UJUMBE WA LEO
15/2/2015
TUNZA MAMLAKA ULIYOPEWA
Ili niweze kutunzaq mamlaka
niliyokabidhiwa na Yesu Kristo inatakiwa nifanye mambo yafuatayo:-
A)Nijifunze Neno la Mungu (Biblia)
Kuhusu kujifunza Neno la Mungu inatakiwa liwe ni jambo lenye
mwendelezo , kwasababu jinsi ninavyozidi
kujifunza ndivyo ninavyopata
kina cha kumjua Mungu.
(Mamlaka aliyonayo mtu inahitaji nguvu ya Neno la Mungu ili
iweze kuwajibika )
(Nikimjua Mungu mamlaka niliyopewa nitakuwa na uwezo wa kuitunza)
Watu wengi sanasana jamii ya waaaminio wanashindwa kutunza
mamlaka , kwasababu hawana muda wa kutosha
wa kujifunza Neno la Mungu.
B)Nijitahidi
kujisomea Neno la Mungu mara kwa mara
Nikijisomea Biblia kutanisaidia kuniwekea ulinzi vilevile
kutanisaidia mbinu za kudhibiti aina mbalimbali za majaribu, kwasababu ndani ya
kujisomea Biblia ninapata ufahamu wa kujua shetani pamoja na mbinu zake
anazotumia kuathiri maisha ya waamini (Wakristo).
(Kama sina muda wa kusikiliza Neno la Mungu , vilevile muda
wa kujisomea Biblia nijiandae kuwa
jalala la matatizo, kwasababu ndani
mwangu sitakuwa na mbinu yoyote ya kumkabili shetani , kwa hiyo ni rahisi yeye
kupenya na kuleta kila aina ya madhara , Sababu sina kinga yoyote).
(Kuna matatizo mengine yanayotukumba kwasababu sisi wenyewe
tunajitenga mbali na uso wa Mungu).
Neno la Mungu ni kiunganishi kinacho zaa imani ambayo
inamfanya Mungu kujua uzito wa tatizo la mwamini .
Wakristo wengi wana shida hii,wakati wa tatizo linaanza
hawaoni umuhimu wa kumtafuta Mungu, lakini wakati wa tatizo limeshakuwa kubwa
yaani haliwezekani tena ndiyo
wanamtafuta Mungu , Je!kuna kuponywa hapo?
Mungu anahitaji mwamini ambaye amefanya maandalizi ya imani yake kabla ya kuingia
kwenye uso wake kuomba .
Yakobo 5:17-18
Kuiandaa imani yangu kabla ya kuingia kwenye maombi
kutanisaidia kunipa utulivu ndani ya
moyo , vilevile kutanirahisishia hali ya
wepesi wa mtiririko wa Roho Mtakatifu katika hoja
ninazopeleka kwenye uso wa Mungu.
Kushinwa kwangu kunatokana na hali ya kutokuiandalia
mazingira imani yangu ya kupokea kitu kutoka kwenye uso wa Mungu .
Sauti ya Mungu tunaisikia kupitia kwenye mlango wa ufahamu
wa moyo wa mtu , ndio maana tunahitaji utulivu wakati wa kuomba
Mathayo 6:7.
(Kama sina utulivu kwenye moyo haitakiwi niombe , kwasababu
nitakuwa najitaabisha bure).
Ninasisitizwa kusoma Biblia ili ufahamu wangu ujengwe katika
hekima ya Kimungu.
Mwamini ambaye ni msomaji wa Biblia kinywa chake kinayo
mamlaka ambayo ina uwezo wa
kusababisha chochote kutokea muda
wowote, ndio maana tunahitaji kutamkiwa
neno na kinywa chenye mamlaka.
Nikiamini neno ninalotamkiwa kutoka kwenye kinywa chenye
mamlaka linakuwa lina asilimia zote
kudhibitika , kwasababu katika mamlaka
kuna nguvu ya neno nyuma yake inayolazimisha jambo kuumbika.
Maisha ya wakristo yamekuwa magumu, kwasababu wanashindwa kuitumia mamlaka waliyonayo, nah
ii mara nyingi hutokana na vifungo vya dhambi wanazojikwaa kila iitwapo leo.
Nguvu ya dhambi mara nyingi huunyima moyo wa mwamini uhuru
wa kuamini kile anachoomba kwenye uso wa Mungu kwamba kitajibiwa.
Mamlaka iliyo ndani ya mtu huathiriwa na mtu anavyozidi
kujikwaa katika dhambi .
KAZI YA MAMLAKA
Mamlaka inayo kazi kubwa sana ndani ya mtu,kwasababu ndio inayolazimisha mambo mengine
magumu kudhibitika hata kama sio wakati wake.
(Uovu wangu ndio unaoninyima ujasiri wa kuitumia
mamlaka niliyonyo kutnda kazi).
(Nikishakuwa na uwezo wa kusimama mbele ya adui yangu bila hofu maana yake nimeshinda).
Tuepuke kukiri udhaifu , kwasababu jinsi ninavyokirik
udhaifu ndivyo ninavyofungua malango wa kuathiriwa jumla.
Ninavyokiri kushindwa ndivyo ninavyoathiri mfumo mzima wa Baraka
za Mungu katika maisha yangu, vilevile mamlaka yangu ninaipotezea uwezo wa
kuniumbia mambo mengine kudhibitika ,
lazima nikubali kubadilisha ukiri wangu.
(Kama ninavyoweza kusikia nikaamini, ndivyo ninavyoweza
kunena ikawa).
Mamlaka humvusha mwamini katika mazingira magumu sana , hata
kama mazingira hayo hayamsapoti
Luka 10:19.
Mamlaka ina kazi ya kumtiisha shetani juu ya kitu chochote na akatii.
Kushindwa kwangu ni matokeo mabaya ya mahusiano kati ya mimi
na Mungu, ndio maana shetani hupata mpenyo wa kuniathiri.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni