mungu ataongea na
mimi waziwazi).
Inatakiwa niitumie Biblia kutatua matatizo yaliyonizunguka, kwasababu Biblia ni
sauti ya Mungu mwenyewe Yohana 1:1-3.
Nikitaka kuishi maisha ya hakilazima niliatamie Neno la
Mungu,kwasababu nguvu ya kushinda kila aina ya udhaifu ipo ndani ya Neno la
Mungu.
Neno la Mungu linafanya kazi ndani ya mtu kutokana na imani
aliyonayo katika Neno hili.
Ukiona umeombewa ukawa bado hujapokea uponyaji ni picha wazi
kwamba bado kiwango cha imani yako kina
udhaifu,kwahiyo hakina uwezo wa kukabiliana na jambo hilo,hapo inatakiwa
niongeze bidii katika kujiongeza kiufahamu wa Kibiblia.
Ili mabadiliko yaweze kutokea kwenye maisha ya mtu lazima
moyo wa mtu huyo ukubali mafundisho ya Neno la Mungu.
Moyo wangu ukikubali mafundisho ya Neno la Mungu ndipo hatua
za mabadiliko zinakoanzia,Hata kitabu cha Mithali kimesema wazi Mithali 1:8-9.
Watu wengi hatujibiwi maombi yetu ingawa tunasikiliza na
kuyasoma,sababu hii inatokana na jamii kubwa ya waaminio hawana tabia ya
kutendea kazi Maandiko Matakatifu.
(Kuishi maisha Matakatifu kuna raha yake,
MFANO-Kutambulika kwenye uso wa Mungu kwamba hata mimi ni
sehemu ya Ufalme wa Mungu Yohana 1:12).
(Maisha ya dhambi ndiyo yanayotunyima kibali cha upendeleo
kwenye uso wa Mungu).
(Haki ndiyo inayoleta kibali kwenye maisha ya mcha Mungu).
Nikiwa kama mwamini inatakiwa muda wangu mwingi niutumie
katika kubuni mbinu mbalimbali za kumpendeza
Mungu,hii itanisaidia kunisogeza karibu na uwepo wake.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni