Jumapili, 22 Februari 2015

KWA NINI NINASHINDWA KUSHINDA KINACHO NISHINDA

22/2/2015 UJUMBE WA LEO 
KWA NINI NINASHINDWA KUSHINDA KINACHO NISHINDA 
- Hivi kinacho nishinda kukishinda ni nini? 

- Kile ninachoshindwa kukishinda mara nyingi ndicho kipingamizi kinachofanya maombi yangu yasijibiwe kwa wakati. 
- Kwa hiyo nikimwomba Mungu na wakati huo huo nina dhambi ndani mwangu  kuna  hatari ya kutokujibiwa maombi yangu, Ee Yesu nisaidie nifanye mabadiliko. 
- Siku zote katika maisha ya mwanadamu ndani mwake kuna asili, na hiyo asili asipoweza kuishinda bado atakuwa na wakati mgumu sana wa kukua kiroho. 
- Maisha ya watu wengi waliookoka huwa yana ugumu wa kufanikiwa kwa sababu hawataki kuzivua jumla asili, kwa hiyo wanapoingia kwenye maombi ile asili huwa ndio kipingamizi chakufanya maombi yake yasipate mpenyo.
- Mwamini ambaye ameamua kuivua asili jumla kibiblia anaitwa mwamini anayeishi maisha ya kweli , na huyo ndiye Mungu anamtafuta.  
- Ile asili iliyo atamia maisha yangu ndio inakuwa kikwazo kikuu cha kuyafanya maisha yangu yasipate mpenyo kiroho na kimwili. 
- Nikijiwekea mikakati ya kupambana na asili niliyonayo huo ndio unakuwa mwanzo wa maisha yangu ya kirohoo kufunguka.
- Maisha ya mkristo mara nyingi hudhalilishwa na asili iliyo mvaa, kwa hiyo mkrish asipokuwa  makini anaweza kujikuta anaishi maisha ya maumivu mpaka mwisho wa maisha yake.
- (Asili ni ile hali ninayo shindwa kuishinda ndani mwangu)  
- nikifanikiwa kuivua asili na nikawa na msimamo katika maisha yangu ya kiroho nitaitwa mwamini ninayetembea katika kweli ya Mungu, kwa hiyo baraka za Mungu zitakuwa ni sehemu za maisha yangu Jambo hili hata Biblia imelifunua (Zaburi 51: 6)
- Maisha ya ukweli ndiyo itakayo fanya mwamini aweze kusikia Sauti ya Mungu akisema nae kwa sababu Mungu ni kweli.
- Kama Mungu ni kweli na mimi nikaishi maisha ya kweli basi nitamsikia Mungu akisema kama mimi ninavyo weza kuongea na wewe na kunisikia.
- nikiikana asili nikaipinga kabisa na nikaivua, kuna mambo haya yatakayo  ambatana na mimi :-
i). Nitaisikia sauti ya Mungu. 
ii). Nitapata kibali kwa Bwana na kwa wanadamu pia. 
iii). Nitakuwa mtu wa kubarikiwa kwa sababu mkondo wa baraka za Mungu utakuwa wazi. 
maana yake hakutakuwa na kipingamizi chochote.

- Mwamini anayeishi maisha ya ukweli ndio mwenye uwezo wa kuisikia sauti ya Mungu ikisema.
- Mungu anautumia moyo wa mtu kunena ndio maana ninasisitizwa unyoofu wa ndani ya moyo wangu ni muhimu sana. 
- Kuabudu kwa mwamini kutakuwa na maana  kwenye uwepo wa Mungu, kama mwamini ataanza safari ya kuishi maisha ya ukweli. Hata Yesu Kristo alisisitiza sana wakristo tunao mwamini tuishi katika kweli. ( Yohana 8:32 ) , hii inadhihirisha wazi kwamba faida, baraka, mafanikio, uzima vitaambatana na mwamini anayeyaishi maisha ya ukweli. 
- ( Inawezekana wewe kufanya mabadiliko kwa sababu wewe ni mtu mwenye akili timamu na kile unacho kifanya unakijua). 
- kweli ambayo Biblia inaizungumza katika Yohana 8:32 ni Neno la Mungu.
- Maisha ya ukweli ataweza kuyaishi mkristo ambaye ameamua kuzama katika kina cha neno la Mungu, kwa sababu katika neno la Mungu ndipo tunapopata ufahamu wa kumtambua shetani na mbinu zake vile vile namna ya kumdhibiti.
- kama mimi si msomaji wa Biblia, vile vile sina muda wa kukaa chini na kusikiliza neno la Mungu mahali popote ni vigumu mimi kuyaishi maisha ya ukweli, kwa sababu maisha ya ukweli yanamhitaji mkristo aliye ikana nafsi yake na huo ndio ukweli. 
- Matatizo, magonjwa, umasikini na maisha ya tabu vinatukumba sana jamii ya waaminio kwa sababu tunaishi nje na kanuni/mfumo wa Roho Mtakatifu, ndio maana walokole wanaishi maisha ya taabu sana. 
- Nikiwa ninaishi nje na mfumo wa Roho Mtakatifu lazima kila janga litafanya ndani mwangu ni kituo, kwa hiyo ili niweze kuliepuka hili inatakiwa nianze kufanya jitihada za kutafuta ufahamu wa neno la Mungu ili ndani ya neno nipate mbinu za kukabiliana na changamoto za majaribu. 
- Mfano mzuri ni Paulo mtume alipo fika korinto aliliona kanisa la korinto likisali nje ya mfumo wa Roho Mtakatifu, (1Kor 3:1- 7 )

MBINU ITAKAYO NISAIDIA KUSHINDA KINACHO NISHINDA 
- Mbinu itakayo nisaidia kushinda kinacho nishinda, ni kuyaruhusu maisha yangu  yaongozwe na Roho Mtakatifu.
- 1.Kushinda kinacho nishinda, ni kumwachia utawala Roho Mtakatifu. 
ANGALIZO NO. 1
- Asili inanyonya nguvu za Mungu katika maisha ya mtu, kwa hiyo ili niweze kuizibiti hii lazma Roho wa Mungu aliyeko ndani mwangu nimlishe ashibe na Roho wa Mungu anakula katika njia tatu:-
a). Kusoma Biblia mara kwa mara yaani asubuhi mchana na jioni, sawa sawa na neno la Yoshua 1:8 kitabu hiki cha Torati kisitoke kinywani mwako bali yatafakari maneno yake mchana na usiku,upate kuangaia kutenda sawa sawa na maneno yote yaliyoandikwa humo, maana ndipo utakapoifanikisha njia yako kisha ndipo utakapositawi sana. 
-( Nikisha kuwa na uwezo wa kumtunza Roho Mtakatifu bila kumnajisi nimefanikiwa njia zangu)
b). Kulisikiliza Neno la Mungu mara kwa mara yaani kuhudhuria vipindi vya mafundisho kanisani, hata hili jambo limeelezwa pia kimaandiko (Mithali 4: 20-21)
c). Kusali na kufunga, jambo hili hata Biblia imelielezea kwa undani (Mathayo 17:21)
- Hakuna asili inayoweza kumshinda mtu mwenye bidii ya kufunga na kuomba kwenye uso wa  Mungu.

Ufafanuzi wa kipengele (a) Kusoma Biblia mara kwa mara:-
- Kama Biblia inasema niyatafakari maneno ya Mungu mchana na usiku, basi kila neno ninalo lisikiliza inatakiwa niliwekee mwendelezo yaani kwa maana zaidi nilitendee kazi au niliweke katika vitendo ndipo kufanikiwa kwangu kutakuwa  dhahiri. 
- Maisha ya mwamini anayemtegemea Yesu Kristo yatazidi kustawi kiroho na kimwili kama mwamini ataruhusu hali ya mwendelezo wa kujifunza Biblia katika maisha yake. 

Ufafanuzi wa kipengele (b) Kusikiliza neno la Mungu mara kwa mara.
- Mithali 4:20 na 21 ni picha wazi kwamba kusoma Biblia ni sehemu ya moyo wa mtu kusikiliza neno la Mungu, kwa hiyo nikitambua hilo kama mwamini ninaye mtafuta Mungu inatakiwa niongeze juhudi zangu katika kusoma Biblia muda wote kama inawezekana. 
- ( Kusoma Biblia kunaleta ujasiri katika moyo wa mkristo )
- Kusoma Biblia kunamvuvia mwamini nguvu za kiroho, kwa sababu unapoingia kwenye kuomba una hoja yenye nguvu. 

Ufafanuzi wa kipengele (c) Kusali na kufunga:-
- Yesu Kristo alitoa mwongozo wa kusali na kufunga kwa sababu ndo njia pekee itakayo msaidia mwamini kuvuka kwenye kipindi cha ugumu wa majaribu bila kuathirika kiroho. 
- Na siku zote majaribu yanamuogopa mwamini anayefunga na kuomba kwa sababu kufunga na kuomba kunamwongezea mwamini nguvu za kiroho, kwa hiyo nikilifahamu hilo inatakiwa nilifanye kuwa ni sehemu ya maisha yangu.  

2. Mbinu ya pili itakayo nisaidia kushinda kinacho nishinda:- Maelezo
- Maisha ya haki anayoweza kuishi mwamini mara nyingi ndio yanayoweza kuugusa moyo wa Mungu, na jambo hili lilitokea hata maisha ya Nuhu. (Mwanzo 6:8,9)
- Maisha ya haki nitakayo ishi leo ndiyo yatakayo mshawishi Mungu kunifungulia milango ya kubarikiwa.
Itaendelea wiki ijayo.............




Hakuna maoni: