Jumapili, 19 Aprili 2015

AMINI KATIKA NENO LA MUNGU


AMINI  KATIKA NENO LA MUNGU
Inatakiwa niamini katika Neno la Mungu, kwasababu Neno la Mungu ndilo  chimbuko halisi la Yesu Kristo, hii ina maana zaidi Yesu Kristo ametokana na Neno la Mungu tunalolisoma kila siku,hata Maandiko yanathibitisha  maneno haya Yohana 1:14

Kwanini ninasisitizwa niamini katika Neno la Mungu ni kwasababu chimbuko la vitu vyote yaani duniani, chini ya nchi, mbinguni  vimetokana na  na Neno la Mungu , kwahiyo nikiiendeleza roho yangu katika Neno la Mungu nitapata faida nyingi sana na moja ya faida hizo kuurithi ufalme wa Mungu.

Mfano katika hali ya kibinadamu:Mtoto anapopelekwa Shule lengo kuu la mzazi ni kumuendeleza mtoto wake kiakili  apate elimu itakayo mheshimisha katikati ya jamii na kuitwa mheshimiwa fulani , vilevile na kupata maisha ya duniani yaliyo bora
SWALI: Je! kujiendeleza zaidi kiroho hauoni utapata faida iliyo bora zaidi ?.

Maana kuu ya Yesu kuzaliwa katika mwili ni kurejesha kile kizazi ambacho kilishamuasi Mungu ili kiishi katika haki na kweli.

Huu ni ukweli usiobadilika na haupingiki kamwe yaani kila mwanadamu mwenye mwili atahukumiwa  na Neno la Mungu (Biblia).

Nisipo yaamini manen o ya Mungu kamwe siwezi nikaikwepa hukumu ya milele ,kwasababu Neno la Mungu  ninalolisoma kila siku  na kulisikiliza ndani yake kuna pumzi hai, ndiyo maana lina uwezo wa kuponya ,kuokoa na kumrithisha mwamini uzima wa milele , hata Biblia inayathibitisha wazi maneno haya Waebrania 4:12.

Hii ni picha wazi kwamba Neno la Mungu linanijua vizuri sana  hata kama mimi ninalisoma.

Neno la Mungu ndilo limeleta muunganiko  kati ya mwanadamu mwamini  na Yesu Kristo , hii ina maana kwamba hauwezi kusema unamwamini Yesu Kristo kama kwanza hauliamini Neno la Mungu, vilevile hauwezi kusema kwamba unaliamini Neno la Mungu  alafu haumwamini Yesu Kristo.

(Ni vigumu kusema ninayaamini Maandiko Matakatifu (Biblia)na wakati huohuo sijamkiri Yesu Kristo kuwa Bwana na mwokozi wa maisha yangu, hiyo imani haitoki kwa Mungu aliyeiumba mbingu na nchi, kwasababu Yesu Kristo ametokana na Neno , vilevile wokovu wa kuurithi Ufalme wa Mungu unatokana na Yesu Kristo, Je! Hapo kama mkristo unatafakari nini?).

Mkristo kama hajaokoka yaani hajamkiri Yesu Kristo kuwa Bwana na mwokozi wa maisha yake hawezi kusema anamjua Mungu  wala ni sehemu ya Ufalme wa Mungu, kwasababu Maandiko yanathibitisha neno hili katika kitabu cha Warumi10:9, vilevile kitabu cha Wafilipi 2:8-11.

Inatakiwa niende kanisani kwa kutamani kubadilika katika tabia niliyonayo , kwasababu Neno la Mungu ndilo lenye nguvu ya kung’oa asili yaani tabia aliyonayo mtu.

Neno la Mungu likiielimisha roho ya mwamini ufahamu wa mwamini huyo ukakua , hapo ndio utakuwa mwanzo wa huyo mwamini kuishi katika haki.

Inatakiwa nibadilishe mfumo wa maisha yangu nguvu nyingi  nguvu nyingi ninayoitumia katika kutafuta pesa inatakiwa niitumie katika kumtafuta Mungu,kwasababu pesa sio upako, ila upako ndio unaov uta pesa ,hata Maandiko yamethibitisha maneno haya Isaya 60;11,16.

Nisipoliamini Neno la Mungu maana yake nimefarakana na Baraka za Mungu waziwazi.

Jambo la kujua kama mkristo ninayemwamini Yesu  Kristo,lolote lililompata Yesu Kristo mimi kama mwamini sitaliepuka ila tunitahitaji Neema  ya Mungu isababishe wepesi wa kuvuka .


Katika safari ya kumcha Mungu katika kweli na haki yaani kwenye misingi ya wokovu inatakiwa nikubali kupata hasara ya kila kitu ndipo safari yangu itafika salama.

Hakuna maoni: