MSAMAHA :
Sehemu ya 2. Tarehe: 12/4/2015
Haya maneno matatu a). Kuomba msamaha ,b). Kusamehe c).Kusamehewa, yapo ndani ya neno msamaha
UFAFANUZI KUHUSU NENO KUSAMEHE.
- Wakristo wengi neno kusamehe limekuwa gumu katika maisha yao mara nyingi wakristo walio wengi wanamwabudu Mungu nje na Roho Mtakatifu
- Kutokusamehe limekuwa ni jambo ambalo limewaweka wakristo waamini katika kifungo, na mwisho wake huwaletea madhara na magonjwa.
- Moyo wangu nikiunyima haki ya kusamehe maana yake naupotezea utulivu wa kuisikia sauti ya Mungu.
- Ili niweze kumlingana Mungu inatakiwa niwe mwepesi wa kusamehe katika maisha yangu
- Mlango wa Mungu kunisamehe mimi ninautengeneza mimi kwa kusamehe wale ambao ni vikwazo kwenye maisha yangu ya kila siku.
- Kusamehe kunaleta hali ya wepesi katika maisha ya mtu kujibiwa maombi yake kwenye uso wa Mungu, kwa sababu Yesu Kristo ametoa agizo hili kupitia kitabu cha Marko 11:25,26.
- Kama sina uwezo wa kusamehe chochote ninachotendwa basi hata Mungu hawezi kunisamehe chochote ninachomkosea, kwa hiyo nitabaki chini ya hukumu siku zote za maisha yangu.
- Mfano: nimemsamehe yule aliye nikosea lakini nikimuona moyo wangu unaniuma, hii ina maana kwamba sijasamehe bado.
- ( Mtu ambaye nimemsamehe lakini bado haamini kwamba nimemsamehe maana yake hiyo ni picha wazi yeye mwenyewe hana tabia ya kusamehe ).
- Kama sina tabia ya kusamehe wengine walionikosea katika mzunguko wangu wa maisha kila siku ina maana tatizo nililonalo haliwezi kutoka, kwa sababu ile hali ya kutokusamehe ni kipingamizi kinacho weka ukuta kati ya mimi na baraka za Mungu.
- ANGALIZO NO.1
Moyo nikiunyima utulivu lazima utasababisha magonjwa , ndio maana tunasisitizwa sana kusoma Neno la Mungu vile vile kusikiliza Neno la Mungu mara kwa mara, kwa sababu Neno la Mungu ndilo lina nafasi ya kuleta utulivu na tumaini jipya katika maisha ya mtu.
- Moyo ukipoteza utulivu mfumo mzima wa maisha ya mtu lazima uharibike, ndio maana inatakiwa niwe na hazina kuu katika Neno la Mungu ili vitu vyote vya kimwili nivihesabu ni bure, ndio maana kitabu cha Mathayo 6: 20,21 imeweka picha wazi.
- Moyo wangu ukiwa na hazina ya Neno la Mungu hata siku moja moyo wangu hauwezi kubeba mabaya, na hii ndio inayotakiwa iwe staili ya wakristo waliookoka au wanaomtegemea Mungu.
- Jambo ambalo inatakiwa nilijue kwenye maisha yangu ninayo ishi kila siku kuna makwazo na hayaepukiki, kinacho takiwa ni nini? inatakiwa nijiimarishe vizuri katika misingi ya Neno la Mungu ili moyo wangu upate wepesi wa kuachilia na kusamehe kila aina ya kwazo linalojitokeza.
- Nikiwa kama mkristo ninaye mjua Mungu nimepewa nafasi moja tu na ambayo inatakiwa niipende nafasi hiyo kwa umakini sana, vile vile katika Marko 11:26 kuna maneno mawili yametumika na maneno hayo ni LAKINI, KAMA.
- ( Hakuna kitu chochote ambacho Mungu anaweza kunitendea kwanza bila mimi kutanguliza msamaha, kwa sababu msamaha ndio unaosababisha mimi nipate wepesi wa kubarikiwa kwenye uso wa Mungu.)
- Taasisi iliyo bakia chini ya jua katika kutenda haki ni KANISA, kwa hiyo KANISA nalo lisipo simama katika haki na kweli mambo yatakuwa yameharibika ee YESU KRISTO tusaidie.
- Moyo wa mkristo ukishindwa kusamehe ndani yake huwa una maumivu na maumivu hayo ndiyo husababisha hali ya kulipiza visasi.
- Hasira ni roho anayopagawa nayo mtu akiwa na akili zake timamu na mara nyingi hasira huwa nayo mtu ambaye moyoni mwake hana tabia ya kusamehe.
- Kinachotakiwa kwa mkristo mwenye ufahamu wa rohoni, haitakiwi amchukie mwenzake aliye mkosea bali inakiwa aichukie roho iliyoko ndani ya huyo aliye mkosea, na hapo ili uweze kumsaidia lazima uchukue jukumu la kufunga na kuomba katika kuitoa ile roho ndani ya mtu )
- ( Njia zangu zikimfurahisha Mungu atanipatanisha na wale wote wanao nichukia )
NINI KIFANYIKE ILI KUPOTEZA KUMBUKUMBU YA MAMBO NILIYO

- huu mchoro uliopo hapo juu ni sehemu kidogo tu ya kudhihirisha namna ambavyo mkristo aliyeokoka anayesema Bwana Yesu asifiwe namna ambavyo anastahili kuwa ndani ya moyo wake , vile vile mtu wa aina hii ndiye anaye staili kuzishiriki baraka za Mungu pia hata mbingu itakuwa wazi kwa mtu huyu.
- Moyo wa mkristo aliyeokoka ukiwa una ukamilifu katika mazingira yote kama ninavyo ona mchoro hapo juu mtu huyu atapata upendeleo wa kuisikia sauti ya Mungu waziwazi ikisema
- Ninajifunza Neno la Mungu ili niweze kupata upeo wa kupambanua kazi za shetani kabla hajazileta ndani mwangu zikaniletea uharibifu.
- shetani kabla hajaanza kuingiza uharibifu kwenye moyo wa mwamini huwa kwanza anatazama aina ya madhaifu aliyo nayo mwamini na ndipo akigundua udhaifu safari yake ya kuanza kumuathiri mwamini huanzia hapo
- ( Kwa ajili ya Yesu Kristo nakubali kupata hasara ya kila kitu ninacho kiona ni kizuri katika maisha yangu na Yesu nisaidie )
- Mfano ambavyo shetani huanza kutaka kuathiri maisha ya mtu, huja kwanza kwenye moyo wake na kutazama ndani ya moyo wa mtu huyo je kuna muunganiko wake?
- Akikosa muunganiko huondoka na kwenda kujipanga upya na akiukuta muunganiko safari ya uharibifu ndani ya maisha ya mtu huanzia hapo, ndio maana tumechorewa mchoro kwa sehemu maisha yetu lazima yawe na ukamilifu ili kuzuia uvamizi wa kipepo.
- Hatutaweza kumdhibiti shetani kwenye maisha yetu kama hatutajali kuimarisha mioyo yetu kupitia Neno la Mungu.
- Mimi kama mkristo ninaye mwamini Yesu Kristo inatakiwa nitembee au niishi katika mazingira ya kusamehe hata kama hilo jambo lina maumivu ya aina gani, hapo kibiblia nitaitwa mkristo mtendea kazi neno la Mungu, hata Yesu mwenyewe kupitia kitabu cha Yakobo 5:16 alitoa agizo.
- Nikisamehe kutokea kwenye utu wangu wa moyo lile jambo nililotendwa sitalikumbuka tena kwa sababu nimesamehe katika Roho Mtakatifu.
- Mtu ambaye hana hofu ya Mungu na maneno ya Mungu hayaamini ni kuwa na tahadhari naye kwa sababu anaweza akafanya tendo lolote wakati wowote.
- Baada ya kumsamehe aliye nikwaza ninatakiwa nichukue hatua za kumwombea rehema kwenye uso wa Mungu hapo nitaitwa mkristo mwenye ufahamu wa rohoni na niliyekamilika katika upendo
- (Nikimsamehe aliye nikosea maana yake nimeyaponya maisha yake, Eeeh Yesu nisaidie niwe mtu wa kusamehe kila siku katika maisha yangu.)
.
Sehemu ya 2. Tarehe: 12/4/2015
- Wakristo wengi neno kusamehe limekuwa gumu katika maisha yao mara nyingi wakristo walio wengi wanamwabudu Mungu nje na Roho Mtakatifu
Moyo nikiunyima utulivu lazima utasababisha magonjwa , ndio maana tunasisitizwa sana kusoma Neno la Mungu vile vile kusikiliza Neno la Mungu mara kwa mara, kwa sababu Neno la Mungu ndilo lina nafasi ya kuleta utulivu na tumaini jipya katika maisha ya mtu.
- huu mchoro uliopo hapo juu ni sehemu kidogo tu ya kudhihirisha namna ambavyo mkristo aliyeokoka anayesema Bwana Yesu asifiwe namna ambavyo anastahili kuwa ndani ya moyo wake , vile vile mtu wa aina hii ndiye anaye staili kuzishiriki baraka za Mungu pia hata mbingu itakuwa wazi kwa mtu huyu.
.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni